Koncept TV

Koncept TV Pata Habari za Hivi Punde/Kitaifa/Kimataifa/Biashara na Uchumi/Siasa, Michezo/Burudani/Teknolojia na Hamasa Whatsapp ; 0658123310



Like Page Upate Uhondo.

Pata Habari za Hivi Punde/Kitaifa/Kimataifa/Biashara na Uchumi/Siasa, Michezo/Burudani/Teknolojia na Hamasa


LIKE PAGE Kisha Tembelea Website Yetu Kupata UHONDO Zaidi

18/07/2025

Aliyekuwa Balozi wa Cuba, Humphrey Polepole, ameweka wazi watu walioenda nyumbani kwa dada yake na kumteka wakimtaka atoe taarifa zake.

18/07/2025

Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba Humphrey Polepole ameeleza kuwa aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ndiye aliyemshauri kuacha programu yake ya Shule ya Uongozi ambayo Polepole alikuwa akiitoa kupitia mtandao kwa kile Ndugai alichodai kuwa ni 'hali ya upepo'.

Polepole ameyasema hayo siku ya ljumaa wakati akizungumza na wanahabari kwa njia ya mtandao akisema kuwa hakuona sababu yoyote ya kuacha programu hiyo.

Hata hivyo haikumchukua muda mrefu kwa yeye kuendelea na jambo lake hilo kutokana na kupangiwa nafasi ya Ubalozi nchini Malawi kutoka kuwa Mbunge wa kuteuliwa.

18/07/2025

Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, linafatilia na kuchunguza tukio la kuvamiwa na kuchukuliwa na watu wasiojulikana wa dada yake Balozi mstaafu wa Cuba, Humphrey Polepole, anayefahamika kwa jina la Christina Polepole (52), mkazi wa Mtaa wa Katumba Bahari Beach jijini Dar es Salaam, lililotokea Jana usiku Julai 17, 2025.

Jeshi limesema dada huyo baada ya kurudishwa nyumbani kwake alifika Leo Julai 18, 2025, alifika kituo cha Polisi Kawe kuripoti tukio hilo.

Mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amejumuika na Watanzania na wadau mb...
17/07/2025

Mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amejumuika na Watanzania na wadau mbalimbali kushiriki hafla ya uzinduzi wa Dira ya Taifa ya 2025-2050 (Dira 2050), iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Mtangazaji wa Wasafifm   ameongelea Sakata la   linaloendelea mitandaoni baada ya mahojiano kuonekana kutokuwa mazuri ka...
17/07/2025

Mtangazaji wa Wasafifm ameongelea Sakata la linaloendelea mitandaoni baada ya mahojiano kuonekana kutokuwa mazuri kati ya watangazaji na msanii.

amedai msanii ana haki kukataa baadhi ya maswali ila watangazaji walipaswa kujua namna ya kumfanya ajibu maswali hayo, vile vile amedai kuwa amemkosea kwa kushindwa kumpa heshima kwani kufanya nae wimbo ndio kumemfanya ajulikane Zaidi.

Ameandika.. " DOGO Alikuwa SawaMSANII ANA HAKI YA KAUKATAA Baadhi Ya Maswali Watangazaji Walipaswa Kuitumia Maswali Ya Mitego ILI Kufanya DOGO Aongelee Shule Bila Kujijua .
Lakini Pia Nilishuhudia MEDIA Kubwa Marekani Ikimuuliza Lukuga K**a KUNA Swali Hataki Kuulizwa Kabla Ya Interview ILI asiulizwe Hewani Au K**a YuponTayati Aulizwe Chochote.

So Wangekaa Na DOGO Before Kuandaa Interview Nzuri.

