Mesu Kiyuga

Mesu Kiyuga Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Mesu Kiyuga, Digital creator, Dodoma.

*»»Dunia si kamilifu—ina machungu. Lakini kwa wale wanaosafiri kwa moyo wazi, ni shule ya upendo na matumaini.**»»Dunia ...
30/06/2025

*»»Dunia si kamilifu—ina machungu. Lakini kwa wale wanaosafiri kwa moyo wazi, ni shule ya upendo na matumaini.*

*»»Dunia hujaribu kwa magumu, lakini pia hubariki kwa mema. Safari yetu si kuepuka maumivu, bali kuyabadilisha kuwa hekima na shukrani.*

✍️Mesu kiyuga to bariadi, sukuma moja 🙏

PAPA FRANCIS ALILIPA GHARAMA ZA MAZISHI YAKE KABLA YA KIFO CHAKE Vatikani imedokeza kuwa Papa Francis alikuwa tayari ame...
22/04/2025

PAPA FRANCIS ALILIPA GHARAMA ZA MAZISHI YAKE KABLA YA KIFO CHAKE

Vatikani imedokeza kuwa Papa Francis alikuwa tayari ameshailipa gharama za mazishi yake kabla ya kifo chake na aliomba azikwe katika kaburi rahisi na la bei nafuu.

Katika barua aliyoiandika mwezi Juni 2022 ambayo sasa imeachiwa, Papa aliomba kaburi lake liwe rahisi, bila mapambo yoyote na liandikwe neno moja tu: Franciscus.

Papa katika barua hii alisema alitaka azikwe katika Basilika ya Mtakatifu Maria Mkuu huko Roma, kanisa alilolipenda na alilozuru mara kwa mara ili kuomba kabla na baada ya safari zake.

"Kaburi linapaswa kuwa chini ya ardhi, rahisi, bila mapambo maalum, likiwa na maandishi pekee: Franciscus," aliandika Papa.

Vatikani ilisema gharama za mazishi zitafadhiliwa na fedha alizoandaa Papa zipelekwe kwa kanisa kupitia mtu ambaye jina lake halijafichuliwa.

Alipewa maelekezo hayo Kardinali Rolandas Makrickas, ambaye anasimamia basilika hiyo.

Papa pia alishiriki kuwa alikubali uchungu alioupitia katika miaka yake ya mwisho k**a sadaka kwa amani ya dunia na umoja miongoni mwa watu.

"Gharama za maandalizi ya mazishi zitafadhiliwa na kiasi cha fedha kilichotolewa na mfadhili, ambacho nimeshauri akitoe kwa Basilika ya Papa ya Mtakatifu Maria Mkuu," ilisomeka barua hiyo.

"Nimeshauri maelekezo muhimu kuhusu hili kwa Kardinali Rolandas Makrickas, Kamishna Maalum wa Basilika ya Liberia."

Na MESU KIYUGA

NINATOA SALAMU ZA POLE KWA KANISA KATOLIKI, WAKATOLIKI WOTE NCHINI TANZANIA NA ULIMWENGUNI KOTE. MMEPOTEZA KIONGOZI ALIYEJALI UTU, UBINADAMU NA KUMPENDA MUNGU.

Ni nani atakayelipa gharama za mazishi yako?

MAISHA YANA MAJIRA. Na hakuna aliye wa kipekee kutopitia majira yote ya maisha. K**a mwaka ulivyo na majira ya masika, b...
06/04/2025

MAISHA YANA MAJIRA. Na hakuna aliye wa kipekee kutopitia majira yote ya maisha. K**a mwaka ulivyo na majira ya masika, baridi, vuli na kiangazi ndivyo na maisha yetu yalivyo.

Kusudi la majira magumu ama yanayotesa ni kukufua na kumuibua mtu bora aliyeko ndani yako(majira ya mvua na tope ambayo ni kero kwa wasio wakulima ndiyo hupelekea majira ya kuvuna[vuli] na hutupatia chakula). Majira ya furaha na utulivu ni majira ya kujiandaa na nyakati ngumu zijazo, usibweteke.

Unapopitia nyakati ngumu sehemu kubwa ya mapito yako iwe kutaka kufahamu na kuelewa madhaifu yako yaliyokupelekea kuingia mahali pagumu na mambo ya kuzingatia mbeleni ili usiangukie tena magumu. Je, ni kukosa mipaka? Je, ni kutokujali kanuni za afya bora? Je, ni kuchelewa kufanya maamuzi na kuchukua hatua? Je, ni kupotezea ishara/dalili za hatari? Je ni kutojiamini ama ni kujiamini kupitiliza?

