Agape Television Network ( ATN )

Agape Television Network ( ATN ) TWITTER: https://twitter.com/ATN_TZ
YOUTUBE: https://www.youtube.com/ ATN is the Educational and Inspirational Channel in Tanzania.

ATN has 9 stations all over the country and very wide coverage. The stations are located in: Dar-es-Salaam, Morogoro, Arusha, Tanga, Dodoma, Mwanza, Kigoma, Sumbawanga, Mbeya. Agape Television Network (ATN) the Educational and Inspirational Channel in Tanzania since September 15, 2001. Education in all areas are the most crucial part of this network. Since its inception till today various programs

from religious to secular education is being produced and broadcasted through out. Programs such as: Newspapers reading on headlines which is being rebroadcasted via other radio stations in Tanzania everyday is a program in demand. Local and International news programs, sports, music, education on women, men, youth, various discussion programs, religious education, children's programs, matters arising, programs, movies etc are part of their packages. Any organization or institution who wishes to use ATN to educate in any area are welcome to use this media channel.

Ibada Ya Jumapili Kanisani Ilioongozwa na Askofu Steven Saro Kanisani Mbezi Beach Jogoo Hakika Ilikua Ni Ya Kubarikiwa s...
21/09/2025

Ibada Ya Jumapili Kanisani Ilioongozwa na Askofu Steven Saro Kanisani Mbezi Beach Jogoo Hakika Ilikua Ni Ya Kubarikiwa sana. Tunapenda Kuwakaribisha Katika Ibada Zetu Kani Sani Kwetu Na Mungu Awabariki

21/09/2025
21/09/2025

Shaloom,
Kanisa la Agape Life Church Mbezi beach Jogoo linapenda kukukaribisha ibadani tumsifu na kumwabudu MUNGU kwa pamoja, karibu sana na MUNGU akubariki.
UJUMBE: JE UNAMPENDA YESU

Klabu ya Simba SC kwa kushirikiana na mzabuni wake, Jayrutty Investment East Africa Ltd, umetangaza kugundua jezi feki z...
19/09/2025

Klabu ya Simba SC kwa kushirikiana na mzabuni wake, Jayrutty Investment East Africa Ltd, umetangaza kugundua jezi feki za klabu yao zilizokuwa zikisambazwa katika mikoa ya Morogoro, Singida, Mwanza na Geita. Operesheni iliyoshirikisha Jeshi la Polisi imefanikisha kuk**atwa kwa baadhi ya wahusika, ambao wanakabiliwa na hatua kali za kisheria.
Simba imeonya kuwa uzalishaji, usambazaji na matumizi ya jezi au bidhaa zisizo rasmi ni kosa la jinai na madai, na imeahidi kuweka ulinzi mkali nchi nzima kudhibiti tatizo hilo.
Wanachama na mashabiki wametakiwa kuripoti taarifa za jezi feki Polisi au kwa kupiga simu zilizotolewa na klabu, huku ikiahidi zawadi nono kwa watakaosaidia kufanikisha kuk**atwa kwa wahusika.

Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM aki...
19/09/2025

Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM akizungumza na maelfu ya wananchi waliohudhuria kwenye Mkutano wa Kampeni za CCM Nungwi, Kaskazini Unguja Jana Alhamisi Septemba 18, 2025.
Katika hotuba yake Dkt. Samia ameahidi kuendelea kukuza uchumi na kipato cha mwananchi kwa kuendelea kubuni na kusimamia mikakati yake ya kuzalisha fursa za ajira, utoaji wa mikopo, urasimishaji pamoja na elimu ya ujuzi kwa Vijana ili kuweza kuwa na shughuli za kiuchumi na uzalishaji.

