23/04/2024
Watuhumiwa watatu wamefikishwa Mahak**a ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoani Pwani jana tarehe 22 Aprili, 2024 wakikabiliwa na mashtaka ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Methemphetamine Kilogramu 424.84 pamoja na He**in Hydrochloride gramu 158.24 kinyume cha kifungu cha 15 (1) (a) na cha (3) (i) cha Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Sura ya 95 k**a illivyorejewa 2019.
Washtakiwa hao ni Rajabu Kisambwanda (42) mkazi wa Kerege Matumbi, Bakari Said (39) Mkazi wa Kunduchi Mtongani na Hillary Rhite (35) Mkazi wa Kunduchi Sodike.
Wakisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Joyce Mkhoi na Wakili wa Serikali, Agness Ndanzi, alidai mahak**ani hapo kuwa, washtakiwa hao watatu walikutwa wakisafirisha dawa hizo za kulevya mnamo tarehe 10 Aprili, 2024 eneo la Zinga wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani .
Wakili Ndazi aliendelea kuieleza Mahak**a kuwa, katika tukio lingine, tarehe hiyohiyo mshtakiwa Bakari Said (39) Mkazi wa Kunduchi Mtongani alikutwa akisafirisha dawa za kulevya aina ya He**in hydrochloride yenye uzito wa gramu 158.24.
Hata hivyo washtakiwa wote watatu hawakuruhusiwa kujibu chochote kwani Mahak**a hiyo haina Mamlaka ya kisheria kusikiliza shauri hilo na watafikishwa tena mahak**ani kwa ajili ya kutajwa tarehe 7 mwezi Mei, 2024.
Katika tukio lingine, watuhumiwa wengine tisa (9) wamefikishwa Mahak**a ya Hakimu Mkazi Kisutu jana tarehe 22 Aprili, 2024 wakikabiliwa na mashtaka ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya he**in na methamphetamine zenye uzito wa kilogramu 332.
Akisoma mashtaka yao mbele ya mahak**a hiyo, wakili wa serikali Batilda Mushi amewataja washtakiwa hao kuwa ni Ally Ally (28), Bilali Hafidhi (31), Mohamed Hamisi (47), Idrisa Mbona (33), Rashid Rashid (24), Shabenga Shabenga (24), Dunia Mkambilah (52), M***a Hussein (35) na Hamis Omary (25).
Amesema, katika shtaka la kwanza, tarehe 16 Aprili, 2024 karibu na hotel ya white sands wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, washtakiwa walikutwa wakisafirisha dawa za kulevya aina ya Methamphetamine kiasi cha kilgramu 100.83.