14/06/2025
Spika wa Bunge la Minnesota, Emerita Melissa Hortman na mumewe, Mark, wamepigwq risasi na kuuawa leo Jumamosi asubuhi nyumbani kwao huko Brooklyn Park.
Shambulio hilo kali limetikisa Minnesota huku mtu aliyejifanya kuwa Afisa wa Polisi alifanya shambulio hilo la risasi lililolenga nyumba za Wabunge wawili wa Chama cha Democratic.
Karibu saa mbili asubuhi, mtu mwenye bunduki alifyatua risasi katika nyumba ya Champlin ya Seneta wa Jimbo John Hoffman, ambapo mwanamume na mwanamke walipigwa risasi.
Muda mfupi baadaye, nyumba ya mwakilishi Melissa Hortman huko Brooklyn Park pia ilishambuliwa.
Takribani watu watatu wamepigwa risasi, na mshukiwa bado hajak**atwa.
Mamlaka zinachukulia mashambulizi hayo k**a yamechochewa kisiasa, na msako wa Jimbo zima unaendelea.