30/08/2024
Assalam alaykum warahmatullah..
U hali gani ndugu?
Huenda wewe ni miongoni mwa watu wanao struggle kuamka kusali Tahajjud..
Umeset alarm, lakini wapi..🤦🏽♂️
Umejitahid ulale mapema, wapi wee..🤦🏽♂️
Ukamuomba hadi mtu akuamshe, ase kwan uliamka basi..😄
Ikiwa huyu ni wewe basi shuka nami nikueleze mambo 5 ya kufanya ili uweze kuamka usiku na kumuomba Allah..
1. Lala ukiwa twahara (wudhu), na utakapolala ukiwa na wudhu utapata Faida ya kuomba na malaika pindi utapopatwa na usingiz hadi utakapoamka na kutokana na hilo itakuwa rahisi kwako kuamka..
2. Weka Nia ya kuamka usiku kuswali, Na hakika penye Nia, Pana njia. Utakapokusudia kuamka usiku, itakuwa vyepesi kwako kuamka usiku na pia hata usipoamka utalipwa na Allah kwa Nia yako ya kuamka
3. Jitahidi Usile Sana usiku, Usile hadi ukashiba. Kumbuka shibe ni mwana malevya😄. Ukishiba sana utalewa na utashindwa kuamka usiku kuswali..
4. Ikiwa utapata nafasi mchana, pumzika kidogo lala. Ili kuupa mwili nguvu ya kuamka usiku..
5. Jiepushe na maradhi ya Moyo k**a vile chuki, hasadi, unafiki, kusengenya watu katika moyo wako, kuwadhania watu vibaya moyoni mwako, kuwasema watu vibaya moyoni mwako n.k.
Kwan ukiwa na tabia hizo moyo wako utakuwa mzito na utashindwa kuamka kuswali Tahajjud.
By the way, ikiwa unahitaji kujifunza zaidi na kupata ukumbusho na mawaidha kutoka kwangu kwa njia ya WhatsApp bonyeza hapo
https://bit.ly/3Mx7IPH
Al Akh. Mubaarak