19/04/2026
UTAMBULISHO WA MUONEKANO RASMI WA BMH ENTERTAINMENT (THE MOTHER BRAND)
Tunayo furaha na fahari kubwa kuwatambulisha muonekano rasmi (Official Logo) ya BMH Entertainment. Hii ndiyo "Logo Mama" na moyo wa kampuni yetu, inayobeba maono, mwelekeo, na mwavuli wa vitengo vyetu vyote vya BMH Music , BMH Film, BMH Media , BMH Talent, na BMH Academy.
Chini ya uongozi wa CEO & Founder Amos Kiula , BMH Entertainment imesimama k**a kituo kikuu cha ubunifu na habari. Logo hii si tu alama ya biashara, bali ni nembo ya Nguvu, Thamani, na Harakati ambazo kampuni yetu inazipitia katika kuleta mapinduzi ya kitalamu nchini na duniani kote.
Hapa ndipo moyo wa BMH ulipo—mahali ambapo kila wazo linageuzwa kuwa uhalisia kwa kutumia kauli mbiu yetu ya kudumu: "Excellence in Motion".
ILANI YA KISHERIA (Copyright Notice):
© 2026 BMH Entertainment. Haki zote zimehifadhiwa. Alama hii (Logo) ni miliki halali ya BMH Entertainment. Hairuhusiwi kuitumia, kuinakili, au kuisambaza kwa namna yoyote ile kwa madhumuni ya kibiashara au binafsi bila idhini ya maandishi kutoka kwa uongozi wa kampuni. Ukiukwaji wa ilani hii utapelekea hatua kali za kisheria chini ya mamlaka husika (BRELA, COSOTA, TRA & TCRA).
KWA WADAU NA MASHABIKI WETU:
Huu ndio utambulisho wetu mkuu! Je, una maoni gani kuhusu muonekano huu wa Logo Mama ya BMH Entertainment? Angusha maoni yako hapa chini! 👇✨