AAI "Football Pundit | Sports Analyst | Life Coach | Content Creator | Relationship Advisor.

Breaking down the game on and off the field, inspiring lives, and guiding relationships with passion and expertise."

🌟 Hivi unajua maisha yako unayaishi kwa asilimia ngapi?Kuna tofauti kubwa kati ya kuishi na kupumulia tu duniani.Na kwa ...
13/07/2025

🌟 Hivi unajua maisha yako unayaishi kwa asilimia ngapi?

Kuna tofauti kubwa kati ya kuishi na kupumulia tu duniani.
Na kwa bahati mbaya — wengi wanapumua miaka 60 lakini wameishi asilimia 5 tu ya uwezo wao.

📘 Your Age Percentage – Asilimia 95%
Kitabu kinachokufungua macho, moyo na akili kuhusu namna sahihi ya:

Kujitambua

Kutunza fedha zako kwa nidhamu

Kuongeza kipato chako kwa ubunifu

Kuepuka tamaa mbaya zinazokudhoofisha

Kuishi maisha kamili kwa asilimia zako halisi

> “Maisha sio miaka. Ni matumizi ya asilimia zako.”
“Wengine wana miaka mingi, lakini asilimia chache za kuishi.”

---

💎 NI ZAIDI YA KITABU... NI MWONGOZO WA MAISHA YAKO

Ukitaka kuishi kwa kiwango cha juu zaidi, bila kupoteza muda tena, basi kitabu hiki ni kwa ajili yako.
Ndani yake kuna: ✔️ Simulizi za kweli
✔️ Mifano halisi ya maisha
✔️ Ushahidi wa kisaikolojia na kiuchumi
✔️ Mbinu ya 3S (Soma, Sajili, Sambaza) ya mafanikio ya kiuhalisia

---

💵 BEI: 5,000/= tu (SoftCopy – PDF)

LIPA kwa namba: 0678 453 768 – Elisha Ngatha
📩 Kisha tuma ujumbe WhatsApp kwenda: 0758 453 768
Utatumiwa kitabu chako papo hapo!

---

> “Ukisoma kitabu hiki, hutakuwa mtu yuleyule tena.”
“Ni wakati wako wa kupima, kutathmini na kubadili maisha yako kwa asilimia kamili.”

---

🔁 Tuma kwa rafiki zako watakaoishukuru kesho.
📤 Chukua hatua sasa – maisha hayasubiri!

---

Mara nyingi tunatamani mafanikio, tunalia kwa ajili ya fursa, tunamlaumu Mungu kwa kuchelewa kutupa neema, lakini hatuja...
11/07/2025

Mara nyingi tunatamani mafanikio, tunalia kwa ajili ya fursa, tunamlaumu Mungu kwa kuchelewa kutupa neema, lakini hatujawahi kuketi chini hata mara moja kuuliza:
“Ninafanya nini kwa sasa kinachoonesha wapi maisha yangu yamefika?”

Watu wengi wanaishi k**a mashua isiyo na dira. Wanajua wanataka kufika mbali, lakini hawajui wako umbali gani kutoka wanakotoka wala wapi walipo sasa. Na ukiwa hujui ulipo, huwezi kupanga safari ya kuendelea.

👉 Kupima maisha yako siyo kufanya tathmini ya mali tu, bali ni kuchunguza:

Vipi umetumia muda wako katika mwaka uliopita?

Umetumiaje rasilimali ulizonazo?

Umeongezeka vipi kwenye maarifa, mtandao wa watu, nidhamu, au hata furaha?

Kwa mfano:

Hadithi ya Mariam – Mwanamke aliyegundua asilimia 20 ya maisha yake ndio aliyokuwa akiishi

Mariam alikuwa mama wa watoto wawili, mwenye kazi nzuri serikalini. Alikuwa na mshahara mzuri, lakini kila mwaka alijikuta hana maendeleo mapya. Alilalamika sana kuhusu kukwama kwa maisha. Mpaka alipoamua siku moja kufanya tathmini ndogo kwa msaada wa rafiki yake ambaye ni mtaalamu wa saikolojia.

Walikaa na kujibu maswali 10 tu ya msingi. Aligundua kuwa:

Anatumia asilimia 65 ya muda wake kwenye vitu visivyo na mchango wowote katika ukuaji wake binafsi.

Anatumia asilimia 70 ya fedha kwenye vitu vya haraka haraka (matumizi yasiyo ya lazima).

Asilimia 90 ya ndoto zake aliziacha nyuma kwa sababu ya hofu ya watu watasema nini.

