04/08/2025
๐จ BREAKING NEWS
Yanga SC ๐น๐ฟ wamefikia makubaliano ya kumuuza mshambuliaji wao chipukizi Clement Mzize ๐น๐ฟ kwa klabu ya Al-Sadd SC ๐ถ๐ฆ kwa ada ya usajili ya USD 900,000 (zaidi ya TSh 2.3 bilioni)! ๐ฐ๐ก๐ข
Hata hivyo, dili hilo bado halijakamilika rasmi kutokana na tofauti ya makubaliano ya maslahi binafsi ya mchezaji na klabu mpya.
๐ Hali ilivyo kwa sasa:
Yanga SC wameridhia dili na tayari wamefungua mlango wa kumruhusu Mzize kwenda Qatar.
Wakala wa Mzize anataka mshahara wa USD 50,000 kwa mwezi kutoka kwa Al-Sadd.
Al-Sadd SC wapo tayari kutoa USD 30,000 kwa mwezi, kiwango ambacho bado hakijakubalika na upande wa mchezaji.
Hii inaashiria kuwa licha ya klabu kuridhiana, hatua ya mwisho ya kukamilisha uhamisho huu iko mikononi mwa mchezaji na wakala wake kuhusu makubaliano ya mshahara.
๐ Mzize amekuwa kwenye kiwango bora akiwa na Yanga SC, na hili linaweza kuwa dili kubwa zaidi kwa mchezaji chipukizi wa Tanzania katika historia ya karibuni.
Cc