Maarifa Katika Jamii

Maarifa Katika Jamii Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Maarifa Katika Jamii, Publisher, Mipango, Dodoma.

13/10/2023

MAISHA BILA KUWA NA NATUMAINI NI HATARI MNO.

Matumaini Kwenye maisha ni muhimu Sana, inakutaka wewe uwe na tumaini ndani yako hata K**a mazingira hayaruhusu wewe Kuwa na tumaini

Hata ukiwa ndani ya giza nene namna gani bado unapaswa kuwa na tumaini la kuona mwanga

Hata ukiwa uko peke yako kiasi gani bado unatakiwa Kuwa na tumaini la kutoboa

Hata k**a unaona mwelekeo wa mahusiano yako umekuwa ndivyo sivyo, bado unatakiwa Kuwa na matumaini ndani yako ya kwamba lazima yaende kwenye mwelekeo unaotakiwa

Hata watu wakikudhihaki, wakakucheka, wakakuona huna MALENGO, unapoteza muda wako bure hapo ulipo, bado unatakiwa Kuwa na matumaini ya kutoboa

Hata K**a unapanga mipango na inafeli, unafanya mambo Fulani na yanakufa au hayafiki kule unataka bado unatakiwa Kuwa na matumaini ya kutoboa

KWANINI NAKWAMBIA UWE NA MATUMAINI? NDANI YA MATUMAINI KUNA VITU HUZALISHWA NAVYO NI...

1. Tumaini likiwa ndani yako hata uwezo wa kufikiri Huwa mzuri,

2. Tumaini huzalisha kujiamini, kwahiyo Ukiwa na tumaini hata uwezo wa kujiamini huongezeka

3. Tumaini hutengeneza mlango wa kutoka hasa pale mtu unapokuwa na imani ya kwamba Kuna muda atavuka pale alipo

4. Tumaini humtia nguvu mtu hata K**a bado anajiona mnyonge, unyonge wake utafunikwa na tumaini ambalo hugeuka Kuwa nguvu ndani ya moyo wake

5. Tumaini humfanya mtu awe chanya kwenye maisha yake

6. Tumaini humfanya mtu awe na msimamo mzuri

Kuwa na matumaini kwenye maisha yako, Mtumaini Mungu wako hata k**a Mambo Ni magumu sana wewe ndani yako usipoteze tumaini.

KWA AJILI YA KUPIGA VITA UMASIKINI NA Njaa TUMIA SUPER GRO*_SUPER GRO_Ni kichocheo  cha afya ya mimea ya aina yote.  Bid...
20/06/2023

KWA AJILI YA KUPIGA VITA UMASIKINI NA Njaa TUMIA SUPER GRO*

_SUPER GRO_

Ni kichocheo  cha afya ya mimea ya aina yote.  Bidhaa hii sasa ni maarufu duniani na huku Africa Mashariki kwani imeweza kuwasaidia wakulima kuongeza mazao na kupunguza gharama za kilimo hasa madawa na mbolea.

📶SUPER GRO IMEWEZA KUJIBU CHANGAMOTO ZA WAKULIMA MFANO

1⃣Uhaba wa mvua

2⃣Mazao hafifu

3⃣Udongo uloishiwa rutuba

4⃣Wadudu na Magonjwa

5⃣Gharama kubwa za pembejeo

6⃣Masoko ya mazao yao

👆Changamoto hizo za wa kulima zinajibiwa na 👉Super Gro tu.

Ili kupata wasiliana nami kwa nambari 0789665149

29/03/2023

Uaminifu ni sura ya kwanza ya kitabu cha hekima. Ukikosa uaminifu utaishi maisha ya kitapeli, janjajanja, uongo, wizi na ulaghai ndio maana Yesu akatuasa tuwe waaminifu hata kwa mambo madogo! Fid Q anasema usimuamini muongo hata k**a anasema ukweli. Unapewa kazi ya kukusanya michango ya harusi unataka uk**alizie nyumba yako, huo ni utapeli. Ndio maana watu wengi siku hizi hawachangii harusi na mimi nikiwemo. Fikiria watu 100 mnachangia laki laki, halafu siku ya harusi watu kumi mnakula kuku mmoja wa buku ten na bia za promotion, ukiomba juice unaaambiwa imeisha. Unabaki kujiuliza pesa imekwenda wapi? Bora basi hata maharusi wangepewa zawadi nono, unakuta wamepewa mahotpoti na vitenge. Kumbuka hapo familia ilitoa kianzio cha milioni mbili siku ya kuzindua k**ati! Kweli usimuamini mtu mpaka apate hela!

