Yuston Tv

Leo ni kumbukizi ya kifo cha Hayati John Pombe Magufuli na imetimia miaka minne sasa toka kufariki kwake.Aendelee kupumz...
17/03/2025

Leo ni kumbukizi ya kifo cha Hayati John Pombe Magufuli na imetimia miaka minne sasa toka kufariki kwake.

Aendelee kupumzika salama uko alipo,

Kitu gani ukiona unamkumbuka sana Magufuli?

02/11/2024
Hivi sasa, watangazaji wamepoteza ubunifu au ni kiki tu?maana sielewi kwa nini kila wanapopata nafasi ya kumhoji mtu wan...
12/09/2024

Hivi sasa, watangazaji wamepoteza ubunifu au ni kiki tu?
maana sielewi kwa nini kila wanapopata nafasi ya kumhoji mtu wanauliza swali lilelile kila siku. Mfano mzuri ni majuzi ambapo Mavoko alitoa nafasi kwa baadhi ya vyombo vya habari kufanya mahojiano naye. Nilifuatilia, na asilimia kubwa ya waandishi walimuuliza maswali aliyokwisha yajibu miaka 6 iliyopita, hasa kuhusu kuondoka kwake WCB. Hakuna aliyejaribu kuuliza kitu kipya ambacho kingemfanya azungumzie kazi zake za sasa. Hivi majuzi aliachia wimbo akiwa na Chino, lakini bado maswali yalikuwa yanafanana. Je, hii ni ishara ya kuwa na watangazaji wengi wasio na ueledi au ni ukosefu wa ubunifu?

"Enzi za uhai wake Kanumba aliniambiaga mama wewe kaa kula matunda yangu, kula mshahara wako kwasababu umeteseka sana ku...
12/09/2024

"Enzi za uhai wake Kanumba aliniambiaga mama wewe kaa kula matunda yangu, kula mshahara wako kwasababu umeteseka sana kunilea mimi ndio dada ndio kaka, acha nikuhudumie. Alikuwa hapendi nijulikane wala nisiisogelee camera ndio maana hakuna mtu aliyekuwa ananijua kipindi hicho"

"Lakini haikuwa hivyo, wakati yeye anapanga kumbe Mungu naye kampangia yake, ikabidi nianze kuigiza ili nipate kujimudu ila k**a mwanangu angekuwepo mpaka leo hii msingekuwa mnanijua maana alikuwa hapendi kabisa nijulikane"- Mama Kanumba, Mwigizaji wa filamu Tanzania.

Toa maoni yako


"Yani kufanya kote kazi na wewe umetumia msemo wangu (We huogopi) umenitumia na mimi unanilipa elfu 50 kweli 😭? Kumbe kw...
25/07/2024

"Yani kufanya kote kazi na wewe umetumia msemo wangu (We huogopi) umenitumia na mimi unanilipa elfu 50 kweli 😭? Kumbe kwenye sanaa kuna dhuluma na dharau kiasi hiki daaah!!!. Nimejitoa sana Watanzania mliona kweli hii ni haki? Msemo wangu uibiwe na video vifanye bure kweli?"- Suzi Bale amlalamikia Msanii wa muziki Phina.

Toa maoni yako

Jennifer Lopez (Jlo); licha ya umri kuonekana kuanza kumtupa mkono lakini bado ni mrembo ingawa moja sifa yake kubwa amb...
03/07/2024

Jennifer Lopez (Jlo); licha ya umri kuonekana kuanza kumtupa mkono lakini bado ni mrembo ingawa moja sifa yake kubwa ambayo siyo nzuri ni kwamba Staa huyu ni mbinafsi, muda mwingi anaonekani amekunja uso hana furaha, hazoeleki kirahisi.

Sio rahisi kukuta shabiki anamkimbilia kumuomba kupiga selfie kwasababu walishaomba wakachoka bila matumaini mwisho wakaamua kumchukulia k**a alivyo. Kawaida imezoeleka mastaa wakubwa wakienda mahali palipo na waandishi wa habari lazima wawapungie mikono lakini kwake hiyo haipo ni mtu wa siriasi muda wote.

Address

Mwenge
Dar Es Salaam

Telephone

+255624591513

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Yuston Tv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category