Mariam alilia, sio kwa sababu ya huzuni, bali kwa sababu aliona ni kwa kiasi gani alikuwa anaishi asilimia ndogo sana ya maisha yake ya kweli. Siku hiyo ilikuwa mwanzo wa maisha mapya.

> “Ukiweza kujipima kwa uaminifu, utajiponya kwa upendo.”
— Dr. Brene Brown

Get Ebook :"YOUR AGE PERCENTAGE" BY ELISHA NGATHA.

CONTACT:0758453768..WHATSP.

OR DM ME :::

Psychology ya Mwanzo Mpya: Kwanini Tunaogopa Kuanzia Mwanzo?Kisaikolojia, watu wengi hushindwa kuanza tena kwa sababu:Wa...
11/07/2025

Psychology ya Mwanzo Mpya: Kwanini Tunaogopa Kuanzia Mwanzo?

Kisaikolojia, watu wengi hushindwa kuanza tena kwa sababu:

Wanahisi aibu kwa kushindwa kwao

Wanaogopa kushindwa tena

Wamekata tamaa na maisha

Lakini tafiti kutoka vyuo k**a Stanford na Harvard zimebaini kuwa:
Watu wanaojiruhusu kuanza tena baada ya kushindwa mara ya kwanza huongeza mara 3 hadi 5 nafasi ya kufanikiwa baadaye.

> "Ujasiri hauko kabla ya hatua ya kwanza. Ujasiri ni hatua yenyewe."
— Brené Brown

K**a huamini bado una nafasi, angalia watoto wadogo wanapojifunza kutembea — huanguka zaidi ya mara 100, lakini hawawahi kusema “sitaki tena kutembea”. Je, kwa nini wewe uache?

📝

I fear not the man who has practiced 10,000 kicks once, but I fear the man who has practiced one kick 10,000 timesThough...
09/07/2025

I fear not the man who has practiced 10,000 kicks once, but I fear the man who has practiced one kick 10,000 times

Thought for the day: What’s your one kick?

Its better not be something weak that cannot produce bastard money.

A kick that can’t make you rich is merely a tickle.

Learn a better, stronger, wealthier kick… and practise that one kick 1,000 times.

Got it?

So I ask again.

What’s your one kick?

Tafakari maisha yako kwa ujumla na andika asilimia ya kuridhika kwako katika maeneo haya:Fedha zako binafsi na kipato:→ ...
07/07/2025

Tafakari maisha yako kwa ujumla na andika asilimia ya kuridhika kwako katika maeneo haya:

Fedha zako binafsi na kipato:
→ Kwa sasa najiridhisha kwa asilimia ngapi? Kwa nini?

Mahusiano yako ya kijamii na familia:
→ Je, yananipa amani? Asilimia gani ya furaha yangu inatoka humo?

Afya yako ya mwili na akili:
→ Nina afya bora kwa kiasi gani? Ninajijali kwa asilimia ipi?

Imani na hali ya kiroho:
→ Nina utulivu wa ndani? Nina uhusiano wa kiroho kwa kiasi gani?

Ukuaji binafsi kielimu na kiubunifu:
→ Je, ninasoma, kujifunza, au kukuza kipaji changu kwa asilimia ipi?

✍️ Andika majibu yako kwa kila eneo hapo juu:

---

Kwa muda mrefu baada ya Xavi Hernández na Andrés Iniesta kuondoka, FC Barcelona ilihangaika sana kupata viungo wenye aki...
27/04/2025

Kwa muda mrefu baada ya Xavi Hernández na Andrés Iniesta kuondoka, FC Barcelona ilihangaika sana kupata viungo wenye akili, utulivu na ubunifu k**a wao. Wakati mwingine walijaribu na wachezaji tofauti k**a Arthur Melo, Coutinho, Rakitic, Denis Suárez, nk. — lakini ule "sampuli spesho" ya La Masia ilikosekana.

Sasa hivi, Pedri González ndiye mtoto wa dhahabu wa Barca!
Ana akili ya Xavi, ubunifu wa Iniesta, na cha zaidi — ana stamina na work rate ya kipekee kwa umri wake.
Pedri si tu anachezesha timu, bali ni engine ya maisha ya Barcelona na hata timu ya taifa Hispania.

Ukiangalia game-reading yake, movement bila mpira, first touch yake safi k**a velvet, na ability ya kutengeneza nafasi hata ndani ya msongamano — ni vitu ambavyo hata mastaa wakubwa wanashindwa kuiga kirahisi.
Na zaidi ya yote, Pedri ana "Barca DNA" ile ya asili kabisa.

