
14/08/2025
Najua kwa hali hii siwezi tena kupona Afande, najua nitawachosha vitani, najua mtaumia sana bila mimi kwakuwa tuliingia wote Jeshini
Nimezikumbuka zile stori zetu za utani nyakati za furaha enzi zile Kuruta tu! Nimezikumbuka zile W3, naomba nikutajie tena Rafiki yangu
Unakumbuka nilikwambia kitu kuhusu War? Ndio hii vita Ndugu yangu tupo hapa tunapambana ijapo mimi nipo taaban, vita hii tunapambana ila Ndugu yako tayari siko salama
Nikuombe kitu, nenda usimame, chukua silaha yako mimi nisogeze tu pale pembeni, nitalala kuwasubiri k**a mtarudi na ushindi au mwili wangu uwe chakula cha Tai na Fisi
Lakini najua lazima mshinde, k**a mtashinda basi uje hapa Rafiki yangu, nataka mwili wangu ufunikwe bendera ya Taifa langu, napenda sana kuona hivyo
K**a nifika msinizike hapa, chukueni mwili wangu upelekeni nyumbani, pale nyumbani walipo wazazi wangu, haijalishi wataona nini wakiufunua mwili wangu
Wakiuliza kuhusu makovu waambie walinizaa kwa ajili ya taifa langu, Mtoto wao nilikufa nikipambania taifa langu, wakiuliza kuhusu majeraha waambie uhai wangu lazima utolewe kwa nguvu mimi ni Mwanajeshi
Nilikwambia nikifa nipeleke nyumbani walipo wazazi wangu, hiki kidani mpe Mwanangu, hii kacha mpe Mke wangu na Mama akilia sana mwambie Mwanajeshi mwanao alikufa huku akitabasamu
If i die, dont burry me here, take my body to my Parents 🙏