NINO TV

NINO TV Media entertainment |Music |sports| political |social | Religious News 🌍

Nani atauzima mziki wa Mix by Yas 😂FULLTIMESimba SC 1-0 KenGold Sc🏟️KMC Complex⚽ ⚽Ateba🏆  Powered by 🎂     🌍
18/12/2024

Nani atauzima mziki wa Mix by Yas 😂

FULLTIME

Simba SC 1-0 KenGold Sc
🏟️KMC Complex

⚽ ⚽Ateba

🏆
Powered by 🎂
🌍

Mwanamuziki kutoka Nchini Nigeria Wizkid, ameingia kwenye vichwa mbalimbali vya habari mara baada ya kumzawadia dada yak...
18/12/2024

Mwanamuziki kutoka Nchini Nigeria Wizkid, ameingia kwenye vichwa mbalimbali vya habari mara baada ya kumzawadia dada yake gari aina ya ‘Big body Range Rover 2025’yenye thamani ya dola za kimarekani $150,000 sawa na zaidi ya Milioni mia tatu kwa hela za Kitanzania kuelekea kusherekea sikukuu ya krismasi.

Powered by 🎂
🌍

Mtoto King John Mseke (9) ambaye ni Mtoto wa Msanii Staa wa Hiphop Tanzania Joh Makini (  ), amewasili katika Academy ya...
17/12/2024

Mtoto King John Mseke (9) ambaye ni Mtoto wa Msanii Staa wa Hiphop Tanzania Joh Makini ( ), amewasili katika Academy ya Club ya Manchester City iliyopo Jijini Manchester Nchini Uingereza kwa ajili ya mafunzo ya soka.

Joh Makini ameiambia kuwa mwaliko huo kutoka Manchester City Football Academy ni nafasi kubwa na ya kipekee katika maisha ya King ambaye ndoto yake kubwa siku zote imekuwa ni kucheza mpira na kwamba haikuwa rahisi kufika Manchester City Academy kwani ni nafasi ambayo Joh amekuwa akiipambania kwa muda mrefu

“Ni stori ndefu sana, hivi ni vitu ambavyo tumekuwa tukitafuta wenyewe na kuvifanyia kazi kwa miaka kuhakikisha kipaji cha Mtoto kinaonekana, King alianza mafunzo serious akiwa na miaka minne au mitano baada ya kumuona ana kipaji ilibidi niivalie njuga sikutaka kuchukulia poa kabisa” - Joh Makini.

King ( ) ambaye ni Mwanafunzi wa darasa la tano, aliondoka Tanzania kwenda Uingereza Ijumaa December 13 2024 ambako atakuwa kwenye mafunzo hayo ya Manchester City kwa muda wa wiki mbili “haya mafunzo unapata mwaliko kutokana na juhudi zako na uwezo wa Mtoto”.

“Wakishamaliza mafunzo wanaandaa ripoti jinsi walivyomuona Mtoto na pia wanakushauri vitu vya kufanyia kazi, unajua wale wako mbele sana wana vipimo vyao Mtoto anapimwa kila kitu yani wanaweza kukwambia mpaka shuti la huyu Mtoto uzito wake, mikimbio yake kitaalamu n.k, naamini hii safari yake itafungua milango mingi sana kwa huyu Mtoto” ——— Joh Makini.

Powered by 🎂
🌍

“Mwanamke ujue kupika ugali, uwe flexible na uwe na sauti ya kutoa nyoka pangoni. Nyash sio issue 😂” - Ameandika .Powere...
22/11/2024

“Mwanamke ujue kupika ugali, uwe flexible na uwe na sauti ya kutoa nyoka pangoni. Nyash sio issue 😂” - Ameandika .

Powered by 🎂
🌍

📸 Familia, ndugu na jamaa na marafiki wamefika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kwa jailli ya kupokea miili ya ndugu zao w...
18/11/2024

📸 Familia, ndugu na jamaa na marafiki wamefika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kwa jailli ya kupokea miili ya ndugu zao waliofariki katika maporomoko ya ghorofa la Kariakoo Jijini DSM.

Poleni sana familia, ndugu na marafiki mliowapoteza wezetu katika maporomoko ya ghorofa la Kariakoo, Mungu azidi kuwapa nguvu na subra katika kipindi hiki kigumu 🙏🏽🙏🏽



Miili ya watu waliofariki kwenye Ajali ya kuporomoka kwa jengo la Biashara la Kariakoo siku ya November 16,2024 inaagwa ...
18/11/2024

Miili ya watu waliofariki kwenye Ajali ya kuporomoka kwa jengo la Biashara la Kariakoo siku ya November 16,2024 inaagwa muda huu kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.


Mhe Damas Ndumbaro Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo tayari amewasili Leaders Club ambapo inafanyika ibada ya kuuaga...
18/11/2024

Mhe Damas Ndumbaro Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo tayari amewasili Leaders Club ambapo inafanyika ibada ya kuuaga mwili wa mpendwa wetu King Kikii.


Powered by 🎂
🌍

Wakati zoezi la kutoa misaada mbalimbali likiendelea kwa wahanga wa ajali ya Kariakoo, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mk...
18/11/2024

Wakati zoezi la kutoa misaada mbalimbali likiendelea kwa wahanga wa ajali ya Kariakoo, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, na Uratibu, Dkt. Jim James Yonazi, ametoa wito kwa wananchi kuwa makini na michango inayoendeshwa kwa ajili ya msaada wa wahanga.

Dkt. Yonazi amesisitiza kuwa akaunti inayokusanya michango ya fedha ni moja pekee na sio nyingine, na kwamba michango yote inayohusu tukio hili inapaswa kwenda kwenye akaunti maalum ya serikali.

“Michango yote inayohusu tukio hili inakwenda kwenye akaunti maalum ambayo ni ya serikali,” alieleza Dkt. Yonazi, akiwataka wananchi kutofanya michango kupitia akaunti zisizo rasmi ili kuepuka udanganyifu.

Hii ni katika kuhakikisha michango inafika kwa wahanga wa ajali hiyo na kusaidia juhudi za uokoaji na matibabu.
Powered by 🎂
🌍

NINO MEDIA GROUP, inaungana na wananchi wote wa Tanzania kuwapa pole Wafanyabiashara wa KARIAKOO, kipekee salamu za pole...
17/11/2024

NINO MEDIA GROUP, inaungana na wananchi wote wa Tanzania kuwapa pole Wafanyabiashara wa KARIAKOO, kipekee salamu za pole zifike kwa ndugu na jamaa wa wafiwa wote pamoja na majeruhi.

NINO MEDIA iko bega kwa bega na wote walioathirika katika kipindi hiki kigumu.
Tunawatakia majeruhi kupona kwa haraka na Faraja kwa wote walioathirika kwa njia moja ama nyingine.


Hali ilivyo usiku huu soko Kuu la Kimataifa la Kariakoo Mtaa wa Kongo Mchikichini kwenye jengo la ghorofa lililoporomoka...
16/11/2024

Hali ilivyo usiku huu soko Kuu la Kimataifa la Kariakoo Mtaa wa Kongo Mchikichini kwenye jengo la ghorofa lililoporomoka.

Hadi kufikia saa 11:00 jioni watu 70 wameokolewa wakiwa hai lakini kwa mujibu wa taarifa za kidaktari watu 4 tu ndio wamepoteza maisha.
🌍

Address

Dodoma

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00
Sunday 09:00 - 17:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when NINO TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share