10/01/2023

Huwezi kurudi nyuma na kubadili mwanzo mbaya lakini unaweza kuanzia hapo ulipo kubadilisha mwisho mbaya! Usiruhusu jana itawale sana leo yako. Usibebe jana mbaya kwenda nayo kesho.Najua umefeli katika mengi. Ngoja nikwambie. Kufeli siyo kinyume cha kufanikiwa, kufeli ni mafanikio yenyewe. Waliofanikiwa sana ni wale waliofeli mara nyingi. Yaliyotokea kubali tu yameishatokea. Ukitazama hapo ulipo ona kuwa kuna jambo unaloweza kufanya kuboresha kesho yako. Ukitazama mbele unakokwenda kuwa na imani kwamba utafika. Ukiwa na imani hata ndogo k**a mbegu ya haradali, utaweza kuhamisha milima alisema Bw. Yesu. Imani ni bora kuliko dini. Kuchanika kwa jamvi sio mwisho wa maongezi. Mnaweza hata kusimama na stori zikaendelea. Njia pekee ya kuwa mtu unayetaka kuwa ni kujitahidi kuwa bora kuliko jana. Kila siku inapobadilika ina maana yake, baraka zake na kumbukumbu zake muhimu. Ipe maana njema kesho yako ili ufanikiwe kirahisi!

MFAHAMU KWAME NKRUMAHAlizaliwa mwaka 1909 mjini Nkrorful Ghana wakati huo ikiitwa Gold Coast. Hakuna aliyekuwa na elimu ...
01/02/2022

MFAHAMU KWAME NKRUMAH

Alizaliwa mwaka 1909 mjini Nkrorful Ghana wakati huo ikiitwa Gold Coast. Hakuna aliyekuwa na elimu katika familia yake enzi hizo. Kwame ni jina wanalopewa watoto wa kiume wanaozaliwa Jumamosi katika mila za Ghana.

Baada ya elimu yake ya awali nchini Ghana mwaka 1935 Nkurumah alisafiri kwenda Pennsylvania USA ambako alisoma Batchelor of Arts, Batchelor of Theology na Masters of Science.

Mwaka 1945 alijiunga na London School of Economics kufanya PhD ya Anthropology

===================================

HUYU NDIYO KWAME NKRUMAH JABALI LA UKOMBOZI WA AFRIKA.

Kwa mamilioni ya watu ndani na nje ya Afrika, Kwame Nkrumah ndiye Afrika na Afrika ndiyo Kwame Nkrumah; Kwa Wakoloni na Mabeberu jina la Nkrumah ni laana kwao; kwa Masetla na Walowezi jina lake ni onyo kwamba siku zao zinahesabika; kwa Waafrika wanaokandamizwa kwa ukoloni na ubeberu wa kimataifa, jina lake ni pumzi ya matumaini, nyenzo ya uhuru, ushindi, udugu na usawa kwa wote”.
Ndivyo yalivyosomeka maneno ya bango moja mjini Accra, Ghana miaka ya 1960 wakati wa kilele cha harakati za Uhuru barani Afrika. Ghana ilipata uhuru Machi 6, 1957 chini ya Dakta Kwame Nkrumah k**a Rais wa kwanza.

Lakini Nkrumah hakuridhika na uhuru wa nchi yake pekee, alisema: “Uhuru wa Ghana hautakuwa na maana k**a nchi zingine za Kiafrika zitaendelea kuwa chini ya Utawala wa Kikoloni”, kuonesha jinsi mwanaharakati huyu alivyokuwa tayari kujitoa mhanga kwa ukombozi wa Bara zima la Afrika.
Mwaka mmoja tu baada ya uhuru wa Ghana, Nkrumah aliitisha Mkutano wa mataifa yote ya Afrika (All African People’s Conference) mjini Accra, Desemba 1958, kuzungumzia agenda ya harakati za uhuru, namna ya kulinda uhuru unaopatikana na kuendeleza mapinduzi ya Kiafrika. Kati ya waliohudhuria, baadhi yao ndio hao waliokuja kuwa viongozi wa nchi zao kufuatia uhuru.

