Rick Media

Rick Media We cover All Sports News across the World
Under

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Februari 27,2026 ameandaa Iftar maalum kwa wakazi wa Mkoa huo h...
27/02/2026

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Februari 27,2026 ameandaa Iftar maalum kwa wakazi wa Mkoa huo hafla ambayo imefanyika katika ukimbi wa Diamond Jubilee.

Katika hafla hiyo viongozi mbalimbali wa Dini na Serikali pamoja na wananchi kutoka maeneo tofauti ya Jiji la Dar es Salaam wamehudhuria.

Mgeni rasmi katika tukio hilo alikuwa M***i Mkuu wa Tanzania Dkt Abubakar Zubeir bin Ally ambaye aliwaongoza waumini katika dua ya kuiombea nchi amani, mshik**ano na maendeleo endelevu.

Akizungumza katika hafla hiyo RC Chalamila aliwataka wakazi wa Dar es Salaam kuendeleza umoja na upendo miongoni mwao, akisistiza kuwa mwezi mtukufu wa Ramadhani ni fursa ya kuimarisha mshik**ano wa kijamii na kusaidiana. Alieleza Serikali ya Mkoa itaendelea kushirikiana na Viongozi wa Dini katika kudumisha amani na utulivu.

Kwa upande wa M***i Mkuu aliishukuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kuandaa Iftar hiyo, akieleza kuwa matukio ya aina hiyo huimarisha uhusiano kati ya Serikali na Jamii ambapo ametoa wito kwa watanzania kuendelea kuiombea nchi na kuzingatia maadili katika kipindi hiki cha Ramadhani.

Hafla hiyo ilihitimishwa kwa futari ya pamoja iliyoambatana na mawaidha mafupi ya kidini huku washiriki wakionyesha furaha na mshik**ano mkubwa.

  Umeshamtambua Huyu ni Staa Gani?
27/02/2026

Umeshamtambua Huyu ni Staa Gani?

  Mahak**a ya Kaunti ya Bomet County imemhukumu Bernard Miyeiende Kerongo kifungo cha miaka 50 jela na faini ya KSh50 mi...
27/02/2026

Mahak**a ya Kaunti ya Bomet County imemhukumu Bernard Miyeiende Kerongo kifungo cha miaka 50 jela na faini ya KSh50 milioni kwa kosa la kupatikana na kusafirisha bangi.
Kwa mujibu wa Office of the Director of Public Prosecutions (DPP), Kerongo alik**atwa Machi 22, 2024 katika mji wa Mulot kando ya barabara ya Bomet–Narok akiwa na magunia kumi ya bangi yenye uzito wa kilo 278, yenye thamani ya KSh8,340,000.
Aidha, ameagizwa kulipa faini ya KSh50 milioni au atumikie kifungo cha ziada cha miaka mitano iwapo atashindwa kulipa.

  Rapa Wiz Khalifa ameshindwa katika rufaa yake nchini Romania baada ya Constanța Court of Appeal kuthibitisha hukumu ya...
27/02/2026

Rapa Wiz Khalifa ameshindwa katika rufaa yake nchini Romania baada ya Constanța Court of Appeal kuthibitisha hukumu ya kifungo cha miezi tisa jela kwa kosa la kupatikana na bangi mwaka 2024.
Mahak**a ilitupilia mbali ombi lake la kufuta hukumu na pia kukataa kusimamisha adhabu hiyo. Awali alikuwa amepigwa faini ya lei 3,600, lakini waendesha mashtaka walifanikiwa kuomba adhabu kali zaidi.
Bado haijulikani k**a Romania itaanzisha mchakato wa kumrudisha nchini humo, kwani ni raia wa Marekani na haishi Romania.

  wakili mwingine wa Rapa Nicki Minaj amejiondoa katika kesi inayomkabili Rapa huyo ya dola milioni 10. Wakili huyo, Mat...
27/02/2026

wakili mwingine wa Rapa Nicki Minaj amejiondoa katika kesi inayomkabili Rapa huyo ya dola milioni 10.
Wakili huyo, Matthew Abbott, ameomba kujitoa kwenye kesi akidai kumekuwa na tatizo la mawasiliano kwa sababu hajafanikiwa kuwasiliana na Nicki kwa miezi kadhaa licha ya kutuma ujumbe na barua pepe mara nyingi.
Kesi hiyo ilifunguliwa na shabiki aitwaye Tameer Peak. Inaripotiwa pia kwamba wakili wake wa awali, Judd Burstein, naye alijiondoa mwaka jana.
Jaji bado hajatoa uamuzi kuhusu ombi la Abbott, lakini Nicki amepewa muda wa kujibu.

