12/11/2025
Msimamizi wa Aziz ANDABWILE andabwile_02 anaitwa Hilary akiongea na CROWN SPORTS ya , kabla ya kuongea na Hilary Crown FM iliulizia kwanza TFF k**a kweli kuna kesi yoyote ya Yanga SC na mchezaji wake ANDABWILE tukajiridhisha kwamba shauri hilo lipo.
Hakuna mwenye nia ya kumchafua yoyote ila ni kufikisha taarifa kwa umma kwa kufuata weledi, kuna ambayo tunayajua na ushahidi tunao kwenye jambo hili, hata caption tulianza kuiona kabla ya kupostiwa, tusillazimishane kuonyesha kilakitu.
Tukubaliane vilabu kudaiwa ni kawaida na Yanga SC kudaiwa na kufikishwa FIFA na TFF ni kawaida sana kwa siku za karibuni, acheni kabisa kuwatisha waandishi wakifanya kazi zao.
Wakati mwingine hatuwezi kusema kilakitu kwa sababu za kimahusiano zaidi na kupevuka kwa fikra zetu, lakini tusionane k**a wote ni sawa na wale wanaopewa vijihela, NO, BIG NO. Ila kumbukeni wachezaji hawa ni ndugu zetu, wanetu, majirani zetu, watoto wetu, etc, wakitoka kwenu tunakuwa nao kitaa, msijisahulishe sana.
Vijana (wachezaji) hivi vilabu vishapendwa sana, sasa mkiweka mapenzi mbele mtaula wa chuya, watu wanajuta kwa kujifanya wanavipenda hivi vilabu. Pia kudai haki zenu sio dhambi mkiogopa kujisimamia itakula kwenu, sio unatishwa kidogo unajikojolea huo wakati haupo na hayo unayodai ni maslahi na haki yako na kufanya hivyo si dhambi. Mbaya pale unaleta jambo usaidiwe halafu baadae unaenda kulazimishwa kukana, wakati ukweli unaujua. Kuna wengi mnakufa kisabuni na hamtaki kusema, Shauri yenu.
ββββBIN KAZUMARI MTIPA (Real voice of voiceless)