24/02/2026
Alishika namba 1 kitaifa matokeo ya mitihani Kidato cha sita mwaka 2006, Elias Kihombo pichani aliyesoma PCM alipata division 1.3 akiwa na A za juu katika masomo yote kuliko wanafunzi wengine wote wa michepuo mingine kitaifa. Alihitimu secondary ya Tosamaganga.Huyu jamaa alihitimu kidato Cha nne na alipataga 1.14 hapo hapo tosamaganga akiwa na Mabanda A za physics na Chemistry huku akipata B kwenye Mathematics na Biology hivyo hakuna aliyewaza kuwa huyu Comrade angekuwa T.O 2006 kwa kupata alama za juu zaidi.
Baada ya form six alijiunga na University Of Dar es salaam(UDSM) alichukua BSc In Telecommunication Engineering(4yrs) lakini ikiwa imebaki miezi michache kabla hajahitimu inaelezwa ali-disco katika hali ambayo imewaacha wengi na maswali vichwani
Hata hivyo, mitandaoni wengi waliosoma michepuo ya PCM na PCB wanamsifu sana Elias Kihombo kwamba alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kufundisha hasa Physics hata maswali magumu yaliyo watatiza wengi bila yeye kushika kitabu. Ali-solve maswali Kwa njia wanayojua wengi kisha wanasema alikuwa akitumia njia nyingine k**a tano wasizozijua au za kwake halafu jibu linakuja lilelile
Elias Kihombo alizunguka katika shule nyingi kongwe na maarufu za secondary zenye wanafunzi wanaotajwa kuwa na vipaji maalum aliwasaidia, alijaza watu wengi sana katika tuitions zake wanafunzi waliambiana akija wasikose kwenda. Imeeleza hata kabla hajahitimu degree yake ya kwanza tayari alitunga vitabu vyake vya Physics ambavyo viliuzika sana
Baada ya ku-disco UDSM, inaelezwa takribani miaka nane baadaye alirudi tena kuanza upya kusoma BSc In Petroleum Engineering ila kabla ya kuhitimu alifar!ki dunia 2020
Kwa siku kadhaa sasa, mitandaoni Elias Kihombo posts kumhusu zinasambaa sana wengi waliopitia mikononi mwake katika somo la Physics wakimtaja kwamba bila shaka yeye ndie Tanzania One maarufu zaidi na genius zaidi kuwahi kutokea Bongo. Inaelezwa shule nyingi za secondary zilitaka kumpa ajira ya kudumu kufundisha ila alikataa ili kufanya ziara zake za kufundisha tuition shule mbalimbali nchini
Nini mtazamo wako, kuna T.O mwingine mkali zaidi kumzidi Elias Kihombo?
:
Follow
:
๐น๐ฟ ๐น๐ฟ