Central Press Club

Central Press Club Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Central Press Club, Media, Street address:, Regional Commissioner's Office building Block 12 Room No:11, Nyerere Road (old kuu street road), Dodoma.

27/04/2016

HAYA NI BAADHI YA YALIYOJIRI LEO BUNGENI DODOMA - 27 APRIL,2016
NAIBU spika wa bunge dr TULIA AKSON amesema ipo haja ya kurekebisha Sheria zilizopo itakayowezesha mbunge kulipwa posho baada ya kutekeleza majukumu yake ipasavyo na siyo kuandika kuhudhuria katika mkutano au vikao pekee.
Kauli hiyo ya dr TULIA ameito wakati akijibu muongozo uliotolewa na mbunge wa Nzega mjini HUSSEIN BASHE.
Katika muongozo wake BASHE ametumia Kanuni ya 68 kifungu kidogo cha 7 ya Kanuni za Kudumu za Bunge kufuatia Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuamua kutoshiriki mjadala lakini Wabunge wa Kambi hiyo wanasaini na kulipwa mshahara na kuhoji endapo ni haki na ni sahihi kwa Wabunge hao kupokea posho wakati hawashiriki na kutimiza wajibu wao wa kikatiba na kisheria.
Dr TULIA amesema Michango ya Wabunge ni muhimu kwa kuwa kupitia michango yao Wabunge wanatoa usimamizi mzuri wa shughuli za Serikali ambazo ni muhimu sana katika kuwaletea wananchi maendeleo hivyo ili kukabiliana na hali ya namna hiyo inapaswa kuweka utaratibu mahsusi.
Amesema malipo ya posho kwa wabunge yanatokana na mahudhurio yao Bungeni na siyo Kuchangia lakini Kimsingi kuhudhuria Bungeni pekee si njia inayopendeza kwa kuwa Mbunge anapofika Bungeni anatarajiwa atekeleze majukumu yake ya kikatiba k**a yalivyoainishwa katika Ibara ya 63 na kusisitiza kuwa tabia hiyo haikubaliki na haistahili kuendelea.
Amewataka Wabunge wote kuwa Wazalendo kwa Nchi yao na kushiriki kikamilifu katika kuchangia Bajeti iliyopo mbele yao na kwamba tabia ya kuhudhuria Bungeni Kwa ajili ya kulipwa posho bila ya kuitolea jasho inabidi iachwe mara moja.
Wiki iliyopita wakati bajeti ya Ofisi ya waziri mkuu inawasilisha hotuba yake kambi ya upinzani bungeni ilisusia kutoa hotuba yao na kuchangia kwa madai kuwa katiba imekiukwa.
***************************************
TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imepokea na kuchunguza jumla ya malalamiko 13,709 katika kipindi cha kuanzia mwaka 2010 hadi 2016.
Hayo yameelezwa bungeni na waziri wa Katiba na Sheria dr HARRISON MWAKYEMBE wakati akijibu swali la mbunge wa Mtambile MASOUD ABDALLAH SALIM.
Katika swali lake mbunge huyo ametaka kujua ni kwa kiasi gani Tume imefanikiwa kutekeleza jukumu hilo kwa kipindi cha mwaka 2010-2016.
Dr MWAKYEMBE amesema kati ya malalamiko hayo yaliyopokelewa malalamiko 6169 yalihitimishwa na malalamiko 7540 yanaendelea kuchunguzwa.
Ameainisha malalamiko hayo kuwa ni migogoro ya ardhi ya wakulima na wawekezaji,wakulima na wafugaji,wananchi na maeneo ya hifadhi,matumizi mabaya ya madaraka kwa watendaji,ukatili dhidi ya wanawake na watoto,ucheleweshaji wa haki kwa mahabusu na wafungwa na matumizi ya nguvu kwa vyombo vya dola.
Dr MWAKYEMBE amesema pamoja na taarifa hiyo, Tume ilifanya tafiti kuhusu haki za watoto,ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi,kutoa elimu kwa umma kuhusu haki za binadamu na misingi ya utawala bora,kutembelea magereza na kufanya uchuguzi wa matukio ya uvunjwaji wa haki za binadamu.
**************************************

