01/09/2026
π₯ BILIONEA WA NIGERIA ASHUKA MITAANI LAGOS KUHUBIRI INJILI YA YESU KRISTO
Picha na video za mfanyabiashara bilionea wa Nigeria, Dr. Cosmas Maduka, zikimuonyesha akihubiri Injili ya Yesu Kristo mitaani jijini Lagos, zimeendelea kuvuta hisia za watu kwenye mitandao ya kijamii.
Maduka ni mwanzilishi na Mwenyekiti wa Coscharis Group, kampuni kubwa ya Nigeria inayojihusisha na sekta mbalimbali ikiwemo magari, uzalishaji, kilimo na biashara nyingine.
Licha ya nafasi yake kubwa katika ulimwengu wa biashara na mafanikio yake ya kifedha, Maduka amekuwa akijulikana kwa kuweka wazi imani yake ya Kikristo na kushiriki katika shughuli za uinjilisti.
Katika video hiyo, mfanyabiashara huyo anaonekana akiwa ameshika Biblia na kipaza sauti, akiwafikishia watu ujumbe kuhusu Yesu Kristo, huku akiwa na mkalimani anayemsaidia kutafsiri ujumbe wake kwa lugha ya Yoruba.
Maduka amewahi kueleza kuwa kuhubiri hadharani si jambo jipya kwake, akisema amekuwa akifanya evangelism kwa muda mrefu. Video za aina hiyo ziliwahi kusambaa kwa kiasi kikubwa mwaka 2019, na baadaye tena mwaka 2024, zikizua mijadala kuhusu namna anavyoweka wazi imani yake licha ya kuwa mmoja wa wafanyabiashara wenye mafanikio makubwa nchini Nigeria.
Kinachowagusa wengi si utajiri wake pekee, bali ni kitendo cha mtu mwenye hadhi kubwa katika ulimwengu wa biashara kushuka mitaani na kuzungumza moja kwa moja na watu kuhusu imani yake, badala ya kuishia kwenye majukwaa makubwa au ndani ya makanisa pekee.
Kwa Maduka, mafanikio ya kifedha na imani ya Kikristo vinaweza kwenda pamoja, huku uinjilisti ukiwa sehemu ya maisha yake ya hadharani.
π SWALI KWAKO: K**a ungekuwa na utajiri mkubwa k**a Dr. Cosmas Maduka, ungekuwa tayari kushuka mitaani na kuwahubiria Yesu Kristo watu usiowajua?
Nigeria Lagos GospelToTheNationsTZ