18/09/2025
Klabu ya Soka ya Benfica imetangaza kumuajiri mwalimu wa mpira Jose Mourinho (62) raia wa Ureno , Kuwa kocha mkuu wa Kikosi hicho kwa mkataba wa Miaka 2 utakaomweka klabuni hapo mpaka mwaka 2027 , Akichukua mikoba ya Bruno Lage aliyetupiwa virago kutokana na mwenendo mbovu wa timu hiyo.
Meneja huyo ambaye amewahi kuvinoa vilabu vya Fenerbahce , Chelsea , Real Madrid , Manchester United , FC Porto , Tottenham na AS Roma , Anarejea kwa mara nyingine tena klabuni hapo , Mahali alipoanzia safari yake ya ukocha mwaka 2000.
José Mourinho:🇵🇹🎙"Katika klabu zote nilizowahi kutumikia k**a kocha , Hakuna timu iliyonipa msukumo k**a Benfica."
🌍🌎🌏 🌍🌎🌏