18/05/2024
Jerry William Silaa alizaliwa Februari 9, mwaka 1982, akipata bahati ya kuzaliwa katika familia ya rubani wa ndege 'Captain' Wiliam Slaa, aliyefariki kwenye ajali ya ndege iliyochukua pia uhai wa aliyekuwa Mbunge wa Ludewa Mhe. Deogratius Filikunjombe.
Mhe. Slaa ni mwanasiasa, ambaye Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, alimteua Agosti 30, na kuapishwa Septemba Mosi mwaka jana kuwa Waziri wa Aridhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Baada ya siku 100 za utendaji wake kwenye wizara hiyo Mhe. Slaa, alifanya kikao na Makamishina wa Ardhi Wasaidizi mikoa yote Tanzania Bara kutathmini siku 100 za uongozi wake tangu ameanza kuiongoza wizara hiyo.
Siku 100 za utendaji kazi wa Mhe.Jerry Slaa alifanya tathimini kutengeneza mpango wa kutekeleza maagizo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutatua matatizo ya migogoro ya ardhi na kuwahudumia wananchi wa taifa hili.
Ndani ya utendaji wake akiwa Waziri wa ardhi Mhe. Slaa ameweza kufanya mambo makubwa ambayo yalihitaji ujasiri mkubwa, ambayo hayakuweza kufanywa kwa miaka mingi ikiwepo mpango wake wa kuanzisha kile alichokiita kliniki ya changamoto za ardhi.
Katika kile kinachoelezwa kuwa Mhe.Slaa ameweza na atakuwa msaada na mtaji mkubwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kuonesha kuwa kiongozi anayesimamia ipasavyo haki na sera za chama chake na maagizo ya Mhe. Rais Samia.
Mhe. Slaa akionesha kuwa yuko katika kutetea maslahi na haki za wananchi wangonge wa taifa hili, alikataa kujiita kuwa yeye ni mtoto wa maskini ili kuwaziba midomo wale mafisadi wanaohisi kuwa wanaweza kutumia mwanya huu kumuhongo ili apindishe haki.
Mhe. Slaa ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ukonga, hivi karibuni, alikataa rushwa ya Tsh milioni 300 kutoka kwa tajiri mmoja aliyejenga kituo cha Mafuta Kinyume cha utaratibu pale Mikocheni.
Mhe. Slaa alidhihirisha ukomavu na utendaji wenye ujasili baada ya kuchukua maamuzi magumu ya kusimamia nyumba ya ghorofa moja iliyokuwa kwenye eneo la kiwanja no. 484 Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Slaa alisimamia zoezi la ubomoaji wa nyumba hiyo, inayodaiwa mmiliki wake hakuwa na nyaraka za umiliki wa eneo hilo na pia hakua na kibali cha kujenga hapo na kwamba alivamia eneo hilo ambalo linamilikiwa na Bi. Naomi Raymond ambaye anadaiwa kulipigania eneo hilo kwa takribani miaka 20 sasa.
Sakata la mgogoro huo limedumu kwa takribani miaka 20, ambapo limepita katika ngazi mbalimbali za Serikali na Mahak**a na hatimaye kutolewa uamuzi na waziri Jerry Slaa kwa muda mfupi wa uongozi wake kwenye wizara hiyo.
Kabla ya kuanza majukumu yake ya kazi katika wizara hiyo Mhe. Jerry Slaa alitaka ushirikiano kutoka kwa watumishi wa wizara hiyo kwa kuweka vipambele vyake vikiwemo kutekeleza maagizo ya Rais Samia kuhusu kuondoa changamoto za ardhi nchini.
Katika kuendeleza utendaji wenye kasi kutatua changamoto za ardhi, Mhe. Slaa aliwahi kutoa siku saba kupatikana suluhu ya changamoto za urasimishaji makazi holela wa makazi katika mkoa wa Dar es Salaam.
Agizo la Waziri Slaa lilfuatia kwa mkoa wa Dar es Salaam kuwa moja ya mikoa yenye malalamiko mengi ya urasimishaji makazi holela zoezi ambalo lilianza mwaka jana na kutarajiwa kukamilika mwaka huo.
Mhe. Slaa alitoa tamko hilo Oktoba 4, mwaka jana
alipokutana na uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam na watendaji wa sekta ya ardhi kujadili utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa upande wa sekta ya ardhi.
Pamoja na hatua iliyokuwa imefikiwa kwenye urasimishaji, utekelezaji wa programu ya urasimishaji wa ardhi mkoa wa Dar es Salaa, Slaa aliziona changamoto mbalimbali ikiwemo makampuni yaliyopewa kazi hiyo kushindwa kukamilisha kwa wakati huku wananchi wakikosa imani kwa makampuni na kuacha kuhangia gharama za utekelezaji kazi hiyo na kusababisha zoezi hilo kukwama katika maeneo mengi.
Kwa mujibu wa Waziri Silaa, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amemteua na kumuamini afanye kazi ya ardhi na yeye ameamua kufanya hivyo ili kupunguza k**a siyo kuondoa kabisa kero za ardhi nchini.
Tunamuomba Mungu ampe afya njema waziri Slaa ili aweze kuendelea na kasi ya utendaji ambayo watanzania wanahitaji kuondokana na kero nyingi zilizoko kwenye sekta ya ardhi.
Kupata taarifa za uchunguzi, uchambuzi, siasa, uchumi, jamii, utamaduni na michezo bofya link hapo chini
https://www.tanzaniampya.co.tz/