Taifa Digital Forum

Taifa Digital Forum Tunahusika na Uzalishaji wa Habari na Makala zinazohusu mstakabali wa Serikali ya Tanzania na Wananchi wake | Kufanya Mahojiano na watu mashuhuri.

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameitaka Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Mambo ya Ndani na Vyombo vya Ulinzi...
19/05/2025

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameitaka Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Mambo ya Ndani na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuchukua hatua za haraka kwa wanaotumia mitandao na teknolojia vibaya, akikemea pia wingi wa Wanaharakati kutoka nje ya nchi wanaojaribu kuingilia mambo ya ndani ya Tanzania na kutaka kuivuruga amani.

Rais Samia amesema hayo Jijini Dar es salam leo May 19, 2025 wakati akizindua Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 (Toleo la 2024), ambapo amesema hatotoa nafasi kwa watovu wa adabu kutoka nje ya nchi kuja kujaribu kuvuruga amani, utulivu na usalama uliopo nchini Tanzania.

“Tusiwe shamba la Bibi kwamba Mtu anaweza kuja Tanzania akasema analolitaka, lipo Tanzania halipo, Watu wakajisemea tu, tumeanza kuona mwenendo wa Wanaharakati ndani ya Ukanda huu kuanza kuvamia na kuingilia mambo yetu huku, sasa k**a kwao wameshadhibitiwa wasije kutuharibia, tusitoe nafasi walishavuruga kwao, nchi iliyobaki haijaharibika ni hapa kwetu, niwaombe Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutotoa nafasi kwa Watovu wa adabu wa nchi nyingine kuja kutovuka hapa kwetu, hapana”

“Nimeona clip kadhaa za kunisema, nipo bias na nini, ninalofanya ni kulinda nchi yangu na ndiyo wajibu wangu niliopewa, kwahiyo hatutotoa nafasi kwa kiumbe yeyote kuja kutuvurugia hapa awe yupo ndani ama anayetoka nje”

Katika maelezo yake, Rais Samia ameitaka Wizara na Maafisa wanaohusika kutoa ufafanuzi kuhusu yale yanayosemwa na Wanaharakati na Watu mbalimbali, kukanusha ama kuchukua hatua za haraka ikiwa yanayosemwa yana ukweli kuhusiana na sekta zao mbalimbali.

RAIS SAMIA AWAKARIBISHA DIASPORA  NA RAIA WA KIGENI KUWEKEZA NCHINIRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Su...
19/05/2025

RAIS SAMIA AWAKARIBISHA DIASPORA NA RAIA WA KIGENI KUWEKEZA NCHINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewakaribisha Watanzania wanaoishi Nje ya nchi maarufu k**a Diaspora pamoja na Raia wa Kigeni na Sekta zao binafsi kuja kuwekeza nchini Tanzania, akieleza kuwa sasa Sera ya Mambo ya nje inawatambua rasmi k**a wabia muhimu wa maendeleo ya Tanzania.

Aidha Rais Dkt. Samia ameeleza kuwa uhusiano na Diplomasia ya Kimataifa ni suala linalohusu pia ulinzi na usalama wa nchi hivyo ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama nchini Tanzania kuhakikisha kuwa wanajidhatiti katika kudhibiti vitendo vya uhalifu wa kuvuka mipaka pamoja na matendo ya kigaidi yanayoendelea kote duniani kwa kuhakikisha mipaka inakuwa salama na amani inatamalaki nchini.

Rais Samia amebainisha hayo leo Jumatatu Mei 19, 2025 kwenye Hafla ya uzinduzi wa sera ya mambo ya nje ya Mwaka 2001, toleo la mwaka 2024, akiwahamasisha Watanzania wanaoishi nje ya nchi kuwa mabalozi wema wa Tanzania kwa kutangaza mazuri na fursa zinazopatikana nchini Tanzania.

Aidha Rais Samia ametoa wito kwa watanzania hususani Vijana pamoja na sekta binafsi nchini, kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi na kijamii zilizopo nchini, akizitaka Mamlaka zinazosimamia ajira nje ya nchi kuja na sera na sheria rafiki kwa Watanzania ili waweze kufaidika na mahusiano mema ya Tanzania na Mataifa mengine ambayo yamekuwa yakitoa fursa za ajira kwa raia wa kigeni.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua Sera ya Mambo ya Nje ya mwaka 2001 Tole...
19/05/2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua Sera ya Mambo ya Nje ya mwaka 2001 Toleo la Mwaka 2024 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Mei, 2025.

