Baesadigital

Baesadigital Informing, Educating and Entertaining Knowledge for all.

Ukusanyaji mapato wafikia trilioni 7.5 sekta ya utalii. Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Uta...
25/01/2025

Ukusanyaji mapato wafikia trilioni 7.5 sekta ya utalii.

Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Gerson Msingwa amesema kumekuwa na ongezeko la ukusanyaji wa mapato katika sekta ya utalii kufikia trilioni 7.5 kwa mwaka 2023/2024 ambapo hapo awali mapato hayo yaliishia trilioni 2 hadi 3 pekee.

Msigwa amebainisha hayo Januari 25, Mwaka huu wakati akizungumza na waandishi wa habari ndani ya hifadhi ya Taifa ya Mikumi iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro.

Akifafanua zaidi, Msigwa amesema mapato hayo yametokana na ongezeko la watalii katika hifadhi za Taifa kutoka watalii 1,618,538 mwaka 2022/2023 hadi watalii 1,863,108 mwaka 2023/2024, hivyo kutokana na  uwepo wa ubora wa miundombinu hususan barabara, Viwanja vya ndege na michezo na kumechochea ongezeko la mapato hapa nchini.

"...Mapato yetu yameongezeka sana sasa hivi tunazungumza mapato ya takribani trilioni 7.5 ambayo tumeyapata kupitia watalii wanaokuja kwenye hifadhi zetu..."
amesema Msigwa.

Aidha, Msigwa amesema Serikali imejipanga kukusanya kiasi cha Tsh. Bil. 430.9 Kupitia TANAPA katika mwaka wa fedha wa 2024/2025 lakini hadi kufikia Juni hadi Disemba zimekusanywa Tsh. bil. 325.1

Katika hatua nyingine, Gerson Msingwa amesema serikali imefanikiwa kutatua migogoro mbalimbali iliyokuwa ikiikumba sekta ya utalii ukiwemo mgogoro wa hifadhi ya Tarangire na kijiji cha Kimotoroki.

Migogoro mingine ni pamoja na ile ya hifadhi ya Serengeti na Vijiji saba vya Wilaya ya Serengeti, hifadhi ya Ruaha na Vijiji vya Mbalali, hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale na Kijiji cha Kalilani huku serikali ikiendelea kuelimisha wananchi kuondokana na migogoro isiyo ya lazima kwenye maeneo ya hifadhi.

Sambamba na hayo, Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kusimamia na kuimarisha  matumizi ya teknolojia katika kushughulikia shughuli za kihifadhi, ukusanyaji wa mapato, utangazaji wa utalii na fursa za nje ya nchi ili kukuza kipato cha Taifa.

16/01/2025

Watu Watatu Wak**atwa kwa tuhuma za Wizi wa Nondo

Watu watatu Wilayani Gairo wamek**atwa kwa tuhuma za kujihusisha na wizi wa nondo 10 zilizotolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Msingi Amali inayojengwa katika Kijiji cha Kwipipa, Kata ya Iyogwe Wilayani Gairo.

Hayo yamebainishwa Januari 15, 2025, na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kilosa, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Ndugu Jabir Makame wakati wa ziara ya k**ati hiyo kwa ajili ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa Wilayani humo.

Akizungumza mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo, Ndugu Jabir Makame amewataja watuhumiwa hao watatu waliok**atwa kuwa ni pamoja na John Mbaluka, Petrol Mauji na Mnyandwa Letema.

Kwa sababu hiyo, Mkuu huyo wa Wilaya ameliagiza Jeshi la Polisi kuwafikisha mahak**ani watuhumiwa hao uchunguzi utakapokamilika na kufanya mahojiano ya kina huku akiliagiza jeshi hilo kuwahoji watunza stoo, mafundi na wote wanaoshukiwa na wizi huo ili kufichua mtandao mzima wa tukio hilo.

