02/08/2024
MAONESHO YA NANE NANE 2024 NI TOFAUTI NA NANE NANE ZILIZOTANGULIA
Wananchi mbalimbali waliohudhuria Maonesho ya Nane Nane 2024 katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma wamepongeza maandalizi mazuri ya Maonesho hayo ya Kimataifa ya Kilimo, Uvuvi na Ufugaji yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa jana Agosti 01, 2024 huku yakitarajiwa kufungwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Agosti 08, 2024 (88)
"Nimefika hapa kwenye maonesho ya Nane Nane 2024, nimekuta mabadiliko makubwa sana, tuna kila sababu ya kumpongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Kilimo kwa jitihada zao katika kuwezesha maonesho ya Nane Nane 2024 kuwa hivi, kumejengwa tofauti sana" - Alisema Merkiori Tesha, baada ya kutembeela mabanda mbalimbali viwanja vya 88 Nzuguni Dodoma.
Kwa upande wake, Zaina Mwakijazi, Mkazi wa Makulu Dodoma, yeye amesema Nane Nane ya Mwaka huu imekuwa na maandalizi makubwa zaidi tofauti na miaka iliyopita kwanzia kwenye mazingira lakini pia wafanyabiashara wamejitokeza kwa wingi sana na kuna vitu vingi vizuri.