
18/09/2025
Filamu “Evil Unbound” kuhusu Kitengo cha 731, ilizinduliwa kwa mara ya kwanza duniani jana (Jumatano) mjini Harbin, eneo ambalo hapo zamani lilikuwa makao ya kikosi hicho cha kibiolojia cha Kijapani, ikibainisha ukatili uliofanywa na wanajeshi wa uvamizi wa Japani nchini China wakati wa Vita Kuu vya Pili vya Dunia.
Filamu hiyo inaeleza kisa cha Wang Yongzhang, mfanyabiashara wa eneo hilo, na wengine waliokuwa wafungwa katika “gereza maalum” la Kitengo 731, waliodanganywa kwa ahadi za uongo za kupewa uhuru iwapo wangekubali kushiriki katika kile kilichodaiwa kuwa ukaguzi wa afya na utafiti wa kuzuia magonjwa, lakini hatimaye wakawa wahanga wa majaribio ya kikatili ya kitabibu, ikiwemo majaribio ya kuathiriwa na baridi kali na kufanyiwa upasuaji wakiwa hai.