21/11/2025
โซMkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe Shaibu Ndemanga ametembelea Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo kwa lengo la kuwajulia Hali Wanafunzi wa Shule ya Msingi Jitegemee na Majengo waliopata Changamoto ya ajali ya kuanguka kwa Mti katika Shule hiyo.
Mhe Ndemanga alipata nafasi ya Kutoa pole kwa Wazazi wa Wanafunzi hao ambao walipata changamoto hiyo Leo Novemba 20,2025 wakati wakiwa shuleni muda wa Mapumziko na kudondoka kwa Mti huo wa Muembe huku watoto hao wakiwa pembezoni mwa Mti huo.
Kwa Mujibu wa Taarifa ya Daktari wa Hospitali hiyo ya Wilaya wanafunzi hao walifikishwa Hospitalini hapo wakiwa 6 wanafunzi watano wa shule ya Msingi Jitegemee na Mmoja wa Shule ya Msingi Majengo huku akibainisha hali zao za kiafya zipo vizuri hakuna aliepata majeraha makubwa na taratibu za Kuwapatia huduma Zinaendelea.
Aidha Mhe Mkuu Wilaya ametoa maelekezo kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kuhakikisha Wanashirikiana na Uongozi wa Shule pamoja na Afisa Elimu Awali na Msingi wanatoa miti yote ambayo inaweza kuleta athari shuleni hapo na kukatwa kwa mti ambao umedondoka.
Pia Mhe Mkuu wa Wilaya ametoa rai kwa Wananchi wote kuacha kutoa taarifa ambazo zinazua taharuki kwa Jamii na badala yake kusubiri taarifa kutoka kwa Wahusika kuhusu mambo yote yanaendelea na kutokea katika Wilaya kw ujumla..
repost from