Hao ni pamoja na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Tanganyika); Dakta Hastings Kamuzu Banda (Nyazaland, baadaye kuitwa Malawi); Joshua Nkomo (Southern Rhodesia/Zimbabwe), Dakta Keneth Kaunda (Northern Rhodesia/Zambia) na Patrice Emery Lumumba (Congo Leopoldville/Zaire/DRC).
Wengine walikuwa ni Amilcar Cabral (Portuguese Guinea/Guinea Bissau); Holden Robert (Angola) na Tom Mboya (Kenya) aliyewakilisha Vyama vya Wafanyakazi na ambaye pia alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Mkutano huo.

Walihudhuria pia kwa “Mwaliko maalum”, wanaharakati kutoka Zanzibar: Abeid Amani Karume (Afro-Shirazi Party – ASP) na Ali Muhsin (Zanzibar Nationalist Party – ZNP). ASP na ZNP vilikuwa na ugomvi na uhasama mkubwa wa kisera na kimaono kiwango cha kuzuia meli ya uhuru kuong’oa nanga Visiwani.

Wakati ZNP kilichokuwa cha mrengo wa siasa za Kikomunisti na kiharakati zaidi (kwa msukumo wa Abdulrahman Babu k**a Katibu Mkuu) kilitaka uhuru mara moja; ASP chenye siasa za kati chini ya Karume kilitaka agenda ya uhuru iahirishwe kwa muda (kauli yake ilikuwa “Uhuru Zuia”) kikihofia ZNP kuchukua nchi.

Karume na Muhsin walipatanishwa na Nkrumah mwenyewe pamoja na Msaidizi wake George Padmore. Wawili hao wakaonywa kuepuka kuwa “Vita vya panzi” enzi hizo za harakati za uhuru. Mapatano hayo, yaliyopewa jina “The Accra Accord” kwa lengo la kuimarisha Umoja wa Kitaifa, ulikuwa “Mwafaka” wa kwanza kwa Siasa za mpasuko Zanzibar, japo haukudumu, ambapo leo uhasama huu umerithiwa na “CCM Zanzibar” na “CUF Zanbar” kwa misingi ile ile ya kale.

Nkrumah alikuwa Mwasisi wa wazo la kuundwa kwa Shirikisho la nchi za Afrika, wazo lililozaa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU, sasa AU). Lengo lilikuwa ni kuona Afrika inajizatiti katika kujenga uchumi huru na imara; kujitegemea na kuunda Jeshi kubwa, imara kuweza kukabiliana na uvamizi kutoka nje na ambalo lingetumika pia kwa harakati za ukombozi wa Afrika.

Ni kwa njia ipi na muundo upi Shirikisho la Afrika lingefikiwa, Nkrumah na Nyerere, majabali wawili wa Siasa za Afrika enzi hizo, walitofautiana. Wakati Nkrumah alitaka Afrika iungane mara moja bila kuchelewa kabla viongozi hawajaanza kunogewa na kulewa madaraka, Nyerere alitaka Muungano wa Afrika uanze kwa awamu na kikanda, kwa nchi chache kuungana kabla ya kufikia Muungano wa Afrika nzima.

Kwenye Mkutano wa Pili wa OAU mjini Cairo, Julai 1964, Nyerere na Nkrumah walishambuliana kwa maneno na ukinzani wa hoja nusura washikane mashati juu ya hilo, ugomvi uliopewa jina “The Great Encounter” (Pambano Kuu) ambapo hoja ya Nyerere ilishinda.

Afrika na Dunia nzima bado inajiuliza, ni yupi kati ya wawili hao alikuwa sahihi juu ya kufikia Shirikisho/Umoja wa Afrika, hasa tunaposhudia kwamba hadi leo, Afrika imeshindwa kuungana, huku miungano/jumuiya za Kikanda zikiibuka na kuvunjika haraka na kirahisi? Ni nani huyu, Mwanaharakati Kwame Nkrumah, mwenye kustahili kuitwa “Baba wa Uhuru” barani Afrika; jabali la siasa aliyeweza kusuguana mabega na Mwalimu Nyerere?

Chama cha kwanza cha kiharakati nchini Ghana kilianzishwa mwaka 1947, kikiitwa “The United Gold Coast Convention” (UGCC) chini ya Dakta Joseph Danquah, kilichoanza na hoja ya kubadili jina la nchi kutoka “Gold Coast” kuwa “Ghana” kabla hata ya uhuru. Kilimwajiri Dakta Nkrumah k**a Katibu Mkuu ili kukipa nguvu, kwa kumwita kutoka Marekani na Uingereza alikoishi kwa miaka 12 na kujipatia shahada za juu katika uchumi, Sosholojia na falsafa.

