MOKO TV

MOKO TV Karibu Mwelesi Tv kwa habari, Simulizi, Burudani, Filamu na matukio mbalimbali

Salaam za Eid Mubarak                              @
05/06/2019

Salaam za Eid Mubarak





@

MICHUANO YA VINGUNGUTI SUPER CUP 2019 YAJA KIVINGINEKamati ya maandalizi ya michuano ya Vingunguti Super Cup leo tarehe ...
26/05/2019

MICHUANO YA VINGUNGUTI SUPER CUP 2019 YAJA KIVINGINE

Kamati ya maandalizi ya michuano ya Vingunguti Super Cup leo tarehe 26 imekutana na wawakilishi wa timu mbalimbali katika kikao cha kwanza ili kuthibitisha ushiriki wao katika msimu huu wa 2019/2020

Michuano hiyo itakayofanyika katika uwanja cha Msikate Tamaa imejizolea umaarufu mkubwa katika kata ya vingunguti na maeneo ya jirani, inatarajiwa kuanza kutimua vumbi katikati mwa mwezi wa sita ambapo timu 48 zinategemewa kushiriki

Mkurugenzi wa michuano hiyo Bw. Spear Mbwembwe akiongea na waandishi wa habari, ametaja zawadi za washindi kwa msimu huu, ambapo mshindi wa kwanza atazawadiwa gari aina ya Noah pamoja na pea 20 za viatu, huku mshindi wa pili atakabidhiwa gari aina ya Noah vox wakati mshindi wa tatu atakabidhiwa pikipiki

Lakini k**a vile haitoshi timu zitakazofanikiwa kuingia 16 bora zitapewa jezi za kuchezea mashindano, pia mfungaji bora na mchezaji bora kuzawadiwa zawadi mbalimbali zikiwemo traki suti juu na chini, jezi pamoja na viatu huku golikipa bora atazawadiwa groves na traki suti

Pia Bw. Spear Mbwembwe amesema, mbali na kuboreshwa kwa michuano hiyo katika msimu huu, pia ameziomba taasisi, mashirika, makampuni pamoja na wadau mbalimbali kujitokeza katika kudhamini michuano hiyo ili kuweza kuwatia moyo vijana na kuinua vipaji vyao.

"Michuano ya mwaka huu ina utofauti mkubwa sana na mwaka jana, mwaka huu zawadi zimeboreshwa, mtindo wa kuendesha ligi umeboreshwa na tunatarajia katika kikao cha pili kuweza kuzipitia kanuni zote za michuano hii. Hivyo tunaomba mashirika, makampuni na wadau mbalimbali waje kudhamini hii michuano ili kwa pamoja tuweze kuwatia moyo vijana katika kuinua vipaji vyao"

Eidha Spear Mbwembwe amezishukuru timu zilizoweza kujitokeza leo katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Itungi Lodge uliopo Vingunguti huku akizitaka timu nyingine kujitokeza katika kikao cha pili kitakachofanyika jumapili saa tano asubuhi katika ukumbi huo.

DKT. MSOLLA MWENYEKITI MPYA YANGA SCKlabu ya Yanga imemchagua Dkt. Mshindo Msolla kuwa mwenyekiti wake huku Fredrick Mwa...
05/05/2019

DKT. MSOLLA MWENYEKITI MPYA YANGA SC

Klabu ya Yanga imemchagua Dkt. Mshindo Msolla kuwa mwenyekiti wake huku Fredrick Mwakalebela akishinda katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti.

Katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Bwalo la Polisi Oysterbay Dar es salaam, Dkt. Msola amepata kura 1,276 akimshinda mpinzani wake Dkt. Jonas Tiboroha aliyepata kura 60.

Katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Mwakalebela amepata kuara 1,206 akiwashinda Janneth Mbene aliyepata kura 61, Titus Osoro aliyepata kura 17, Yono Kevela aliyepata kura 31 na Chota Chota aliyepata kura 12.

Walioshinda kwenye nafasi za ujumbe wa Kamati ya Utendaji na idadi ya kura zao ni.

1. Hamad Islam - 1,206
2. Eng. Mwaseba - 1,174
3. Dominick Ikute - 1,088
4. Kamugisha Kalokola - 1,072
5. Arafat Haji - 1,024
6. Salum Ruvila - 976
7. Saad Khimji - 788
8. Rodgers Gumbo - 776.

WAJANE VINGUNGUTI WAULA,  VIJANA WAASWA KUACHA KUBETIDar es Salaam Manispaa ya Ilala imetangaza kukiteua kikundi cha waj...
05/05/2019

WAJANE VINGUNGUTI WAULA, VIJANA WAASWA KUACHA KUBETI

Dar es Salaam

Manispaa ya Ilala imetangaza kukiteua kikundi cha wajane kilichopo kata ya Vingunguti kuwa mabalozi katika kata zote 36 zilizopo Manispaa hiyo kwa ajili ya kutoa hamasa katika vikundi vyengine.

Kauli hiyo imetolewa mapema leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Meya wa Manispaa hiyo ambae pia Diwani wa kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto wakati akizungumza na wanachi wa kata hiyo katika mkutano wa uhamasishaji wa mikopo ya Halmashauri.

Amesema kuwa, wajane hao wamekua mfano wa kuigwa katika Manispaa hiyo, kutokana mafanikio waliyoweza kuyapata yaliojengwa na umoja wao hali iliyoivutia Manispaa hiyo kuweza kuwateuwa kuwa mabalozi wa kuhamasisha wenzao ili waweze kuondokana na hali duni ya umaskini.

Aidha, amewataka vijana wa kata hiyo kuacha tabia ya kucheza michezo ya bahati nasibu (kubeti) badala yake wachangamkie fursa ya mikopo ya Manispaa inayotolewa bila riba ili waweze kujikwamua na umaskini.

Hata hivyo, amesema Vingunguti wanaimani kubwa na Jeshi la Polisi hivyo amewataka wafanye kazi kwa uadilifu ili waweze kuwalinda raia na mali zao na sio kuwaachia askari vidole kuwaumiza wananchi kwa kuwapiga pamoja na kuwachukulia pesa zao kihadaa.

Katika hatua nyengine, Kumbilamoto amekabidhi msaada wa vifaa vyenye thamani ya shilingi 920,000 ikiwemo Feni 3 kwa kikundi cha wajane pamoja na TV moja kwa kituo cha jeshi la polisi ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM ).

18/04/2019

Mvua ya muda mfupi iliyonyesha leo tarehe 18/04/2019 yasababisha nyumba mbalimbali kujaa maji na kusabisha kuharibu vitu mbalimbali huku barabara nyingi kush...

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when MOKO TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to MOKO TV:

Share

Category