
26/05/2024
Ni Baada ya Misa takatifu ya Jumapili ya Tarehe 10 August 2042, Saa 20:08pm jioni Kwa Saa za Africa mashariki, na Saa 16:08pm za pale Ouagadougou nipo nchini Burkna Faso natafakri mema Mungu aliyonitendea. Napiga goti chini na kusema Asante Mungu, Nakushukuru sana Mungu wangu Kwa ulinzi, Afya Bora, Uzima Nakushukuru pia hata kunifikisha hapa.
Wakati namaliza kumsukuru Mungu, Napokea SMS inayonikumbusha Kwenda kumshuhudia Taifa Stars Akibondana na Timu ya Taifa ya Ivory coast "tembo wa africa" Nusu fainali ya michuano ya AFCON 2042 mchezo unaopigwa Katika uwanja wa KI AZIZ Hapa Burkina Faso.
AZIZ KI? kwanini, KI AZIZ? ooooohh Ndipo nakumbuka kuitazama hii picha, Naikumbuka Ile Tarehe 25 May 2024 Naikumbuka hii picha inayonikumbusha uwanja wa Benjamin Mkapa Naikumbuka hii picha Ndio mara yangu ya kwanza kuingia kwenye huo uwanja, nakumbuka ni siku ya PARTY ya KIBINGWA Kwa wananchi, Naikumbuka siku hiyo iliyojaa furaha Kwa wananchi kutoka jangwani
Ndio Naikumbuka Siku hiyo Alikuweko AZIZ KI, Naikumbuka siku hiyo niliingia Benjamin Mkapa Kuitazama jezi ya NICKSON KIBABAGE 30 hiyo namba ilikuwa na wakati mzuri sana Kwa wanajangwani, Nabaki natahamaki!! kuwa mara ya kwanza naingia Benjamin Mkapa nilimuona Ki Aziz badala ya Kibabage30 na Sasa naingia AZIZ KI STADIUM kumtazama kocha Mwamnyeto akiipeleka Taifa stars Fainali.
Kumbukumbu ambayo Haitafutika kwangu ni ahadi ambayo niliwaahidi Ndugu zangu wakati nipo Kenya, msimu huu Mungu akipenda hauwezi kuishi nimeingia Benjamin Mkapa. Kwa kadri Mungu aishivyo Alinibariki siku muhimu na ya kipee Kwa wananchi nami nikawepo Nikashuhudia ubingwa wa 30 wakikabidhiwa baada ya kuipinda Tabora United Goli 3-0 ubao ukapendeza maana ilionekana 30 ukitoa deshi ishara ya ubingwa wa 30.
Ndugu yangu ni ndoto ambayo nimeota Usiku huu mara ya Party ya Jana. Nimejionea mengi siku ya kwanza Benjamin Mkapa, nikajifunza mengi na nitayatendea haki hata siku natoa shuhuda vijana watajifunza Yale napitia Kwa sasa basi kitakuwa faraja kwao, Kukamilisha Yale waliyonayo moyoni.
Asante sana NASALIA KUITWA FRAHINI LEONARD UKIPENDA NIITE FELLA8