Aidha, amewataka wananchi wa Kwipipa na wanagairo kwa jumla kutojihusisha na masuala ya wizi wa vifaa vya miradi ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya Wilaya hiyo kwa sababu vifaa hivyo vinanunuliwa kwa fedha zinazotokana na kodi zao hivyo ni lazima wawe na uchungu na mali hizo na kuwataka hao waliok**atwa kuwa fundisho kwa wengine.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Kwipipa Mhe. Herman Mshomi akiongea kwa njia ya simu na mwandishi wa habari hii, amekiri kutokea wizi huo kijijini kwake na kwamba Bw. Petro Mauji, Mnyandwa Letema na John Mbaluku wanahusishwa na tuhuma za wizi huo wa nondo kumi na kulaani tukio hilo la watu wachache kurudisha nyuma juhudi za serikali za kuwaletea wananchi maendeleo.

Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo wa Kijiji amesema tukio hilo sio la kuikomoa Serikali bali ni kujikomoa wananchi wenyewe kwa sababu miradi hiyo inayoletwa na Serikali haiinufaishi Serikali bali inawanufaisha wananchi wenyewe hivyo wananchi wanapaswa kuwa walinzi namba moja wa miradi hiyo.

"Hii mali iliyokuja japo ni ya Mkoa lakini ni mali ya Kwipipa, kwa vile wanaonufaika ni watu wa Kwipipa tunatakiwa tuitunze hii shule....." amesema Bw. Herman Mshomi.

Bw. Herman sambamba na kuipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kupeleka miradi ya maendeleo katika kijiji hicho ikiwemo ujenzi wa shule hiyo ya Amali, Mshomi ameahidi kuweka mikakati madhubuti ya kulinda miradi ya maendeleo iliyopo Kijijini kwake kwa kushirikiana na wananchi wenzake.

Mwisho.

Hongera kwa kuongeza mwaka mwanafamilia wa Baesa Media
10/01/2025

Hongera kwa kuongeza mwaka mwanafamilia wa Baesa Media

Kampeni ya Mama Samia kuwa mwarobaini wa Migogoro ya wakulima na wafugaji Kilosa. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. D...
15/12/2024

Kampeni ya Mama Samia kuwa mwarobaini wa Migogoro ya wakulima na wafugaji Kilosa.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema Wilaya ya Kilosa imekuwa ikikabiliwa na migogoro mingi ikiwemo ya  wakulima na wafugaji na kwamba imekuwa makao makuu ya migogoro ambayo mwarobaini wake ni Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia - Mama Samia legal Aid Campaign.

Waziri Ndumbaro amebainisha hayo Disemba 15, Mwaka huu wakati akizindua kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia katika kata ya Magomeni Wilayani Kilosa Mkoani humo ikiwa ni siku ya pili baada ya kampeni hiyo kuzinduliwa Kimkoa Disemba 13, 2024.

Akifafanua zaidi, Waziri huyo amesema migogoro inayowakabili wananchi wa Kilosa kumeifanya Wizara ya Uvuvi na Mifugo kuteua Kilosa kuwa makao makuu ya migogoro ya wakulima na wafugaji, hivyo ameitaka timu ya wanasheria wa kampeni hiyo kuandaa ripoti itakayoonesha migogoro iliyotatuliwa na ambayo haijatatuliwa ili  ambayo haijatatuliwa ifanyiwe operesheni maalum ya siku kumi kuhakikisha inaisha.

"...Na mimi niseme sasa baada ya siku hizi kumi itaandaliwa ripoti yenye kuainisha migogoro ipi imekwisha na ipi imesalia ile ambayo imesalia tutakuja na operesheni maalum kumaliza migogoro hiyo..."

Sambamba na hayo, amewataka wananchi wa Mkoa wa Morogoro kujitokeza kwa wingi kwenye kampeni hiyo mara itakapofika katika maeneo yao kwa lengo la kupata usaidizi wa kisheria ili kusuruhisha migogoro yao kwa kufuata misingi ya sheria ili haki ipatikane bila kumuonea mwingine.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amemuomba Waziri wa Katiba na Sheria kuongezewa muda wa kampeni hiyo kwani amesema Wilaya hiyo ni kubwa ambapo Kata 10 na Vijiji 30 pekee vilivyobainishwa kufanyika kampeni hiyo haitakidhi haja ya wananchi wengi wa Wilaya hiyo kufikiwa na Kampeni hiyo.

Amesema, Wilaya hiyo inakabiliwa na migogoro mingi hususan ya wakulima na Wafugaji, migogoro ya kijamii ikiwemo ukatili wa jinsia ya wanawake na watoto, mirathi na ardhi, hivyo kufika kwa msaada huo wa kisheria Kutatatua kero nyingi za kijamii Wilayani na Mkoa kwa ujumla.

Mradi wa TMCHIP kwenda kuboresha afya ya Mama na mtoto. Mradi wa mpango wa uwekezaji wa huduma ya Mama na mtoto (TMCHIP)...
12/12/2024

Mradi wa TMCHIP kwenda kuboresha afya ya Mama na mtoto.

Mradi wa mpango wa uwekezaji wa huduma ya Mama na mtoto (TMCHIP) umelenga  kuboresha afya ya Mama na mtoto pamoja na wananchi wote kwa kuboresha miundombinu yakiwemo majengo, ajira, uboreshaji wa huduma za rufaa na kununua vifaa na vifaa tiba ili kuwa na huduma za uhakika hususan za kundi hilo hapa nchini.

Hayo yamebainishwa Disemba 12, Mwaka huu na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nchi, ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Grace Magembe wakati akifungua mafunzo ya utekelezaji wa mradi wa TMCHIP katika ukumbi wa hoteli ya Cherry iliopo Mkoani Morogoro yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo na kuongeza uelewa wa watendaji na wataalam wa sekta ya afya.

Akifafanua zaidi Naibu katibu huyo, amesema mradi huo unaogharimu zaidi ya Tsh. Bil 16 unalenga kupunguza vifo vya Mama na mtoto ambapo hadi sasa imepunguza kutoka vifo 556 kwa kila vizazi hai 100,000 mpaka 104 kwa kila vizazi hai 100,000  ikiwa ni zaidi ya 80%, hivyo mradi huo una malengo mahsusi ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

"...Mradi huu ambao tunaongelea hapa ni mradi ambao umejikita kuboresha afya ya Mama na mtoto lakini sio afya ya Mama na mtoto pekee bali na afya ya wanannchi wote..." amesema Dkt. Grace Magembe

Aidha, Dkt. Grace amesema mradi huo umepanga kutoa ajira kwa watumishi 1000
ambapo mpaka sasa mradi huo wameajiriwa watumishi 700 na ajira 300 kutangazwa hivi karibuni.

Katika hatua nyingine, Dkt. Magembe amewataka wataalam na wasimamizi hao kusimamia vema miundombinu inayojengwa na mradi huo kwa kutekeleza kwa ufanisi na kuzingatia thamani ya fedha kuendana na ubora wa mradi (Value for money) ili kuwa na miundombinu bora itakayotumika kizazi cha sasa na kijacho.

Sambamba na hayo Dkt. Magembe amewasisitiza kuwa, katika kutekeleza miradi hiyo waepuke uharibifu wa mazingira ili kumuunga Mkono Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kupiga vita uharibifu wa mazingira huku akiwataka Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha maeneo yanayopendekezwa kutekeleza miradi husika yawena hati ili kuepuka migogoro baada ya mradi kuanza kutekelezwa.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi Ya Rais TAMISEMI Dkt. Grace Magembe amepokea Magari sita yaliyotolewa na Amref Health Africa kwa...
12/12/2024

Naibu Katibu Mkuu Ofisi Ya Rais TAMISEMI Dkt. Grace Magembe amepokea Magari sita yaliyotolewa na Amref Health Africa kwaajili ya usimamizi shirikishi wa shughuli za Afya katika Mikoa ya Mara na simiyu.

