17/09/2025
KISA CHA NABII M***A (A.S) NA KHIDR
Kisa chetu cha leo kutoka katika Qur’ani ni hadithi ya mwanafunzi maarufu wa elimu ambaye alianza safari ya kutafuta elimu baada ya kuwa nabii. Ni hadithi ya Nabii Musa na Khidr, na hadithi hii imetajwa katika Qur’ani Tukufu na pia katika Hadith za Mtume Muhammad (s.a.w).
Sababu ya kushuka kwa hadithi hii katika Qur’ani kwa Mtume Muhammad (s.a.w):
K**a ilivyopokelewa katika hadithi ya Mtume (s.a.w) kutoka kwa Ibn Abbas, siku moja Nabii Musa alisimama akihutubia watu wake. Baada ya kumaliza hotuba yake, mmoja wa watu wa Bani Israil akamuuliza: "Ewe Musa, je, kuna mtu yeyote duniani aliye na elimu kuliko wewe?" Musa akajibu: "Hapana. Mimi ndiye mwenye elimu zaidi duniani."
Hapo Allah akamlaumu Nabii Musa(a.s) kwa kutorudisha Nabii M***a elimu kwa Allah (yaani hakusema 'Allah ndiye ajuaye zaidi'). Kisha Allah akamwambia Musa: "Ewe Musa, kuna mtu mmoja mahali panapoitwa 'Makutano wa Bahari Mbili' (Majma’ul-Bahrayn), ana elimu zaidi kuliko wewe. Nenda kwake ukajifunze."
Hapo Musa akamuamuru mtumishi wake Yusha’ bin Nun ajiandae kwa safari ya kumtafuta mtu huyo. Allah alimpa Musa alama ya kumwelekeza mahali mtu huyo alipo: Atakapopoteza samaki waliowekwa kwenye chombo chake, baasi hapo ndipo atakapomkuta.mtu huyo.
Allah anasema katika Qur’ani:
“Na Musa akamwambia kijana wake: ‘Sitakoma mpaka nifike mahali zinapokutana bahari mbili, au nitembee muda mrefu.’ Walipofika mahali pa kukutana bahari mbili, walimsahau samaki wao, naye alichukua njia yake baharini kwa njia ya ajabu. Walipokwisha pita, Musa akamwambia kijana wake: ‘Lete chakula chetu; kwa yakini tumepata taabu sana katika safari yetu hii .’” (Surat Al-Kahf 18:60–62)
Baada ya kuanza safari, Musa na mtumishi wake walitembea hadi wakafika kwenye jabali na wakakaa kupumzika. Wakiwa wamelala, samaki akaruka kutoka kwenye chombo na kuingia baharini kwa namna ya ajabu – maji yalikuwa yakipasuliwa naye samaki, kisha yanagandia nyuma yake.
Walipoamka, waliendelea na safari. Baada ya siku moja na nusu, Musa akamwambia kijana wake: "Tule chakula chetu." Hapo mtumishi akakumbuka tukio la samaki na akamwambia Musa:
“Je, unakumbuka tulipoketi kwenye lile jabali? Nilimsahau yule samaki. Na aliyenisahaulisha ni Shetani, nisimsimulia. Naye alichukua njia yake baharini kwa ajabu.” (18:63)
Musa akasema: "Hicho ndicho tulichokuwa tukikitafuta!" Basi walirudi kwa kufuata alama zao hadi wakamkuta mja miongoni mwa waja wa Allah ambaye Allah alimpa rehema kutoka kwake na alimfundisha elimu kutoka kwake.
Kitu cha muhimu hapa ni hiki: Ingawa Musa ni Nabii, Allah alimwamuru atafute elimu kwa mtu ambaye daraja lake ni la chini kuliko yeye, yaani Khidr. Hii inatufundisha umuhimu wa kutafuta elimu.
Mtume Muhammad (s.a.w) alikuwa kila mara akihimiza umma wake kutafuta elimu. Alisema:
"Fikisheni kutoka kwangu hata aya moja."
Na alisema kuhusu fadhila za elimu:
“Yeyote anayelingania kwenye uongofu atapata thawabu sawa na yule anayefuata hadi Siku ya Kiyama.”
Pia Mtume alisema:
"Pindi akifa mwanadamu , Amali zake zote hukatika isipokuwa mambo matatu: Sadaka yenye kuendelea, au elimu yenye kupatikanwa manufaa au mtoto mwema mwenye kumuombea Dua Mzazi wake"
Na alisema tena:
"Mwenye kupita njia hali ya kuwa anataka ktk njia hiyo ilmu, Allah humrahisishia njia ya kwenda Peponi. Hakika Allah, malaika Wake, viumbe wa mbinguni na ardhini – hadi mchwa kwenye shimo lake, na hata samaki majini – humuombea rehema yule anayefundisha watu mema."
Wanazuoni na watu wema walipojua maneno haya ya Mtume (s.a.w), walijitolea maisha yao yote kwa ajili ya elimu. Safari ya kumjua Allah inahitaji elimu ya nguvu, juhudi za kiutendaji, bidii kubwa, na umakini.
Nabii Daud alisema:
"Elimu moyoni ni k**a taa ndani ya nyumba."
Na Luqman al-Hakim alimwambia mwanawe:
"Ewe mwanangu, kaa na wanazuoni na waandame kwa magoti yako, kwani Allah huhuisha mioyo kwa nuru ya hekima na elimu k**a anavyohuisha ardhi kwa mvua kutoka mbinguni."
Hivyo, somo na faida kutoka katika hadithi ya Musa na Khidr ni kwamba hata mtu mwenye daraja ya juu k**a Musa, alisafiri mamia ya kilomita kutafuta elimu kwa mtu wa daraja la chini kuliko yeye.
Sufyan ath-Thawri alisema:
"Mtu hawezi kuwa na heshima ya kweli mpaka ajifunze kutoka kwa walio juu yake, walio chini yake, na walio sawa naye."
Ushauri wangu kwenu ni: tutafuteni elimu!
Allah awalipe kheri. Na avijaze vizazi vyenu ilmu yenye manufaa duniani na akhera, aamiin🤲
K**a umemaliza kusoma, mswalie Mtume Muhammad (s.a.w)❤️❤️❤️
Like, Share and
Sufian Mzimbiri & Mzimbiri TV