TBCDodoma

TBCDodoma Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from TBCDodoma, Media/News Company, Dodoma.

Nini mtazamo wako kwa baadhi ya watu wasiotoa msaada wa matibabu  kwa ndugu zao  pindi wanapohitaji?Wakisikia wameaga du...
26/08/2025

Nini mtazamo wako kwa baadhi ya watu wasiotoa msaada wa matibabu kwa ndugu zao pindi wanapohitaji?
Wakisikia wameaga dunia ndipo wanapohangaika kugharamia gharama za mazishi.
Katika ABRA 93.7 TBC REDIO JAMII DODOMA tunajadili hilo kwenye Mada Mezani.
Shiriki nasi kwa kutoa maoni kwani mchango wako ni muhimu.
Kuanzia saa 3.00 Asubuhi -6.00 Mchana

Tunapatikana kwenye mitandao ya kijamii.

Facebook TBCDodoma
Instagram tbc_dodoma

Magazeti ya Leo Agost 26,2025
26/08/2025

Magazeti ya Leo Agost 26,2025

Katika mada mezani leo mdau wa  ABRA  93.7 FM TBC REDIO JAMII  DODOMA tunajadili kuhusu tabia ya baadhi ya wanaume kuwaf...
25/08/2025

Katika mada mezani leo mdau wa ABRA 93.7 FM TBC REDIO JAMII DODOMA tunajadili kuhusu tabia ya baadhi ya wanaume kuwaficha wake zao kiwango cha mshahara wanaolipwa. Je, sababu ni nini?

Toa maoni yako kupitia mitandao yetu ya kijamii.
Katika akaunti yetu ya Instagram: tbc_dodoma.
Facebook: TBCDodoma.
ujumbe wako ni muhimu tutausoma ktk kipindi.

Kuanzia saa 3.00 Asubuhi -6.00 Mchana.

25/08/2025
Klabu ya Yanga imetangaza jezi zao mpya zitakazotumiwa na kikosi na benchi la ufundi kwa ajili ya msimu mpya wa 2025/202...
24/08/2025

Klabu ya Yanga imetangaza jezi zao mpya zitakazotumiwa na kikosi na benchi la ufundi kwa ajili ya msimu mpya wa 2025/2026.

Jezi hizo za nyumbani, ugenini na jezi ya tatu (Third Kit) za mabingwa hao wa kihistoria zimetambulishwa rasmi kwa mashambiki leo tarehe 24, Agosti 2025 na tayari zimeanza kuuzwa maeneo mbalimbali nchini.

Chama Cha Mapinduzi-CCM kimemteua, Fadhili Ngajilo kuwa mgombea wake wa ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini mkoani Iringa.Ua...
23/08/2025

Chama Cha Mapinduzi-CCM kimemteua, Fadhili Ngajilo kuwa mgombea wake wa ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini mkoani Iringa.

Uamuzi huo umetangazwa leo tarehe 23, Agosti 2025, kupitia taarifa ya Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla. Katika jimbo hilo miongoni mwa waliokuwa wakiwania kupeperusha bendera ya CCM ni mwanasiasa mkongwe, Peter Msigwa.

Chama Cha Mapinduzi-CCM kimempitisha, Daniel Chongolo kuwa mgombea ubunge wake Jimbo la Makambako mkoani Njombe.Jina la ...
23/08/2025

Chama Cha Mapinduzi-CCM kimempitisha, Daniel Chongolo kuwa mgombea ubunge wake Jimbo la Makambako mkoani Njombe.

Jina la Chongolo limetangazwa kupitia taarifa ya Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla. Jimbo la Makambako lilikuwa likiongozwa na Deo Sanga maarufu ‘Jah People’.

Chama Cha Mapinduzi-CCM kimempitisha Paul Makonda kuwa mgombea ubunge wake Jimbo la Arusha Mjini.Jina la Makonda limetan...
23/08/2025

Chama Cha Mapinduzi-CCM kimempitisha Paul Makonda kuwa mgombea ubunge wake Jimbo la Arusha Mjini.

Jina la Makonda limetangazwa leo tarehe 23, Agosti 2025, na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla.

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua, Amos Makalla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha akichukua nafasi ya Kenani Kihongosi aliyete...
23/08/2025

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua, Amos Makalla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha akichukua nafasi ya Kenani Kihongosi aliyeteuliwa kuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt Moses Kusiluka, uteuzi wa Makalla ambaye alikuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM umefanyika leo tarehe 23, Agosti 2025.

Taarifa hiyo pia imesema uapisho wa Makalla utafanyika tarehe 26, Agosti mwaka huu Saa 5:00 asubuhi Ikulu Chamwino, Dodoma.

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula ametemwa kwenye uteuzi wa wagombea ubunge wa Cham...
23/08/2025

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula ametemwa kwenye uteuzi wa wagombea ubunge wa Chama Cha Mapinduzi na badala yake Nzilanyingi John ameuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu ujao.

Uteuzi wa Nzilanyingi umetangazwa leo tarehe 23, Agosti 2025, na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla.

Address

Dodoma

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when TBCDodoma posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to TBCDodoma:

Share