03/02/2022
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Hussein Ali Mwinyi ametengua uteuzi wa viongozi katika Wizara za elimu, Uchumi na Uwekezaji na wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo.
Taarifa hiyo iliyotolewa na kusainiwa na Katibu Mkuu Mtendaji, Zena Said leo Februari 3, 2022 imewataja waliotenguliwa ni pamoja na Mkurugenzi wa idara ya Utumishi na Uendeshaji Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Omar Ali Omar.