Marekani imetumia kura yake ya turufu Alhamisi kuzuia kupitishwa kwa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lil...
19/09/2025

Marekani imetumia kura yake ya turufu Alhamisi kuzuia kupitishwa kwa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililotaka usitishwaji mapigano Gaza, kuwezesha ufikiaji wa misaada ya kiutu na kuachiliwa kwa mateka.
Azimio hilo ambalo rasimu yake ilianza kujadiliwa mwezi Agosti, iliungwa mkono na wanachama wote 14 wa baraza hilo ispokuwa Marekani ambayo ilipendekeza uwepo wa azimio la kibinaadamu pekee.

Lakini kwa mujibu wa duru za kidiplomasia, Ufaransa, Uingereza na Urusi zilitilia shaka faida na ufanisi wa azimio la kibinadamu pekee kutoka kwa chombo kilichoundwa kwa ajili ya kudumisha amani na usalama duniani.

Mwezi Juni, Marekani ilitumia pia kura yake ya turufu kuzuia azimio k**a hilo ili kumlinda mshirika wake Israel. Mwanadiplomasia wa Marekani Morgan Ortagus ametetea uamuzi wa taifa lake akisema azimio hilo halikujumuisha kauli za kulaani vitendo vya Hamas na kuwa limeshindwa kutambua hali halisi na ukweli kwamba kumekuwa na ongezeko kubwa la mtiririko wa misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza.
Hayo yanajiri wakati Israel imeendeleza operesheni yake kubwa ya kijeshi huko Gaza City huku maelfu ya Wapalestina wakiendelea kuondoka katika jiji hilo na kuelekea eneo la Kusini. Mamlaka za Gaza zimesema watu 85 wameuawa ndani ya muda wa saa 24 zilizopita.

Kundi la Hamas limesema limewasambaza mateka wa Israel katika wilaya kadhaa za mji wa Gaza na kwamba mashambulizi ya Israel katika mji huo yatahakikisha kuwa hakuna mateka yeyote atakayerejea Israel.

Ufaransa yakemea upanuzi wa makazi ya walowezi
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema kutambuliwa kwa taifa huru la Palestina ndiyo njia bora ya kuwatenga Hamas. Macron ameitoa kauli hiyo alipohojiwa mjini Paris na mwandishi wa habari wa Israel Yonit Levi huku akikemea pia vitendo vya Israel kutanua makazi ya walowezi:

Hata hivyo, Wiliete Sports Clube inasalia kuwa mpinzani mwenye rekodi kali katika ligi ya Angola, na kuifanya mechi hii ...
19/09/2025

Hata hivyo, Wiliete Sports Clube inasalia kuwa mpinzani mwenye rekodi kali katika ligi ya Angola, na kuifanya mechi hii kuwa na ushindani mkubwa. Yanga SC itahitaji kuonyesha nidhamu kubwa, ukomavu wa kimataifa, na kutumia uzoefu wa nyota wao ili kupata matokeo chanya.

Donald Trump anakutana na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer siku ya leo Alhamisi Septemba 18 katika mazungumzo yanay...
18/09/2025

