18/09/2026
Jacqueline Moussa, anayefahamika pia kwa jina la Jackie, alilelewa katika familia ya Kiyahudi yenye misingi ya kimila kabla ya kusilimu na kuingia katika Uislamu mwaka 2011
Taarifa kuhusu safari yake ya kusilimu zimekuwa zikichapishwa mtandaoni kwa miaka kadhaa, ikiwemo katika makala zilizohifadhiwa kwenye tovuti k**a The Religion of Islam. Katika simulizi yake, Jackie ameeleza kuwa Uislamu uliendana kwa kiwango kikubwa na mantiki, maadili na misingi ya maisha aliyokuwa akiamini.
Kuhusu kauli inayosambaa mitandaoni kwamba alipata “heshima kubwa katika Uislamu,” kauli hiyo imekuwa ikitumiwa katika machapisho na video mbalimbali za mitandao ya kijamii, hasa katika kusimulia uzoefu wa wanawake waliosilimu. Wanawake wengi wanaotoka katika dini nyingine na kuingia katika Uislamu pia wamekuwa wakieleza hadharani namna walivyohisi kupata heshima, kuthaminiwa na uwazi wa kimtazamo baada ya kuujua Uislamu.
Assalaamu Alaikum Warahmatullaahi Wabarakaatuh
Mtume Muhammad ﷺ amesema: “Mwenye kumjengea Allah msikiti, Allah atamjengea nyumba mfano wake Peponi.” (Bukhari na Muslim).
Hii ni fursa adhimu ya kushiriki katika kujenga na kukamilisha Nyumba ya Allah iliyopo Utengule, Wilaya ya Kilolo, Mkoa wa Iringa. Kila tofali, mfuko wa saruji, mchanga, kokoto au shilingi utakayotoa kwa ajili ya ujenzi huu ni sehemu ya Sadaka Jariyah, ambayo thawabu zake zinaweza kuendelea kunufaisha waumini hata baada ya maisha yetu duniani.
🤲🏽 Usidharau kidogo unachoweza kutoa. Huenda kile kidogo unachokitoa kwa ikhlasi kikawa sababu ya kupata malipo makubwa kutoka kwa Allah سبحانه وتعالى. Tushiriki katika ujenzi wa Nyumba hii ya Allah kwa kadiri ya uwezo wetu, ili iwe sehemu ya kuswali, kumdhukuru Allah na kuwafundisha vizazi vijavyo.
Kwa anayependa kushiriki, unaweza kutuma mchango wako kupitia
M-PESA: 0769 756 490,
YAS | MIX: 0715 868 990,
HALOPESA: 0619 115 190.
Jina: MUDATHIR ISSA YOYOTA.