30/07/2025
Mchambuzi wa masuala ya siasa, Paternus Niyegira, amesema kuna somo la kujifunza kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), hasa katika kipindi cha uchaguzi.
“Cha kujifunza kwenye CCM ni ule umoja na mshikamano linapokuja suala la uchaguzi. Tumeona vyama vingine uchaguzi ukifika wanafarakana, na hata baada ya uchaguzi mfarakano unaendelea,” amesema Niyegira.
Alikuwa akizungumza katika mahojiano kwenye kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC1 leo Julai 31, 2025.
Ameongeza kuwa CCM imekuwa na neema ya kuelewa kwamba hata wakitofautiana ndani kwa ndani, huungana kwa haraka hasa pale wanapoona hatari ya kupoteza madaraka.
“Wanapokuwa kwenye uchaguzi, hata wakikosana au wakianza kuwa na wasiwasi kwamba wanaweza kupoteza madaraka, huamua kushikamana,” amesema Niyegira.