
13/10/2025
Baada ya kipigo cha 4-1 dhidi ya Al Hilal ya Sudan, klabu ya Simba SC imeachwa na maswali mengi
kuhusu uimara wake kuelekea msimu huu mpya wa mashindano ya kimataifa. Licha ya mchezo huo kuwa wa kirafiki, udhaifu wa safu ya ulinzi na mawasiliano hafifu
ulijitokeza wazi, jambo linalompa Kocha Pira Pantev kazi kubwa kurekebisha timu kabla ya mechi za ushindani.
Wachambuzi wamesema Simba inapaswa kuchukulia kipigo
hiki k**a funzo muhimu, si pigo la kukata tamaa, huku
ikisisitizvwa umuhimu wa kurejesha maelewano na nidhamu ya kiuchezaji. Kwa upande wa Al Hilal, ushindi huu
umeonyesha ubora wao kimkakati na maandalizi madhubuti kuelekea mashindano ya Afrika. Simba sasa inapaswa kujipanga upya, kuimarisha mawasiliano
na nidhamu ya kiuchezaji, ili kurejea katika ubora unaotarajiwa na mashabiki wake.
Kwa taarifa za kimichezo na makala maalumu Follow Instagram Link https://www.instagram.com/dofusports?
Follow Facebook Link https://www.facebook.com/Dofusports
Follow Tiktok Link https://www.tiktok.com/?