11/01/2026
Jeshi la Iran limesema litalinda miundombinu na mali ya umma, likiwataka Wairani kuzuia njama za adui huku mamlaka zikikandamiza maandamano.
Taarifa ya jeshi la Iran imetolewa baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutoa onyo jipya kwa viongozi wa Iran siku ya Ijumaa, na baada ya Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio kutangaza kwamba "Marekani inawaunga mkono watu jasiri wa Iran."
Machafuko yameendelea usiku kucha huku vyombo vya habari vya serikali vikisema kuwa jengo la manispaa lilichomwa moto mjini Karaj, magharibi mwa Tehran, na kuwalaumu "wachochezi kwa ghasia".
Televisheni ya taifa imerusha picha za mazishi ya wanachama wa vikosi vya usalama ambao ilisema waliuawa wakati wa maandamano katika miji ya Shiraz, Qom na Hamedan.
Mhariri |