09/06/2026
Kijana mdogo mwenye maono makubwa. 🎶
Wakati wengine wanasubiri fursa, Godlove Williams ameamua kuzitengeneza. Kupitia Youth Music Academy, anaendelea kufungua milango kwa vijana wenye ndoto za muziki kwa kuwapa mafunzo, mentorship na jukwaa la kuonyesha vipaji vyao.
Kwa Godlove, muziki si kipaji pekee bali ni taaluma inayohitaji kujifunza, kujituma na kuwekeza kwenye maarifa. Ndiyo maana anaamini kuwa kila kijana mwenye ndoto ana nafasi ya kufanikiwa ikiwa atapata mwongozo sahihi.
YoungVisionary BoreshaRadio