Donald Trump anakutana na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer siku ya leo Alhamisi Septemba 18 katika mazungumzo yanayolenga kuangazia maswala ya kimataifa katika ziara ya pili ya kitaifa ya kiongozi huyo wa Marekani.
Baada ya siku ya fahari na sherehe ambapo Trump alipanda gari na Mfalme Charles na kusherehekea karamu ya kitaifa hapo jana, rais huyo wa Marekani na Starmer watasherehekea kuzindua kifurushi cha pauni bilioni 150 (dola bilioni 205) za uwekezaji wa Marekani kwenda kwa Uingereza.
Mikataba hiyo, inayohusu maeneo k**a vile teknolojia, nishati na sayansi ya maisha, itautakasa upya 'uhusiano maalum' kati ya mataifa hayo mawili, jambo ambalo Starmer amelifanyia kazi kwa bidii tangu Trump kuwa kiongozi wa taifa la Marekani.
Baadaye leo Alhamisi, viongozi hao wawili watafanya mkutano na waandishi wa habari, wakati waandishi wa habari ambao watapata wasaa wa kuuliza maswali juu ya mkosaji wa ngono, marehemu Jeffrey Epstein. Starmer alilazimika kumfukuza Peter Mandelson k**a balozi wa Marekani wiki iliyopita baada ya uhusiano wake wa karibu na Epstein kurekodiwa na uhusiano wa Trump na marehemu mfadhili pia umechunguzwa.
Awali wakati Trump, akizungumza pamoja na Charles katika Windsor Castle, ngome kongwe na kubwa zaidi inayokaliwa na wengi watu duniani, alielezea ziara yake hiyo k**a mojawapo ya heshima kubwa zaidi ya maisha yake.
Wakati huohuo, Starmer anatumai kuwa maafikiano baina yao hayatabadilika huku akipanga kumzuia kiongozi huyo wa Marekani kuangazia katika maeneo nyeti zaidi ya Uingereza, k**a vile sheria za usalama mtandaoni za Uingereza na msimamo wake kuhusu Israel.
Badala yake, Starmer atataka kutetea mikataba iliyopatikana kati ya nchi hizo mbili, ikijumuisha mkataba mpya wa teknolojia na kampuni kutoka Microsoft hadi Nvidia, Google na OpenAI zikiahidi uwekezaji wa pauni bilioni 31 (dola bilioni 42) katika miaka michache ijayo, katika AI, kompyuta ya quantum na nishati ya nyuklia ya kiraia.

Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu inatarajiwa kuendelea...
18/09/2025

Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu inatarajiwa kuendelea leo Septemba 18, 2025 kwenye viunga vya Mahak**a Kuu, Masjala Ndogo Dar es Salaam baada ya kuahirishwa siku ya Jumanne Septemba 16, 2025.
Mahak**a Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo Dar es Salaam iliiahirisha kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, siku ya Jumanne Septemba 16, 2025 kutokana na wingi wa hoja alizowasilisha msh*takiwa mahak**ani.
Kuahirishwa huko kunatokana na upande wa mashtaka kuomba ahirisho ili kupata muda wa kujipanga na kuandaa majibu ya hoja zilizowasilishwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu.
hoya Mojawapo ya Tundu Lissu ilikuwa ni kuhusu suala la mashahidi, alipodai kuwa hawakufichwa ipasavyo hivyo baadhi ya taarifa zao muhimu kuonekana. Leo, mawakili wa Serikali watakuwa wakijibu hoja mbalimbali zilizowasilishwa na Lissu.

Picha na mikanda ya video imewaonesha wakaazi wa mji huo wakiukimbia kwa kutumia magari yaliyosheheni vifurushi vya mizi...
17/09/2025

Picha na mikanda ya video imewaonesha wakaazi wa mji huo wakiukimbia kwa kutumia magari yaliyosheheni vifurushi vya mizigo ikiwemo magodoro huku wengi wengine wasijue wapi pa kuelekea.

Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz, aliandika kupitia ukurasa wa mtandao wa X kwamba "Gaza inateketea" wakati alipokuwa akitangaza kuanza kwa operesheni hiyo ya kijeshi iliyokosolewa kimataifa.

Mashambulizi makali ya makombora yalisikika kila kona ya Gaza City na vikosi vya jeshi la Israel vilionekana kusonga mbele kwenye viunga vya mji huo.

Operesheni hiyo ya ardhini, ilitanguliwa na mashambulizi mazito ya anga mnamo majuma matatu yaliyopita ambayo kwa sehemu kubwa yaliyaporomosha majengo ya roshani kwenye mji huo.

Mataifa yapaza sauti kukosoa operesheni ya Israel ndani ya jiji la Gaza
K**a ilivyotarajiwa, operesheni hiyoimekosolewa vikali na mataifa mbalimbali, mashirika ya kiutu na makundi ya haki za binadamu.

Address

Mbezi Beach Jogoo
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Agape Television Network ( ATN ) posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category