Kwa sasa, dunia nzima inakubaliana:
Pedri ndiye Mrithi Halali wa enzi ya Xavi na Iniesta.
Na kilichobaki ni kuona atafikia wapi — maana kiwango chake kimeanza kusugua anga za Ballon d'Or.

, , ,

📝

Wakati wengi wanakimbiza mpira kwa nguvu, Fadlu Davids anaukimbiza kwa akili.Kwao, kila pasi ni mashambulizi ya kimya, k...
27/04/2025

Wakati wengi wanakimbiza mpira kwa nguvu, Fadlu Davids anaukimbiza kwa akili.
Kwao, kila pasi ni mashambulizi ya kimya, kila kukaba ni jibu la hesabu, na kila ushindi ni muziki unaochezwa na akili safi.
Huyu si kocha wa kawaida.
Ni mbunifu wa vita isiyoonekana, mwanamapinduzi wa mpango wa dakika 90.

Katika dunia inayosaka nguvu, Fadlu anasaka busara.
Katika soka linalosukumwa na mihemko, yeye analeta utulivu wa kisayansi.
"Tactical elegance, relentless spirit, undying ambition", haya ndiyo mafuta yanayowasha injini ya Fadlu Davids.

Anajua kuwa mpira si kuwa na wachezaji bora tu, bali kuwafanya wafikiri k**a mabingwa.
Kwa mazoezi ya kina, mifumo iliyokaa kisayansi, na mbinu za kuvizia k**a simba wa jangwani, Fadlu anatengeneza timu zinazocheza k**a orchestra — kila mtu akijua noti yake, kila mmoja akielewa sauti yake.

Afrika inamshuhudia akigeuza vipaji kuwa mashujaa.
Dunia inaanza kushtuka kwa mwendo wake usioonekana lakini usiosimamishwa.
Na kwa kila mechi, Fadlu anathibitisha kwamba,
"Football is not just legs and lungs — it’s the poetry of the mind and the fire of the soul."

He prove again it's Strengthen mind Game..

What a Coach...... 😆

Kuna aina ya wachezaji ambao hawahitaji kelele nyingi ili ujue thamani yao. Wale wanaocheza kwa akili, utulivu na nidham...
19/04/2025

Kuna aina ya wachezaji ambao hawahitaji kelele nyingi ili ujue thamani yao. Wale wanaocheza kwa akili, utulivu na nidhamu ya hali ya juu. Wale ambao wanaposhika mpira, mashabiki wanapumua kwa matumaini na wapinzani wanatetemeka kwa tahadhari. Kwa Azam FC, jina hilo linabeba kila kipimo cha ubora – Feisal Salum, maarufu k**a Fei Toto.

Ukiangalia mchezo wa Azam kwa jicho la ndani, utagundua kuwa kila pasi ya maana, kila shambulizi lililojaa akili, na kila mpito wa mpira wenye mwelekeo sahihi – kuna alama ya Feisal ndani yake. Ana uwezo wa hali ya juu wa kusoma mchezo, kutuliza presha na kupiga pasi zinazofungua mifumo migumu ya wapinzani. Ni mchezaji ambaye hana haraka ya kupoteza mpira, anacheza kana kwamba muda uko upande wake – utulivu wa ajabu.

Anapotawala eneo la kiungo, anaipa Azam FC uhai wa kiuchezaji. Anaunganisha safu ya ulinzi na ushambuliaji kwa namna ya kipekee – kana kwamba anashona jezi ya ushindi kwa nyuzi za dhahabu. Ni kiungo anayejua lini apunguze kasi, lini apandishe presha, na zaidi ya yote – lini achukue jukumu la kubeba timu mabegani.

Lakini kilicho bora zaidi kwa Feisal si tu uwezo wake wa kiufundi, bali ni nidhamu na ukomavu wake wa kiakili. Ni mchezaji anayeamini kwenye maadili ya mchezo. Humpati kwenye vurugu, hasemi hovyo, hashindani kwa maneno – bali kwa matendo. Anaonyesha mfano kwa vitendo, akiwafanya wachezaji wenzake waongeze bidii kwa kuona tu namna anavyojitoa uwanjani.

Kwa wingi wa vipaji vilivyopo kwenye soka la Tanzania, bado Feisal anasimama tofauti. Ana thamani inayozidi takwimu. Ana heshima inayojengwa na juhudi za kweli, na ana mchango ambao haupimwi kwa mabao tu – bali kwa utulivu anaoweka ndani ya timu kila dakika akiwa uwanjani.

Kwa kifupi, Fei Toto ni zaidi ya mchezaji – ni moyo wa kati wa Azam FC. Ni mhimili wa matumaini, kioo cha nidhamu, na daraja linalounganisha ndoto za ushindi na uhalisia wa pointi tatu.