Mwisho Ni Kwamba Huyo DOGO Nimemsikia Interview Kadhaa Akionyesha Kutokubali Kwamba ZUCHU KUWEKA SAUTI KWENYE WIMBO WAKE Ndio Kumemkuza Zaidi Na Kuuoa WIMBO WAKE NGUVU NA Kubadilisha Maisha Yake Ghafla.
Anapaswa Kuwa Na HESHIMA Na Adabu plus SHUKURANI...!
ZUCHU Amefanya Uli Wimbo Kwa Mapenzi Makubwa Sana Na Kujitoa Mno Kwenye Promotion...!
DOGO Alipaswa Kumshukuru Sana ILI Ikiwezekana Apate Ngoma Nyingine Na Zuu..!
NATAMANI DOGO ANGEJUA BEI YA KUMSHIRIKISHA ZUCHU KWENYE WIMBO NDIO ANGEJUA KWAMBA AMEOKOTA DODO KWENYE MPERA 🙏🙏🙏"

17/07/2025

Msanii Msami ametoa maoni yake kuhusu sakata la Dogo Pateni na Watangazaji wa Mjini Fm ambapo amesema Dogo Pateni amekosea kujibu majibu yale pia umri wake haumruhusu kufanya show maana bado ni mwanafunzi.

17/07/2025

Mwimbaji wa Bongo fleva, Dayoo amempa makavu Dogo Paten kwa kushindwa kujibu maswali ya kuhusu shule katika mahojiano yake na moja ya kituo cha Radio na mahojiano hayo yakasitishwa. Dayoo amesema angekuwa yeye angejibu tu kwani ndiyo kazi ya msanii.

17/07/2025

National Lottery Instore Nationwide Campaign
Proudly executed by Koncept Group in collaboration with our esteemed client .

🎯 Objective:
To increase visibility, retail engagement, and nationwide awareness of the National Lottery brand through strategic in-store activations across Tanzania.

🏆 Achievements:

Successfully activated over 100+ retail locations nationwide

Boosted customer interaction and ticket sales in key regions

Trained and deployed brand ambassadors to drive consumer engagement

Delivered real-time analytics and brand feedback to the client

This campaign reflects our continued commitment to BTL excellence, brand activation, and results-driven marketing.

Kituo cha Afya Mkondogwa kilichopo Kata ya Chamazi, Manispaa ya Temeke, Julai 15, 2025, kimeanza rasmi kutoa huduma za u...
17/07/2025

Kituo cha Afya Mkondogwa kilichopo Kata ya Chamazi, Manispaa ya Temeke, Julai 15, 2025, kimeanza rasmi kutoa huduma za upasuaji.

Katika hatua ya awali, wakina mama wawili wamefanikiwa kujifungua kwa njia ya upasuaji katika kituo hicho, ambapo wote pamoja na watoto wao wanaendelea vizuri kiafya.

Kituo hicho kilijengwa kwa kutumia fedha za mapato ya ndani ya Manispaa na kugharimu shilingi milioni 520 hadi kukamilika kwake.

Uanzishaji wa huduma za upasuaji katika kituo hicho ni hatua muhimu katika kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Mbagala Rangi Tatu, ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikihudumia wagonjwa kutoka maeneo ya Mbagala, Chamazi na kata jirani.

Kituo cha Afya Mkondogwa kina miundombinu kamili inayojumuisha jengo la wagonjwa wa nje (OPD), jengo la wazazi, jengo la upasuaji pamoja na nyumba za watumishi, hivyo kuwezesha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Hatua hii ni sehemu ya juhudi za Serikali katika kutimiza azma yake ya kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora za afya, kwa gharama nafuu na kwa wakati.

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Toangoma, Ndugu David Kulinga, amefariki dunia usiku wa Jumatano, Julai 16, 2025.Mar...
17/07/2025

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Toangoma, Ndugu David Kulinga, amefariki dunia usiku wa Jumatano, Julai 16, 2025.

Marehemu alifariki dunia katika Hospitali ya Alexia iliyopo Kata ya Toangoma, alikokuwa amelazwa baada ya kuugua ghafla.

Ndugu David alikuwa miongoni mwa waliotia nia kugombea nafasi ya Udiwani Kata ya Toangoma.

Kwa sasa mwili umehifadhiwa katika Hospitali ya Vijibweni, na taarifa rasmi za mazishi zitatolewa baadaye.

17/07/2025

Anaitwa .zungu15 ni kijana toka Muheza, Tanga ni moja ya kijana mwenye kipaji kikubwa sana kwa kupangilia maneno na kuyawekea radha kwenye beat.

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Koncept TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share