02/01/2026
Kwa mujibu wa KUTV 2 News, rapa wa Marekani NBA YoungBoy alisimamishwa na polisi katika jimbo la Utah, Marekani. Inaripotiwa kuwa kulikuwa na mwanamke ndani ya gari wakati polisi walipolisimamisha.
Polisi walikuwa na sababu ya kisheria (probable cause) ya kulisimamisha na kulikagua gari hilo, ambapo walikuta na kuk**ata dawa za kulevya. Hata hivyo, licha ya kuk**atwa kwa dawa hizo, NBA YoungBoy hatakabiliwa na mashtaka kuhusiana na tukio hilo.
Ikumbukwe kuwa hapo awali, NBA YoungBoy aliwahi kutumikia kifungo cha zaidi ya miezi 18 gerezani kwa makosa ya kumiliki silaha kinyume cha sheria, kabla ya kusamehewa na aliyekuwa Rais wa Marekani, Donald Trump.
✍️: