31/05/2026
Kutoka kwenye ukurasa wa instagramu wa Mbunge mstaafu wa Nzega Vijijini, Dkt. Hamis Kigwangalla, ameandika maneno haya.
"Siasa ni muhimu sana.
Lakini taifa haliwezi kujengwa kwa siasa peke yake.
Taifa hujengwa na watu wanaolima, wanaozalisha, wanaowekeza, na Siasa ni muhimu sana.
Lakini taifa haliwezi kujengwa kwa siasa peke yake.
Taifa hujengwa na watu wanaolima, wanaozalisha, wanaowekeza, na wanaofungua biashara zinazotengeneza ajira halisi.
Wiki hii nimekuwa Kapunga Rice Project kusimamia mavuno ya mpunga katika moja ya miradi yetu.
Kila ninapokuwa mashambani ninaamini zaidi kuwa Tanzania ina uwezo mkubwa sana wa kuwa taifa tajiri - tukiamua kuwekeza kwa nguvu katika uzalishaji, teknolojia ya kilimo, viwanda vya kuongeza thamani ya mazao yetu, na masoko.
Nchi haiwezi kuwa na uchumi mkubwa ikiwa tunazalisha malighafi pekee bila kujenga biashara na mifumo inayounganisha shamba na chakula mezani.
Ndiyo maana pamoja na kilimo, tunaendelea pia kuwekeza kwenye biashara za chakula na value addition kupitia miradi k**a Kigwangalla’s Farm: Steaks & More. Ndoto ni kuwa na chain ya hizi outlets!
Nimepitia nyakati tofauti katika uongozi wa umma, nimejifunza mengi, ila jambo moja muhimu ni kuwa:
Mijadala ya mitandaoni hupita. Lakini kazi hubaki.
Uchumi wa taifa hujengwa na kazi. Na heshima ya taifa pia hujengwa na kazi.
Tuendelee kujenga.
Kazi iendelee kuongea."