11/09/2026
Mbunge wa Jimbo la Mwera Zanzibar na Mwenyekiti wa Mwera Development Foundation Mhe. Suleiman Mohamed Rashid, amekutana na viongozi wa kambi za wanafunzi kutoka shule sita na kutoa jumla ya Shilingi milioni sita, sawa na Shilingi milioni moja kwa kila shule, kwa ajili ya kusaidia shughuli za kambi hizo za maandalizi ya mitihani.
Kambi hizo zinahusisha wanafunzi wa Kidato cha Nne, Kidato cha Pili na Darasa la Saba, huku shule zilizonufaika zikiwa ni Skuli za Msingi Mtoni Kidatu, Kianga na Regeza Mwendo, pamoja na Skuli za Sekondari Mtoni Kidatu, Kianga na Regeza Mwendo.
Akizungumza wakati wa kukutana na viongozi wa kambi hizo, Mhe. Suleiman amesema mpango huo unalenga kuongeza motisha kwa wanafunzi, kukuza ufaulu na kuboresha mazingira ya kujifunzia ili kuwawezesha kufanya vizuri katika mitihani yao.
βLengo ni kuongeza motisha na kukuza ufaulu kwa wanafunzi, pamoja na kuboresha mazingira yao ya kujifunzia,β alisema Mhe. Suleiman.
Amesema uamuzi huo umetokana na kutambua kuwa bado kuna changamoto katika kiwango cha ufaulu, hivyo kuna umuhimu wa kuanza kuwekeza mapema katika elimu, hususan katika mazingira ya kujifunzia na maandalizi ya wanafunzi.
βTunajua hali ya ufaulu si nzuri, kwa hiyo tumeamua kufanya hivi ili tupate wanafunzi wenye ufaulu mzuri na pia kuwabaini wale wenye vipaji maalum,β alisema.
Mhe. Suleiman amesema mpango huo haujalenga tu kuongeza ufaulu, bali pia kutoa fursa ya kuwabaini wanafunzi wenye uwezo na vipaji mbalimbali ambao wanaweza kusaidiwa na kuendelezwa zaidi.
Amesema awali aliwahi kukutana na wanafunzi wa Kidato cha Nne waliofanya vizuri katika mitihani na kuwapatia zawadi, jambo lililomfanya kutafakari umuhimu wa kuwekeza katika ufaulu kabla ya matokeo badala ya kusubiri wanafunzi wafanye vizuri ndipo wapewe motisha.
βNiliwahi kukutana na wanafunzi wa Kidato cha Nne ambao walifaulu vizuri na kuwapa zawadi, lakini nikasema tuanze kwenye ufaulu. Tuanze kuboresha mazingira yao ya kujifunzia kuanzia mwanzo,β alisema.
Kwa mujibu wa Mhe. Suleiman, hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za kuweka mazingira yatakayowasaidia wanafunzi kuongeza ari ya kusoma, kujiandaa viz