Magari hayo yamekabidhiwa kwa Mikoa hiyo ikiwa ni awamu ya pili ambapo awali magari mawili yalikabidhiwa Kwa Mkoa wa Simiyu na sasa Amref imetoa Magari manne ambapo matatu yataenda Mkoa wa Mara na moja Simiyu na kufanya jumla ya Magari matatu Kwa Mkoa wa Mara na Simiyu.

ADHA YA MAJI YAISHA MANGAE,  MHE. MKUCHIKA AISHUKURU HALMASHAURI KWA USIMAMIZI BORAWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikuku ...
27/10/2024

ADHA YA MAJI YAISHA MANGAE, MHE. MKUCHIKA AISHUKURU HALMASHAURI KWA USIMAMIZI BORA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikuku (kazi Maalum) Captain Mstaafu Mhe. George Mkuchika (MB) ameishukuru na kuipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro kwa usimamizi na ufuatiliaji mzuri wa fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ili kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

Mhe. Mkuchika amebainisha hayo Oktoba 27, 2024 wakati akizindua mradi wa maji wa Mangae ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro ya kukagua, kutembelea na kuzindua miradi mbalimbali inayotekelezwa ndani ya Mkoa huo.

Mhe. Mkuchika amesema nia ya Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuendelea kutoa fedha na kutekeleza miradi ya maji hapa nchini ili kumtua mama ndoo kichwani na kuwashukuru watendaji wa Halmashauri hiyo kwa usimamizi bora wa fedha na kuweza kutekeleza miradi kwa kiwango cha juu.

"...Naishukuru Halmashauri kwa kusimamia vizuri matumizi ya fedha hizi hamkuruhusu mchwa kula noti za hapa..." amesema Mhe. George Mkuchika.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amemshukuru Mhe. Rais kwa niaba ya wanamorogoro kwa kuwajali na kuwaletea miradi mbalimbali hususan ya maji ambapo hapo awali kipindi cha kiangazi idadi ya mifugo hupungua kwa sababu ya uhaba wa maji ya kutosha ya kunywesha mifugo.

Pia amesema uwekezaji wa ujenzi wa tenki la maji katika kijiji cha Mangae utaondoa kero ya upatikanaji wa maji ambapo amemuomba Mhe. Rais kuendelea kutoa fedha katika Mkoa huo ili kuweza kutokomeza adha ya maji.

Naye, Meneja wa RUWASA wa Wilaya ya Mvomero Mhandisi Mlenge Nasib akisoma taarifa ya mradi huo wa maji wa Kijiji hicho amesema mradi huo umegharimu jumla ya shilingi Milioni 643.7 hadi sasa fedha zilizotumika ni shilingi Milioni 388.8 ambapo mradi huo umefikia asilimia 85% kukamilika ambpo utahudumia wakazi 4049 na kuweza kuondoa changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji katika kijiji cha Mangae.

Tumieni Fursa hii ya kuonana na madaktari bingwa - Dr. NkunguMganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro D...
10/10/2024

Tumieni Fursa hii ya kuonana na madaktari bingwa - Dr. Nkungu

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro Dkt. Daniel Nkungu amewataka wananchi wa Mkoa wa huo kutumia fursa iliyotolewa sasa kujitokeza kwa wingi katika hopsitali hiyo kwa ajili ya kuonana na madaktari bingwa kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI).

Dkt. Nkungu amebainisha hayo Oktoba 10, 2024 wakati akiongea na waandishi wa habari kwa lengo la kutoa taarifa ya uwepo wa madaktari hao bingwa Mkoani Morogoro na hiyo itaanza kutolewa kuanzia Oktoba 15 hadi 19, 2024 katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Morogoro ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Dkt. Nkungu amesema matibabu hayo yataongozwa na madaktari bingwa kutoka MOI wakishirikiana na madaktari bingwa wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na kwamba huduma ya kumuona daktari itatolewa bila malipo
Kwa sababu hiyo amewataka wananchi wa Mkoa wa Morogoro na Mikoa ya jirani kutumia fursa hiyo kufika na kuonana na madaktari hao bingwa ili kupata tiba za kibingwa.

