02/01/2026
Je Wajua?
Muonekano halisi wa VVU?
Kumekuwepo kusambaa kwa taarifa na picha za upotoshaji inayosemekana ni muonekano wa kirusi cha UKIMWI (VVU) aliyevutwa kwa hadubini ya umeme (electronic microscope), jambo ambalo si kweli.
Picha hiyo inayosambaa k**a ionekanavyo kwenye picha sio VVU bali ni kiumbe mkubwa ambaye anaonekana kwa macho ya kawaida bila ya kutumia hadubini, kiumbe huyo ni kiwavi(lavar) mwenye miba anaitwa SPIKY CATERPILLAR, ni kiluwiluwi k**a wengine ambao ni miongoni mwa hatua za ukuaji wanazopitia wadudu(insects) mbalimbali k**a vile vipepeo, nondo n.k.
Viwavi hawa huwa na mwili uliozungukwa na miba, nywele ngumu au vinyweleo vyenye ncha kali zenye sumu katika sehemu mbalimbali ambavyo huwasaidia kujilinda na maadui mbalimbali na sumu hiyo huweza kusababisha muwasho, maumivu, uvimbe, vipele au mzio(allergy) kwa atakaegusa au kuchomwa na miba hizo.
Na picha ya pili unayoiona ndiyo picha iliyothibitishwa na wataalam husika kuwa inafanana zaidi na VVU.