Upendo Media

Upendo Media We are Christian Media House owned by The Evangelical Lutheran Church in Tanzania, Eastern Coastal Diocese (ELCT ECD).

Upendo Media is the home of Upendo TV, Upendo FM Radio and Upendo Weekly Newspaper.

27/08/2026
Kwaya Kuu ya KKKT - DMP, Mtaa wa Misugusugu, inatarajia kufanya uzinduzi wa albumu yao ya video inayoiitwa “SHANGWE – SH...
27/08/2026

Kwaya Kuu ya KKKT - DMP, Mtaa wa Misugusugu, inatarajia kufanya uzinduzi wa albumu yao ya video inayoiitwa “SHANGWE – SHANGWE”, yenye jumla ya nyimbo nane.

Uzinduzi huo utafanyika Agosti 30, 2026 pale KKKT- Mtaa wa Misugusugu, Kibaha kuanzia saa mbili na nusu asubuhi.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo ni Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Gideon Kingu, atakayeambatana na wageni na watu mashuhuri walioalikwa.

Usikose kuwa sehemu ya tukio hili kubwa la uzinduzi wa album ya video ya Kwaya Kuu Misugusugu!

Kwa mawasiliano zaidi, tafadhali piga simu kwa namba zifuatazo: 0712 215 412 – Mwinjilisti Kiongozi ; 0784 594 585 – Mwenyekiti Kwaya Kuu AU 0713 760 958 – Mwenyekiti Kamati ya Uzinduzi.

Pia usisahau ku-subscribe kwenye ukurasa wa YouTube , ili uweze kufuatilia nyimbo, video na matukio ya Kwaya Kuu Misugusugu.

Kwaya Kuu Misugusugu – SHANGWE! SHANGWE!


27/08/2026

🎤 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, akiwa bungeni leo katika maswali ya papo kwa papo kutoka kwa Wabunge.


27/08/2026

Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank PLC, Lomnyaki Saitabau, amejinasibu kiwa benki hiyo ni mfano katika kuyafikia makundi yote ya uzalishaji uchumi katika jamii.

Kuanzia mikopo ya mtu mmoja hadi vikundi, Lomnyaki amesema Maendeleo Bank ndo jibu la kuaminika.

Ameyasema hayo leo Agosti 27, 2026 akizungumza katika kipindi cha Wakeup call kinachorushwa mbashara na Upendo TV.


27/08/2026

Maendeleo Bank PLC yajayo yanafurahisha
🎤 Lomnyaki Saitabau
Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank PLC akizungumza katika kipindi cha Wakeup call kinachorushwa mbashara na Upendo TV.

27/08/2026
Saa zisizozidi 36 zimetosha kwa CCM, kumpata Deogratius Ndejembi, kuwa mrithi wa aliyekuwa Makamu wa Rais wa sita wa Jam...
26/08/2026

Saa zisizozidi 36 zimetosha kwa CCM, kumpata Deogratius Ndejembi, kuwa mrithi wa aliyekuwa Makamu wa Rais wa sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ambaye amejiuzulu nafasi hiyo.

Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, ameviambia vyombo vya habari usiku wa leo Agosti 26, 2026 kuwa kupitia Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama hicho, wamemteua Ndejembi aliyekuwa Waziri wa Nishati ambaye sasa jina lake litapelekwa Bungeni ili kuidhinishwa rasmi kabla hajaapishwa.

Pamoja na hilo, ametangaza kuwa Halmashauri Kuu ya Taifa imemfukuza rasmi uanachama, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi.

Ndejembi ni Mbunge wa CCM, akiwakilisha wananchi wa Jimbo la Chamwino, mkoani Dodoma.


Mkutano wa Nne wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, umeanza leo jijini Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine ut...
26/08/2026

Mkutano wa Nne wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, umeanza leo jijini Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine utajadili miswada mitano ya sheria ambayo imesomwa leo kwa mara ya kwanza.

Miswada hiyo ni Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Kilimo wa Mwaka 2026; Muswada wa Sheria ya kufuta Sheria ya Tasnia ya Pareto wa Mwaka 2026; Muswada wa Sheria ya Mikopo kwa Dhamana za mali zinazohamishika wa mwaka 2026; Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali za mwaka 2026 na Muswada wa Sheria za Marekebisho ya Sheria mbalimbali Na. 2 wa mwaka 2026.

Taarifa ya Bunge, imesema leo kuwa mkutano huo wa bunge utamalizika Septemba 4, mwaka huu ambapo jumla ya maswali ya kawaida 140 yataulizwa na Wabunge na kujibiwa na Serikali.



Address

P. O BOX 13603
Dar Es Salaam
12115

Opening Hours

Monday 08:00 - 20:00
Tuesday 08:00 - 20:00
Wednesday 08:00 - 20:00
Thursday 08:00 - 20:00
Friday 08:00 - 20:00
Saturday 08:00 - 20:00
Sunday 12:00 - 20:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Upendo Media posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share