17/03/2025

"Tumewaahidi wananchi kuimarisha usimamizi wa sekta hii, na ni lazima ahadi hiyo itimie. Katika kulitekeleza hilo, Mheshimiwa Waziri pamoja na Menejimenti ya Wizara, kuna jambo nilikuwa nasikiliza kwa makini ulipokuwa ukizungumza. Niliposikia unasema... ‘tunafanya katika ngazi yetu, tunashirikiana...’ nilikuwa nasikiliza kwa makini, lakini kichwani kwangu nilikuwa nawaza jambo.

Ikiwa tumeweza katika upande wa uwekezaji kuweka huduma zote ndani ya nyumba moja—kuanzia upimaji, usajili, usimamizi wa ardhi hadi utoaji wa hati—nadhani hata hili linawezekana. Tunaweza kuwa pamoja, na hili litawezekana endapo mtakuwa na chombo kinachoitwa Kamisheni ya Ardhi.

Nimeona ndani ya wizara mna Makamishna na mna Kamishna Mkuu wa Ardhi, lakini ukweli ni kwamba kamishna hawezi kuwepo bila kuwa na kamisheni. Basi, nawaomba mkalitazame upya suala hili—muundo wake mpya. Katibu Mkuu Kiongozi yupo hapa, kaangalieni umuhimu wa kuwa na Kamisheni ya Ardhi na kubainisha vizuri majukumu yake. Nadhani hii itarahisisha zaidi utendaji wenu. Kwa hiyo, litazameni hilo kwa umakini."

Amesema Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa uzinduzi wa Sera ya Ardhi ya mwaka 1995, Toleo la mwaka 2023, leo Machi 17, 2025, katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma.

17/03/2025

Serikali imepanga kuongeza kasi ya usajili wa ardhi nchini licha ya hatua kubwa zilizopigwa katika upimaji wa ardhi, ambapo takwimu zinaonesha kuwa takribani asilimia 75 ya ardhi bado haijasajiliwa. Hali hii haichangii tu kupotea kwa mapato ya serikali, bali pia inasababisha ukosefu wa usawa kwa kuwa baadhi ya wamiliki wa ardhi wanalipia umiliki wao huku wengine hawalipi, jambo ambalo si sawa wala haki.

Katika kukabiliana na changamoto hiyo, serikali imebaini kuwa sera iliyopita haikuwa na sharti la kuwataka wamiliki wa ardhi kusajili ardhi yao. Hivyo, kupitia sera mpya, serikali imekusudia kuhakikisha kuwa kila kipande cha ardhi ndani ya nchi hii kipangwe, kipimwe na kisajiliwe rasmi.

Akizungumza leo Machi 17, 2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma, wakati wa uzinduzi wa Sera ya Ardhi ya mwaka 1995, Toleo la mwaka 2023, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa kuna kesi nyingi ambazo watu hupoteza ardhi yao kiholela kutokana na udanganyifu unaofanywa na baadhi ya watu wasio waaminifu.

“Mtu anamiliki ardhi yake kihalali, lakini matapeli wanashirikiana na baadhi ya watu ndani ya wizara kubadilisha hati za umiliki, hali ambayo hupelekea migogoro ya ardhi mahak**ani na mmiliki halali kunyang’anywa haki yake. Haya yote tunakwenda kuyaondoa, ndugu zangu,” amesema Rais Samia.

Rais amesisitiza kuwa mfumo mpya wa usajili wa ardhi utaweka msingi imara wa uwazi na haki kwa wamiliki wote wa ardhi, huku ukidhibiti mianya ya udanganyifu na kuongeza mapato ya serikali kupitia kodi halali za umiliki wa ardhi.

19/01/2025

Mtaalam na mchambuzi wa masuala ya Siasa na mai Maendeleo Dkt. Dennis Muchunguzi amemwagia sifa Makamu Mwenyekiti wa CCM bara Ndugu, Stephen Wasira baada ya kuchaguliwa kwa Kishindo na wajumbe wa Mkutano mkuu Maalum wa CCM uliofanyika jana Tarehe 18 Januari 2025 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika Januari, 2025.
30/12/2024

Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika Januari, 2025.