SERIKALI imesema katika kipindi cha mwaka 2010 mpaka 2015 hakuna ng'ombe waliotaifishwa na serikali katika wilaya ya Ushetu.
Naibu waziri wa maliasili na utalii injinia RAMO MAKANI amesema hayo jana bungeni wakati akijibu swali la mbunge wa Ushetu ELIAS KWANDIKWA aliyetaka kujua ni ng'ombe wangapi wametaifishwa na serikali kwa kuingia katika hifadhi ya Kigosi eneo linalopakana na jimbo la Ushetu.
Aidha ametaka kujua pia utaratibu unaotumika kuua ng'ombe wanaoingia kwenye hifadhi na ni ng'ombe wangapi waliuawa katika kipindi cha mwaka 2010-2015.
Akijibu maswali hayo Injinia MAKANI amesema serikali imebaini kuwa watu wanaopeleka mifugo ndani ya mapori ya Kigosi Mayowosi ni pamoja na wageni toka nchi jirani ambao wanaingia hifadhini na silaha za kivita.
Katika jitihada za kuwatoa wafugaji wa aina hii katika hifadhi maafa yametokea hapa na pale ambapo askari kadhaa wa wanyamapori wamepoteza maisha,mifugo kadhaa wakiuawa katika mazingira ya aina hiyo.
Hata hivyo amesema serikali hainasera,sheria,kanuni au utaratibu wa kuua mifugo.
***************************************

SERIKALI imewaagiza wafanyabiashara wa sukari nchini kutoa sukari waliyonayo ili iendelee kuuzwa kwa bei elekezi na kuondokana na upungufu wa sukari unaodaiwa kuwepo nchini.
Aidha imewaagiza maafisa biashara kwenye halmashauri na wilaya zote nchini kufanya ufuatiliaji kwenye maduka yote ili kujihakikishia kuwa sukari haifichwi ili ije iuzwe kwa bei ya juu badala ya bei elekezi ambayo imetolewa na serikali.
Akihitimisha hoja ya bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya waziri mkuu kwa mwaka 2016/2017 Waziri mkuu mheshimiwa KASSIM MAJALIWA amesema kwa sasa wameshaweka malengo ya uzalishaji wa ndani ya nchi ili kuweza kufikia mahitaji ya kitaifa na kuwasihi wananchi kuwa sukari itaingia baada ya muda mfupi.
Amesema takwimu zinaonyesha kuwa sukari iliyopo nchini ni tani zisizozidi 37 ambazo wanaamini zikiendelea kuuzwa zitazuia upungufu wakati wanaendelea kusubiri sukari nyingine.

Katika hatua nyingine serikali imesisitiza dhamira yake ya kutotoa vibali vya kuagiza mchele kutoka nje ya nchi ili kusaidia wakulima kupata soko la uhakika na bei nzuri jambo ambalo linawaongezea kipato na pia kuwahamasisha kuongeza uzalishaji zaidi.
Kutokana na hilo Mheshimiwa MAJALIWA ameviagiza vyombo vya dola kuendelea kuimarisha ulinzi wa mipaka hasa katika mwambao wa Bahari ya Hindi ili kuzuia uingizwaji holela wa mchele wa magendo kutoka nje ya Nchi na kwamba endapo patatokea upungufu wa mchele nchini Serikali itaangalia uwezekano wa kuruhusu na kuingiza mchele kutoka nje.
Ameitaka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kuhamasisha uwekezaji katika teknolojia ya Ukoboaji mpunga na Wizara ya Fedha na Mipango kuendelea kulinda soko la mchele la ndani kwa kuhakikisha kiwango cha wigo wa pamoja wa Ushuru wa Forodha kwa Afrika Mashariki hakishushwi.

Bunge limepitisha bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya waziri mkuu kwa mwaka 2016/2017.
***************************************

25/04/2016

Vision

Central Press Club envisions a strong and well informed civil society; where people actively participate in decision-making process to ensure transparency and accountability of the state and the people in an interdependent world; where human rights, good governance, cultural diversity, gender equality and peace, respect, justice, sustainable human security and sustainable development are accepted and enjoyed by all citizens regardless of s*x, age, religion, race, education status and ranks.

MISSION

As one of activist media organisation, Central Press Club is committed to strengthen citizenship, accountability, good governance and human development through capacity building linkages including advocacy, and lobbying, networking and awareness creation by using available resources in particular media channels towards influencing decision making processes at all levels.

Address

Street Address:, Regional Commissioner's Office Building Block 12 Room No:11, Nyerere Road (old Kuu Street Road)
Dodoma
P.O.BOX1816,DODOMA,EASTAFRICA

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Central Press Club posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Central Press Club:

Share

Category