".. niwaombe na kuwashauri wananchi wote wa Mkoa wa Morogoro na Mikoa jirani kutumia fursa hii adhimu kuonana na madaktari bingwa na wabobezi kwa ajili ya kupata matibabu..." amesisitiza Dkt. Daniel Nkungu.

Aidha Dkt. Nkungu amebainisha magonjwa ambayo yatatibiwa kuwa ni ni pamoja na watu wenye matatizo ya mivunjiko ya mifupa, matatizo ya nyonga, magoti, mgongo, kiharusi, ubongo, mishipa ya fahamu, watoto wenye ulemavu na mguu kifundo, kibiongo, mgongo wazi na vichwa vikubwa.

Kambii hii ya madaktari bingwa na wabobezi ni utekelezaji wa agizo la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kusogeza huduma za kibingwa na kibobezi karibu na wananchi.

MWISHO.

RC MOROGORO ATOA WITO, UTUNZAJI WA MAZINGIRA.Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amewataka wadau wa mazing...
04/10/2024

RC MOROGORO ATOA WITO, UTUNZAJI WA MAZINGIRA.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amewataka wadau wa mazingira na misitu hapa nchini kupiga vita vyanzo vya uharibifu wa misitu ikiwemo uchomaji moto na ukataji holela wa miti na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi.

Mhe. Malima amesema hayo Oktoba 3, 2024 wakati wa hafla fupi ya kufunga Jubilei ya miaka 50 ya mafunzo ya misitu hapa nchini iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kilichopo mkoani Morogoro.

Mhe. Kighoma Malima amewataka wataalam wa utafiti wa misitu pamoja na maandiko mbalimbali wahayoandika amesema, bado kuna haja ya wao kwenda kutekeleza kwa vitendo yale waliyoyaandika kwani amesema uharibifu wa mazingira umeendelea kuwa mkubwa jambo ambalo linaongeza mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo ukame, mvua zisizo na uhakika, mafuriko na uharibifu wa mazingira.

" Nitoe wito kwa wadau wa misitu, kuhusu Suala la utunzaji wa Mazingira, tuondokane na tamadumi ya kuchoma misitu hovyo, tunachoma hadi sehemu zenye uoto wa asili, .." amesisitiza Mhe. Adam Malima.

Aidha, amekemea wale wote wanaoendelea kufanya shughulisha za kibinadamu pembezoni mwa mito na vyanzo vya maji k**a kilimo, ufugaji na kufyeka misitu kuacha mara moja tabia hiyo kwani inaongeza uharibifu wa mazingira na akawataka watendaji wa Kata na Tarafa kutoa elimu kwa jamii juu ya utunzaji wa misitu.

Hata hivyo, Mkuu huyo wa Mkoa amemshukuru Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuja na mkakati wa matumizi mbadala wa nishati safi ya kupikia utakaosaidia kudhibiti uharibifu wa mazingira kwa kutokata miti hovyo kwa lengo la kuandaa mashamba na kupata mkaa na matumizi mengine ya kibinadamu.

Katika hatua nyingine, Mhe. Malima ameziagiza Halmshauri za Wilaya za Mkoa wa Morogoro kila moja kuwa na vitalu vya miche ya miti na kutenga ekari 200 kwa ajili ya kupanda miti ili wataalamu kutoka Chuo cha SUA kwenda katika maeneo hayo na kufanya utafiti wa aina ya miti inayostahili kupandwa.

Kamati ya Siasa Morogoro haijaridhishwa na utekelezaji wa mradi wa Barabara ya Mbingu.Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu...
01/10/2024

Kamati ya Siasa Morogoro haijaridhishwa na utekelezaji wa mradi wa Barabara ya Mbingu.

Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Morogoro imesema haijaridhishwa na mwenendo wa ujenzi wa barabara ya Ifakara - Mbingu Wilayani Kilombero uliotakiwa kuanza rasmi kutekelezwa Disemba 8, 2023 lakini hadi sasa bado unasuasua.

Kauli hiyo imetolewa Septemba 29, 2024 na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhandisi Joseph Masunga kwa niaba ya wajumbe wenzake baada ya kutembelea mradi huo ikiwa ni mwendelezo wa ziara yao ya siku tano kukagua utekelezaji wa Ilani ya chama hicho mkoani humo.

"...nieleze masikitiko yangu kutokana na mradi huu kususasua... barabara ndio kero kubwa katika maeneo ya huku..." amesema Mhandisi Joseph Masunga.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa imeelezwa kuwa changamoto kubwa ya mradi huo ni mkandarasi wa ujenzi wa barabara hiyo kutolipwa malipo ya awali (Advance Payment) ambayo kimsingi ni haki yake kwa mujibu wa mkataba huo.

Kwa sababu hiyo, Mhandisi Masunga ameiagiza Serikali ngazi ya Wilaya na Mkoa kufuatilia kwa karibu changamoto hiyo na ili mkandarasi huyo alipwe na kuanza mara moja kwani amesema adha kubwa ya wananchi wa Mlimba ni uwepo wa ubovu wa barabara hususan wakati wa masika.

Hata hivyo, Mhandisi Masunga ameipongeza Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa alioufanya kwenye sekta ya afya ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mlimba na kutumia fursa hiyo kuwapongeza watendaji wote wa serikali ngazi ya Mkoa, Wilaya na ngazi nyingine kwa kusimamia maono ya Rais.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Kighoma Malima, amesema mradi wa Barabara ya Ifakara - Mbingu uko mikononi mwa TANROADS Makao Makuu na Mkoa hivyo ametaka kujipanga zaidi ili kuhakikisha mradi huo unaanza kutekelezwa mapema kwa manufaa ya taifa na usafirishaji wa mazao ya wananchi.

Naye Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro Bw. Geofrey Mtakubwa amesema, mpaka sasa kazi zilizofanyika katika mradi huo ni upimaji, ujenzi wa kambi ya mkandarasi na kuleta vifaa 57 kati ya 137 ambapo ni sawa na 41.6% pamoja na kuleta wataalamu 7 kati ya 9 wanaohitajika.

SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUSOGEZA HUDUMA ZA KIJAMII KWA WANANCHISerikali ya awamu ya sita inayoongozwa  na Dkt. Samia ...
30/09/2024

SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUSOGEZA HUDUMA ZA KIJAMII KWA WANANCHI

Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan imesema imejipanga kuendelea kuwasogezea karibu huduma za kijamii ikiwemo sekta ya Afya wananchi walio maeneo ya pembezoni ili kurahisisha kutofuata huduma hizo kwa umbali mrefu hivyo kuchochea maendeleo yao na ya Taifa kwa ujumla.

Kauli hiyo imebainishwa Septemba 29, 2024 na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro Mhandisi Joseph Masunga wakati wa ziara yake pamoja na wajumbe wa k**ati ya siasa ya Halmashauri kuu ya Mkoa huo kwa lengo la kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya Mkoa huo, na leo ni siku ya tatu wakiwa Wilayani Ulanga.

Mhandisi Masunga amesema, ilani ya CCM inaitaka serikali kuhakikisha inasogeza huduma za kijamii zikiwemo huduma za Afya, Elimu, Maji, miundombinu ya Barabara na umeme na sekta nyingine kwani amesema huduma hizo ndio msingi mkubwa wa maendeleo ya wananchi.

"… serikali inatakiwa kuhakikisha kwamba inapeleka huduma za kijamii karibu zaidi na wananchi na moja ya huduma ya msingi sana ni huduma ya afya…" amesema Mhandisi Joseph Masunga

Akiwa katika mradi wa Daraja la Chigandugandu lililopo Wilayani Ulanga, Mhandisi Joseph amewataka wananchi kulinda miundombinu ya umma likiwemo Daraja hilo huku akiwashauri kupanda miti ama mazao k**a michikichi, mianzi na Migomba pembezoni mwa mto ili kulinda Daraja hilo ambalo hadi kukamilika kwake litagharimu Tsh. Mil. 107.