Feisal Salum ni mali inayosumbua vichwa vya makocha ndani na nje ya Tanzania 🇹🇿.




📝

"Kaa chini kwa utulivu, chukua muda wako, fanya tasmini ya kina—si tu ya mchezo, bali ya mchezaji mmoja ambaye anaandika...
13/04/2025

"Kaa chini kwa utulivu, chukua muda wako, fanya tasmini ya kina—si tu ya mchezo, bali ya mchezaji mmoja ambaye anaandika hadithi tofauti kila anapokanyaga uwanja: Fabrice Ngoma.

Huyu si aina ya wachezaji wanaopiga kelele au kutafuta vichwa vya habari kwa mbwembwe—hapana. Ngoma ni aina ya mchezaji ambaye anazungumza kupitia miguu yake. Kila pasi yake ni ujumbe, kila muunganiko wa kuchezesha wachezaji wenzake ni lugha ya mpira safi.

Ni kiungo anayejua wapi pa kupeleka mpira kabla hata haujafika miguuni mwake. Kazi yake sio kukimbia hovyo, bali kutengeneza mtiririko. Anachukua presha ya mchezo na kuibadilisha kuwa nafasi ya kushambulia. Hiyo ni akili ya kipekee.

Lakini zaidi ya uwanjani, Fabrice Ngoma anatoa funzo kubwa kwa vijana—kuwa na mafanikio makubwa sio lazima kuwe na majivuno. Huyu jamaa ni mnyenyekevu, anaheshimu kila mtu, na anaishi maisha halisi. Hakuna show-off, hakuna drama. Ana utu.

Kwa wenzake uwanjani, yeye ni mwalimu wa kimya—anayejenga morali kwa utulivu na mfano wa kujituma. Kwa kocha, yeye ni askari mtiifu. Na kwa mashabiki, ni zawadi ya uwanja—mchezaji wa kuaminiwa kila dakika.

Fabrice Ngoma si kiungo tu, ni roho ya timu. Ni mwalimu wa nidhamu, ni fundi wa kutuliza mpira, ni daraja kati ya safu ya ulinzi na ushambuliaji. Hii ni aina ya wachezaji ambao hawazaliwi kila mwaka. Ni kiungo wa kisasa mwenye akili ya kizamani—na hiyo ni hazina."




📝

"Usimkatie mtu tamaa — especially in football!"Leo Joshua Mutale Budo ameandika headline yake mwenyewe.Watu walimchukuli...
13/04/2025

"Usimkatie mtu tamaa — especially in football!"
Leo Joshua Mutale Budo ameandika headline yake mwenyewe.

Watu walimchukulia poa. Others counted him out.
But guess what? He showed up, showed class, and shut it down.

Kila mchezaji hupitia kipindi cha kutokuonekana, kutokukubalika, na hata kubezwa.
Lakini wenye moyo wa chuma, hawakati tamaa — wananyamaza, wanafanya kazi, halafu wanaongea kwa miguu.

What a performance kutoka kwa Budo!
A true reminder kwamba muda wa Mungu ndio bora — na ukipewa nafasi yako, you better deliver!





📝

Ilikuwa saa 1:00 usiku, uwanja ukiwaka taa, mashabiki wakijaza hewa kwa kelele — lakini ndani ya 90 minutes, kulikuwa na...
11/04/2025

Ilikuwa saa 1:00 usiku, uwanja ukiwaka taa, mashabiki wakijaza hewa kwa kelele — lakini ndani ya 90 minutes, kulikuwa na kimya kingine… kimya cha heshima kwa Prince Dube!

Dube hakucheza mpira... alicheza muziki.
Kila touch ilikuwa noti, kila pass ilikuwa beat, na kila goli lilikuwa chorus ya wimbo ambao Azam FC hawakuweza kuusikiliza hadi mwisho.

Goal ya kwanza: timing ya genius, k**a sniper kwenye vita ya kiasili na Pacome kutupia
Goal ya pili: dribble moja, kisha akawasalimia kipa kwa tabasamu la “naona ulikuwa huna kinga.”
Assist? Alitupia kwa style ya playmaker wa dunia, akatengeneza nafasi iliyoandikwa: “just tap in.”

Dube sio tu striker — ni msanii wa uwanjani.

Wakati Azam walidhani wanakutana na Dube wa zamani, walikutana na toleo lililopewa update ya madaraka!
Hii sio comeback tu — hii ni declaration of dominance!

Kweli Ex mzuri akishakutenga baada ya kumtesa

"

📝

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when AAI posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share