09/08/2026
🚨😂 HILI TAMASHA LA YANGA DAY SILIELEWI JAMANI!
Nasikia tu “WANANCHI! WANANCHI! WANANCHI!” kila baada ya muda mfupi 😂😂 lakini ukikaa chini kutafuta kile kinachofanya hii siku iwe special, unajikuta unauliza… “Au mimi ndiye nimewahi kuwasha TV?” 🤣
Maana mpaka sasa naona kelele zimefika dakika za nyongeza, lakini tukio lenyewe bado sijaliona! 😂😂
Kila nikidhani sasa ndiyo mambo yanaanza, naambiwa “Wananchi…” 😭
Sawa tumewaona Wananchi, tumewasikia Wananchi, tumewahesabu Wananchi… lakini sasa wananchi wamekuja kufanya nini? 🤣🤣
Au labda Yanga Day ina mfumo wa kusubiri? 😂
Huenda mimi nina haraka sana, wakati wao wanajua kwamba mambo mazuri yanakuja 😅🔥
Basi ngoja nivute subira kidogo… maana sitaki kesho niseme nilihukumu mapema wakati kitu kikubwa kilikuwa kinapikwa jikoni 😂😂
Lakini kwa sasa, nisameheni tu… hii tamasha nimeiona k**a trailer ndefu sana ambayo bado haijafika kwenye movie yenyewe! 🤣🤣🤣
Tunasubiri… ⏳😂
Labda baada ya “Wananchi! Wananchi!” mara mia, ndipo tutafika kwenye “Alichokifuata mwananchi” 😂🔥
Yanga Day bado inaendelea… tusikimbilie hukumu.
Huenda mwisho wake wakatuacha tumefumba midomo kwa mshangao. 😅
Lakini k**a mwisho wa siku hakuna kitu cha maana… basi tutakaa pembeni na kusema:
“Tuliona mapema, ila mlituambia tuvute subira.” 😂😂😂