NUKUU:"Waambieni watu wema wao na uzuri wao, inaweza wasaidia na kuwapa nguvu ya kuendelea kutenda mema kuliko kuja kuel...
22/11/2024

NUKUU:

"Waambieni watu wema wao na uzuri wao, inaweza wasaidia na kuwapa nguvu ya kuendelea kutenda mema kuliko kuja kueleza baadae wakiwa hawana uwezo wa kusikia wala kuona" - Samweli Sasali .samsasali360 : Mwanahabari.

02/08/2024

DIWANI WA MAGOLE KILOSA AWAITA WANAWAKE KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA

Diwani wa tarafa ya Magole wilaya ya Kilosa Bi Raheli Elia Kazimoto amemshukuru Rais Samia kwa niaba ya wanawake wa Kilosa kwa kutembelea wilaya yao pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya barabara, vituo vya afya na elimu.

Sambamba na hilo ametoa wito kwa wanawake wote wa Tanzania kumuunga mkono Rais Samia kwa mengi makubwa aliyoyafanya licha ya watu wengi kutokuwa na imani na utendaji wa wanawake hasa katika masuala ya uongozi. Amesema,

"Wakina mama wote Tanzania hii mnaonisikiliza
tumuunge mkono mama Samia Suluhu Hassan ni mwanamke katika wanawake amefanya mambo mengi kwenye nchi hii mpaka tunakosa namna ya kusema"

02/08/2024

WAFUGAJI WAMFAGILIA RAIS SAMIA KWA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI

Jamii ya wafugaji wa wilaya ya Kilosa imempongeza Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutatua changamoto ya migogoro ya ardhi ambayo kwa muda imekuwa ikiwatesa wakulima na wafugaji hasa katika wilaya ya Kilosa ambapo mara kwa mara wafugaji na wakulima walikuwa wakishambuliana kufuatia kugombania ardhi.

Akizungumza kwa niaba ya wafugaji wengine wakati ziara ya Rais ilipofika wilaya ya Kilosa mwananchi Shaka Stoni ambaye ni mfugaji amesema,

"Kwa niaba ya kilosa na wafugaji wote niseme sisi wafugaji tunamfurahia mama kwa kuwa tangu alipokaa kwenye kiti hatujawahi kuona ugomvi kabisa na bei ya mifugo imeongezeka sisi k**a wafugaji tunampenda sana na tunataka aendelee kwa sababu mama ndio chaguo letu".

02/08/2024

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa na nia ya dhati ya kusogeza huduma za afya karibu na wananchi na ndiyo sababu ya yeye kuboresha kituo cha afya ambacho hakikuwa na miundombinu za kutosha kuwahudumia wananchi wa Gairo.

"Hospitali hii imekamilika kwa kiasi kikubwa kwa sababu huduma za upasuaji kwa ajili ya kuna mama wajawazito zinapatikana hapa, watu hawatakwenda tena Morogoro Mjini au Dodoma kwa ajili ya kupata huduma za upasuaji" Ameeleza Ummy Mwalimu.

Aidha Waziri Ummy amesema kwamba hospitali hiyo ina huduma za kisasa za mionzi katika hospitali hiyo akisema kuwa kwa mkoa mzima wa Morogoro hakukuwa na Digital X- Ray hata moja lakini kwa sasa mkoa una digital x- Ray nane ikiwamo iliyofungwa kwenye hospitali hiyo.

Licha ya hatua zinazozidi kupigwa, Waziri Ummy amesema kuwa bado kuna changamoto ya wananchi kujiunga na mifumo ya bima za afya ambayo imesababisha gharama kubwa kwa wananchi kupata huduma ya afya na kuwaomba Wanagairo na Watanzania kwa ujumla kujiunga na bima ya afya.

06/07/2024

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kiuchumi nchini Dkt Denis Mchunguzi ameeleza kwa undani zaidi tukio la aliyekuwa mbunge wa Iringa mjini na kada maarufu wa CHADEMA Mchungaji Peter Msigwa kuamia CCM.

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Taifa Digital Forum posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Taifa Digital Forum:

Share