Mwenyekiti huyo ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi kujiandikisha kkwenye daftari la kudumu la kupiga kura ili kujihakikishia kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliopangwa kufanyika Novemba 27, 2024 kwani, amesema, hiyo ni haki ya kila mtanzania kupiga kura, kuchaguliwa kuwa kiongozi au kuchagua viongozi bora watakaowaletea maendeleo.

Kwa upande wake, Mjumbe wa k**ati ya siasa ya Mkoa huo Bw. Deogratius Mzelu amewapongeza wananchi wa Wilaya ya Ulanga kwa kushirikiana na serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo baada ya wananchi hao kuchangia zaidi ya Tsh. Mil. 12 kwenye ujenzi wa shule ya Sekondari ya Lukande.

M/KITI MASUNGA AIAGIZA RUWASA KUKAMILISHA MRADI WA MAJI WA IGAWA.Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Morogoro Mhan...
29/09/2024

M/KITI MASUNGA AIAGIZA RUWASA KUKAMILISHA MRADI WA MAJI WA IGAWA.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Morogoro Mhandisi Joseph Masunga amewaagiza Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Malinyi kukamilisha ujenzi wa mradi wa maji wa kata ya Igawa ifikapo oktoba 30 mwaka huu.

Mhandisi Masunga ametoa agiza hilo septemba 28, mwaka huu wakati wa ziara ya wajumbe wa k**ati ya siasa ya Mkoa huo kutembelea baadhi ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya Mkoa leo wakiwa Wilayani Malinyi ili kujionea hatua ya miradi ilipofikia na ubora wake.

Akitoa agizo hilo, Mwenyekiti huyo amesema mradi huo wenye thamani ya Tsh. Milioni 855 ulipaswa kukamilika Julai 7, 2022 hivyo, amewataka watendaji wa RUWASA kukamilisha mradi huo haraka ili kutatua kero ya upatikanaji wa maji kwa wakazi 18674 waliopo katika vijiji vitatu vya Igawa, Lugala na Kiwale.

"… unatakiwa ukamilishe mradi kwa wakati k**a ulivyoahidi hapa, wananchi waanze kupata maji katika kata ya Igawa…" amesema Mhandisi Joseph Masunga.

Katika hatua nyingine, Mhandisi Joseph Masunga amewataka wahandisi wa ujenzi wa barabara ya Itete Njiwa hadi Ipera itakayogharimu Tsh. Mil. 266 kukamilisha mradi huo kwa wakati huku akimtaka msimamizi wa mradi huo uliofikia 65% amlipe kwa wakati mkandarasi ili aweze kutekeleza vema mkataba wake na maagizo anayopewa.

Sambambana hayo, Mwenyekiti Masunga ameipongeza serikali ya awamu ya sita ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji thabiti katika sekta ya elimu ukiwemo ujenzi wa shule ya msingi wa Misegese na kuwapongeza wasimamizi wa mradi huo kwa kusimamia maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake, Meneja wa RUWASA Wilaya ya Malinyi Mhandisi Marco Chogero amebainisha kazi zinazoendelea kufanyika ni ujenzi wa fensi eneo la tanki, uchimbaji na ulazaji wa mabomba na ujenzi wa vituo vya kuchota maji huku akiahidi kazi hizo zote kukamilika kabla au ifikapo Oktoba 30, 2024 k**a ilivyoagizwa.

Naye Diwani wa Kata ya Igawa Mhe. Gegalius Kamguna amesema amefurahishwa na ujio wa k**ati ya siasa wilayani humo kwani amesema inaongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia maelekezo yanayotolewa na Kamati hiyo.

MWISHO.

Address

Dodoma

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Baesadigital posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Baesadigital:

Share