  Hatimaye Basketball Africa League (BAL) imetangaza rasmi makundi mawili yatakayounda hatua ya awali ya msimu wa mwaka ...
26/02/2026

Hatimaye Basketball Africa League (BAL) imetangaza rasmi makundi mawili yatakayounda hatua ya awali ya msimu wa mwaka 2026, pamoja na ratiba ya michezo itakayofanyika katika nchi mbalimbali barani Afrika ambapo timu ya mpira wa kikapu kutokea Tanzania ikiwa ni miongoni mwao.
Msimu wa 2026 utaanza rasmi kwa Kalahari Conference itakayochezwa mjini Pretoria, South Africa kuanzia Machi 27 hadi Aprili 5, 2026. kutoka Tanzania ipo katika kundi la Timu za Afrika Kusini ambalo Michezo itafanyika Pretoria lakini pia ndio timu pekee inayoiwakilisha Tanzania michuano ya Kimataifa.

KALAHARI CONFERENCE - Pretoria (27 Machi — 5Aprili)
Timu zitakazoshiriki ni:

* Al Ahly Benghazi - Libya
* APR BBC - Rwanda
* Dar City - Tanzania
* Nairobi City Thunder - Kenya
* ⁠petro de luanda
* ⁠johnesubarg giants

Baada ya hapo, mashindano yatahamia Afrika Kaskazini kwa Sahara Conference itakayofanyika mjini Rabat, Morocco kuanzia Aprili 24 hadi Mei 3, 2026.

SAHARA CONFERENCE - Rabat (24 Aprili - 3 Mei)
Timu zitakazoshiriki ni:

Al Ahly - Misri
Ville de Dakar - Senegal
• SKA Kings - Côte d’lvoire Petro de Luanda - Angola
Kila kundi litatoa timu nne bora kati ya sita kuelekea kwenye playoffs zitakazopigwa Mwezi May katika mji wa kigali Rwanda.

  Waziri Mkuu wa India Toka 2014, Narendra Modi Amekuwa Mwanasiasa wa Kwanza Duniani Kufikisha Wafuasi Milioni 100 katik...
26/02/2026

Waziri Mkuu wa India Toka 2014, Narendra Modi Amekuwa Mwanasiasa wa Kwanza Duniani Kufikisha Wafuasi Milioni 100 katika Mtandao wa Instagram.
Kwa upande wa Rais wa Marekani Donald Trump Ana Wafuasi takriban milioni 43.

  Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV, anatarajiwa kufanya ziara ya siku 10 barani Afrika kuanzia Aprili 1...
26/02/2026

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV, anatarajiwa kufanya ziara ya siku 10 barani Afrika kuanzia Aprili 13 hadi 23, 2026, kwa Mujibu wa taarifa ya Vatican.
Ziara hiyo itaanza nchini Algeria Hii itakuwa ziara ya kwanza ya Papa nchini humo, ambako Uislamu ni dini ya serikali. Papa Leo anatarajiwa pia kuzuru maeneo aliyohusishwa nayo Mtakatifu Augustine pamoja na kuendeleza mazungumzo kati ya Wakristo na Waislamu.
Pia ataelekea Cameroon na Angola, na kuhitimishwa Equatorial Guinea. Lengo ni kuimarisha mazungumzo ya kidini na kuhimiza amani katika ukanda huo.

  Mwanamitindo Rahman Jago Amesema kupitia X kuwa msanii wa Afrobeat wa Nigeria, Burna Boy, amebadilisha Dini na kuingia...
26/02/2026

Mwanamitindo Rahman Jago Amesema kupitia X kuwa msanii wa Afrobeat wa Nigeria, Burna Boy, amebadilisha Dini na kuingia kwenye Uislamu.
Burna Boy Kupitia livestream ya Novemba 2025 alisema kuwa alikulia katika Ukristo lakini baadaye alichunguza na kuukumbatia Uislamu kupitia maombi na utafiti binafsi.
Swipe left…

  Trump amkalia kooni Maduro. Hata apate ufadhili aina yoyote kwenye kesi yake.Tembelea website yetu rickmedia.co.tz (Li...
26/02/2026

Trump amkalia kooni Maduro. Hata apate ufadhili aina yoyote kwenye kesi yake.

Tembelea website yetu rickmedia.co.tz (Link kwenye Bio) kusoma habari hii kwa urefu zaidi.

  wa jana kampuni ya SAMSUNG imezindua simu zake mpya za SamSung S26 zenye matoleo tofauti tofauti. Tembelea website ya ...
26/02/2026

wa jana kampuni ya SAMSUNG imezindua simu zake mpya za SamSung S26 zenye matoleo tofauti tofauti.

Tembelea website ya rickmedia.co.tz (Link kwenye Bio) kusoma habari hii kwa urefu zaidi.

Address

Dar Es Salaam
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Rick Media posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share