Zipo nyakati za furaha na huzuni, utele na kupungukiwa/umaskini, kukataliwa na kukubaliwa, kufukuzwa na kukaribishwa. Vipo pia vipindi vya kuacha na kuachwa, vipo vipindi vya motisha na kukata tamaa, zipo nyakati una nguvu na nyingine dhaifu.

Usibishane na wakati uliopo, bishana na mambo yaliyokuingiza kwenye wakati huo. Kukubaliana na nyakati na zama ulizopo ndiyo moja ya njia ya kupambana na msongo wa mawazo na kuatamia utulivu. Pia humuwezesha mtu kutambaa. Ukijidanganya kuhusu wakati uliopo utatengeneza mipango hewa isiyokuwa na uwezo wa kubadilisha hali yako.

Dhana ya kuyatazama maisha k**a filamu na sio picha mgando huwa inanipa nguvu kipekee ninapokuwa ninapita kwenye nyakati ngumu na zisizofurahisha.

Naye atakuwa k**a mti uliopandwa
Kandokando ya vijito vya maji, [Uzaao matunda yake kwa majira yake] ,
Wala jani lake halinyauki;
Na kila alitendalo litafanikiwa. ~ Zaburi 1:3

Picha ya kesho ya kila mmoja wetu, baada ya kuondoka kwake..Haitochukua muda, nyumbani kwenu kutakuwa hivi..Watu watakuw...
20/03/2025

Picha ya kesho ya kila mmoja wetu, baada ya kuondoka kwake..

Haitochukua muda, nyumbani kwenu kutakuwa hivi..

Watu watakuwa kazini, baada ya kulipwa kuja kupikia waombolezaji..

Picha yako itakuwa kwenye daftari la michango, na mitandao ya kijamii.

Waliokaa nyuma ya wafiwa, ndio wanaosema kweli kuhusu tabia za marehemu..

Story za mpira na tamthilia za Azam, zitaongelewa k**a kawaida..

Watu wakitoka makaburini watakula, na wataongeza kwa ambao hawajashiba..

Kuna rafiki yako wa karibu, siku ya msiba wako atatoa udhuru kuwa hatokuwepo..

Hadithi yako ni fupi sana, ni kuzaliwa kwa uchungu, kuishi kidogo, na kufa..

Tengeneza kesho yako kwa Mungu, Duniani wewe sio special kiasi hicho..

Usijisahau!!..

✍️ Mesu kiyuga

Mwenyezi Mungu aendelee kukupa pumziko la milele kipenzi cha watanzania Dkt hayati JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI rais wa aw...
18/03/2025

Mwenyezi Mungu aendelee kukupa pumziko la milele kipenzi cha watanzania Dkt hayati JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI rais wa awamu ya nne 😭😭🙏

Na sasa utawala wako utakamilika mwaka 2025!
Tutakukumbuka kwa mengi mazuri hakika hatuna cha kukulipa zaidi ya kukuombea kwa mola 🙏❤️

❤️❤️❤️💪💪
11/03/2025

❤️❤️❤️💪💪

Hawa hapa wagombea wetu sisi CHAMA CHA MAPINDUZI - CCM Mgombea Urais mteule na mgombea  Mwenza.      Uchaguzi ni  Octobe...
11/03/2025

Hawa hapa wagombea wetu sisi CHAMA CHA MAPINDUZI - CCM

Mgombea Urais mteule na mgombea Mwenza.

Uchaguzi ni October. Na hii sio k**a Derby ya Simba na Yanga eti no reform no Election

Kwanza fanya reform nyumbani ndio uje kuomba huku reform.

Sisi tuko tayari Kusonga mbele.
Ni mwenyekiti wa chama mwenye historia zake.

Kwanza ni Makamu wa Rais wa Kwanza Tanzania mwanamke.

Mbili ni Rais wa Kwanza Mwanamke Tanzania mwanamke.

Tatu ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wa kwanza Mwanamke.

Hapa

Ziko Nyakati zitakulazimu UPOTEE kidogo kwa MUDA Kabla haujaoonekana tena.Kuna mambo yakitokea kwenye maisha yako, yatak...
09/03/2025

Ziko Nyakati zitakulazimu UPOTEE kidogo kwa MUDA Kabla haujaoonekana tena.

Kuna mambo yakitokea kwenye maisha yako, yatakulazimisha KUPOTEA pale ulipozoea kuonekana...
..isio kwa sababu UMESHINDWA Ila kwa sababu UNAHITAJI kujipanga UPYA.

Ukikutana na AIBU, KUSHINDWA au CHANGAMOTO kubwa inayoendelea KUKUDHOOFISHA...
..usilazimishe kuendelea kuwa HADHARANI, pata muda wa KUJIPANGA.

Kupotea kidogo ni MKAKATI wa kukusaidia KUKUSANYA NGUVU za kupambana au kuinuka UPYA.

Ila pia kunakupunguzia PRESHA za kuzungumzwa na kuulizwa kila wakati.

Kwenye vita kurudi nyuma kujipanga (Retreat) sio KUSHINDWA...
..Ila ni mbinu ya USHINDI.

Kuendelea KUJIONESHA kuwa uko sawa...
..wakati UNAHITAJI muda wa KUPONA na kujipanga UPYA ni KUJIMALIZA.

✍️✍️ Mesu kiyuga
WhatsApp number 0613996610/0672941928

.

IGIZA NA FIKIRI K**A KIONGOZI - H. IBARRAMasomo 10 Kutoka Kwenye Kitabu cha "Igiza K**a Kiongozi, Fikiri K**a Kiongozi"(...
08/02/2025

IGIZA NA FIKIRI K**A KIONGOZI - H. IBARRA

Masomo 10 Kutoka Kwenye Kitabu cha "Igiza K**a Kiongozi, Fikiri K**a Kiongozi"("Act Like a Leader, Think Like a Leader") cha Herminia Ibarra:

1. Pambanua upya kazi yako kwaajili ya kuleta mchango wa kiuongozi (Redefine your job for leadership impact): Jifunze kwenda nje ya majukumu yako ya kila simu na fokasi kwenye majukumu yenye mchango wa kimkakati zaidi kwenye shirika lako na kuuendeleza uwezo wako wa kiuongozi.

2. Tanua na changanya aina za watu kwenye mtandao wako ili kupanua mtizamo wako (Diversify your network to expand your perspective): Fahamiana na watu kutokea kwenye maeneo(taaluma, tasnia na viwanda) mbalimbali na weledi tofauti ili kupata maono mapya na kuupima(challenge) mtizamo ulionao.

3. Jaribisha mitindo mbalimbali ya uongozi (Experiment with different leadership styles): Toka nje ya mazoea yako na jaribu aina/mitindo mipya ya kuongoza, jifunze kutokana na mafanikio na kufeli.

4. Zingatia mtizamo wa nje ili kuelewa mambo kwa kina (Embrace "outsight" for deeper understanding): Nenda zaidi ya unavyofikiri na tafuta mtizamo wa nje ili kupanua uelewa wako wa jambo katika mazingira tofauti.

5. Jenga "utambulisho wa kiuongozi" kupitia simulizi (Develop a "leadership identity" narrative): Tengeneza simulizi juu ya safari yako ya kiuongozi, maadili yako, na malengo yanyoongoza maendeleo yako na kuwahamasisha wengine.

6. Tumia mabadiliko kwaajili ya kukua (Leverage transitions for growth): Yatazame mabadiliko ya kikazi, changamoto, na hata mikwamo k**a fursa za kujipatia maarifa/ujuzi mpya na kubadilika k**a kiongozi.

7. Tawala kujitilia shaka kwa ufanisi (Manage self-doubt effectively): Tambua uwepo wa shaka na uushinde ili kuzuia usiwe kikwazo kwa uwezo wako wa kuongoza.

8. Endeleza uwezo wako wa kisiasa (Develop your "political savvy"): Elewa jinsi madaraka yanavyofanya kazi ndani ya shirika lako na uzitumie kwa busara ili kufikia malengo yako na kuleta mabadiliko chanya.

9. Jenga uwezo wako

Siku moja Profesa alipanda ndege,kwenye siti yake upande wa pili  jirani yake alikuwa ni mkulima.Profesa akawa amefadhai...
06/02/2025

Siku moja Profesa alipanda ndege,kwenye siti yake upande wa pili jirani yake alikuwa ni mkulima.

Profesa akawa amefadhaika akahitajika kucheza mchezo na mkulima.

Profesa akamwambia tucheze mchezo wa kuulizana maswali pamoja,ukishinda nakupa dola $500 na ukishindwa unanipatia dola $5

Mchezo ukaanza wa kuulizana maswali, Professa akamuuliza mkulima Je kuna umbali gani kutoka uso wa dunia mpaka Kulifikia jua?

Mkulima aliona swali halijui akampatia Proffesa dola $5,ikawa zamu ya mkulima kuuliza swali

Mkulima akamuuliza Proffesa,Ni ndege gani akikwea mlimani ana miguu mitatu na akishuka ana miguu miwili?
Proffesa alifikiri na kutafakari mpaka akajaribu kuandika kwenye Kitabu cha kumbukumbu lakini hakupata jibu, Akatoa dolla $500 akampatia mkulima.

Proffesa akauliza ni ndege gani huyo? Uliyekuwa unamzungumzia ? Mkulima akatoa dolla $ 5 akampatia wakawa wamefika wakashuka kila mmoja aliendelea na safari yake.

Hiki kisa kinatufundisha nini marafiki tafakari halafu niandikie maoni hapa chini.

Usisahau kumfollow
Mesu kiyuga 👇🤳

Whatsapp group 0613996610

Kuna Dem Nilikutana nae saa 3 usiku nikaomba namba akanipa , Saa 4 akaniambia ana shida na elfu 5  , nikamwambia sawa ni...
28/01/2025

Kuna Dem Nilikutana nae saa 3 usiku nikaomba namba akanipa , Saa 4 akaniambia ana shida na elfu 5 , nikamwambia sawa nitakupa , Akaniuliza unakaa wapi nikamwambia hapo mtaa wa pili , kisha akaniambia nitakuja kukutembelea Saa 5 usiku akaja geto , saa 6 akaja nikamwambia sina pesakweye simu wala cash mpaka kesho nikatoe ITM akasema ok by saa 8 usiku hivi nikamsindikiza akaenda home

Saa 1 asubuhi akanichek nikawa bado nimelala , saa 2 asubuhi akanichek nikawa bado nimelala , kuamka saa 3 nikakutana na meseji zake , nikamwambia sorry nilikuwa bado nimelala akaniambia nilikwambia lakini nina shida na 5k ?

nikamwambia ndo naamka halafu ndo nataka nifue kisha niende ITM , BAADA YA HAPOB akaniambia naomba basi hata buku tu nikale "NAOMBA BASI HATA BUKU TU NIKALE'

"NAOMBA BASI HATA BUKU TU NIKALE" Hili neno liliniuma sana pale pale ilibidi nikae nikatoa machozi sana , Kisha nikamuuliza uko wapi ? akniambia yupo home na mimi nimaamka kweli nikafanya mpango nikamtumia 30K

Nilichojifunza

1. Muda mwingine Dada zetu tutawapa kila aina ya majina , malaya , Kimada , changudoa lakini behind siyo kila mwanamke ni malaya kuna situation wanazopitia ni ngumu mno

2. Unapokutana na mwanamke jitahidi kumpa chakula kwanza kisha mambo yenu mengine yatafuata k**a amekutembelea lakini au mnunulie chakula ale kwanza

3. Tusiwahukumu wanawake wanaojiuza tujitahidi kufuatilia background ya maisha yao asilimia kubwa hakuna dada anayeamua kufanya hivyo kwa kupenda

4. Ikiwa umemuahidi mtu pesa jitahidi kumtumia ile pesa muda uliomuahidi , pengine amesubirisha familia haijapata chochote kitu kisa wewe tu pesa unayo na kuituma unachelewa , watu wanapitia magumu mno

5. Sema ukweli huna huna mtu ajue huna usiwafanye watu wakaishi kwa matarajio ambayo kimsingi huwezi kuwasaidia , Ukweli mchungu ni mzuri kuliko Uwongo usiokuwa na faida

Usimnyanyase aliyeko chini leo, kwa sababu kesho anaweza kuwa juu na ukamuhitaji. Maisha yana mafumbo sana.Kwenye kitabu...
24/01/2025

Usimnyanyase aliyeko chini leo, kwa sababu kesho anaweza kuwa juu na ukamuhitaji. Maisha yana mafumbo sana.

Kwenye kitabu cha historia ya maisha yake (Mzee Rhuksha), hayati Mzee Mwinyi alielezea kisa chenye mafunzo makubwa.

Mara baada ya kujiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani, waziri mpya aliyeteuliwa kuchukua nafasi yake alimtaka Mzee Mwinyi ahame mara moja kwenye nyumba ya serikai aliyokuwa anakaa.

Mzee Mwinyi alifanikiwa kuhama kwa fedheha na aliacha baadhi ya vifaa vyake vya ujezi wa nyumba yake. Yule waziri alimdhulumu vile vifaa vyake.

Miaka michache baadaye, Mzee Mwinyi alikuja kuwa Rais wa na akamteua yule waziri aliyemnyanyasa kuwa mmoja wa mawaziri wake. Bila shaka, ilikuwa ni kutoa mafunzo.

Leo k**a una nafasi, cheo, nguvu au mali; Usinyanyase wengine. Mungu anaweza kuwainua na wakawa juu yako kesho.

Jifunze kuwathamini watu hata k**a umewazidi kila kitu, usije ukapata aibu siku ambapo Mungu atawainua zaidi yako.

🪛🪛🪛🪛 Mesu kiyuga Instagram, X, Facebook, you tube

WhatsApp 0613996610

Address

Dodoma

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mesu Kiyuga posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share