
08/07/2023
Mmiliki wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Elon Musk, kupitia wakili wake, ametishia kuishtaki Meta baada ya mtandao wake tanzu wa Instagram kuzindua program (application) mpya inayoitwa Threads, inayolenga kutoa ushindani na kuwa mbadala wa Twitter.
Katika barua iliyotumwa kwa mkurugenzi wa Meta, Mark Zuckerberg, na kuchapishwa mitandaoni hapo jana, wakili wa Musk, Alex Spiro, ameituhumu kampuni hiyo kwa kutumia siri za kibiashara za mtandao Wake pamoja na haki miliki nyingine.