
30/08/2025
UJUMBE KWA VIJANA π
Vijana wenzangu, mahusiano mazuri yanajengwa juu ya uhalisia na uwezo, siyo mashindano ya nani ana mwanamke mrembo zaidi au nani anatumia pesa nyingi zaidi.
π Chagua mwanamke wa level yako β anayekuelewa, anayekubali hali uliyo nayo na mnaweza kusaidiana. Usijilazimishe kuwa na mtu ambaye maisha yake yako nje ya uwezo wako, mwisho wake ni stress, wivu, na mara nyingine matatizo makubwa k**a ugomvi au hata kufikia kujinyonga.
π Siri ya furaha ni:
Mapenzi ya kweli, sio mashindano
Heshima na mawasiliano
Kila mmoja kushirikiana kujenga mustakabali
Tusipojilazimisha kwenye mahusiano yasiyo ya uwezo wetu, tutapunguza visa vya unyanyasaji, stress na hata jela zisizo na sababu. β¨