Akiwa ng’ambo, Nkrumah alijikita katika kuwaunganisha watu weusi ugenini wajitambue na watambue haki zao na kusaidia uhuru wa Afrika. Ni Nkrumah na Weusi wengine wa nchi za Kikarebia, aliyeitisha Mkutano mkuu wa Kwanza wa watu Weusi duniani (Pan-Africanism Conference) mjini Manchester, mwaka 1945 kuzungumzia Mshik**ano wa mtu mweusi.

Mwaka 1949, Nkrumah na Danquah walifarakana; Nkrumah akajiengua UGCC na kuanzisha Chama cha siasa za mrengo wa Ki-Karl Marx (Kikomunisti) cha ”Convention People’s Party” (CPP). Mwaka 1951, alish*takiwa na kufungwa miezi sita kwa makosa ya “uchochezi”, akaendelea kupigania uhuru akiwa kifungoni.

Katika uchaguzi wa kwanza mwaka huo, ambapo aligombea akiwa jela, chama chake CPP, kilipata viti 34 kati ya viti 38 vya Baraza la Kutunga Sheria (LEGCO) na GCP cha Danquah kiliambulia viti vinne. Nkrumah mwenyewe katika Jimbo la Accra alipata kura 20,780 kati ya kura 23,122 zilizopigwa; mpinzani wake kutoka GCP alipata kura 2,342.

Habari za ushindi huo zilimfikia Nkrumah akiwa jela Februari 12, 1951; naye Gavana wa nchi hiyo, Aden Clarke, akalazimika kumtoa kifungoni siku hiyo na kumwomba aunde Serikali ya Mpito.
Julai 1953, huku akionesha dhahiri kupoteza subira, Nkrumah alishinikiza kuundwa kwa Serikali yenye madaraka kamili “bila kuchelewa”. Hata hivyo, ulizuka mtafaruku kati ya Nkrumah aliyetaka kujenga Taifa huru la kidemokrasia na la kisiasa, na Watawala wa kijadi (Machifu) waliotaka kubakia na madaraka yao ya wakati wa ukoloni; ghasia na machafuko yakazuka na nyumba ya Nkrumah ikashambuliwa kwa mabomu. Kwa kisingizio cha kutaka kupata matakwa sahihi ya wananchi, Serikali iliagiza ufanyike uchaguzi mwingine.

Licha ya ushindi mkubwa kwa mara ya pili kwenye uchaguzi wa mwaka 1954 kuelekea uhuru kamili, Serikali ya Uingereza ilikataa kutamka tarehe ya uhuru na badala yake ikatangaza uchaguzi mwingine kufanyika mwaka 1956. Katika uchaguzi huo, CCP kilipata kura 398,000 dhidi ya kura 299,000 za upinzani; na kwa viti vya LEGCO, kilipata viti 72 kati ya viti 104. Kwa matokeo hayo, Uingereza ikaridhia Ghana kupata uhuru Machi 6, 1957.

Mwandishi wa Kimarekani, John Gunther aliyekutana na Nkrumah siku ya uhuru anaelezea haiba ya kiongozi huyo katika Kitabu chake “Inside Africa”, ifuatavyo: “Mwendo, mwenendo na hisia (gesture) zake ni zenye mvuto, nguvu na utulivu wa kuhuisha; hana mikogo wala kauli tata za kutia chumvi”.
Nkrumah, akiwa bado kapera hadi Desemba 1957, maisha yake yalitawaliwa na siasa pekee kuliko vitu vingine; hakuwa mpenzi wa michezo, kinywaji, sigara wala starehe za aina yoyote.

Alikuwa mtu mpweke, mwenye fikra wa kuwaza na kuwazua nyakati zote na hakuamini wenzake na kwa nadra alitaka ushauri wao. Aliweza kuchanganyika na wanawake kwa urahisi lakini hakupenda kuhusiana nao kwa karibu, iwe kwa upendeleo maalum wa kivikundi au mmoja mmoja hivi kwamba kabla ya uhuru aliwahi kusema hakuwa na muda wa kuoa, hadi aliposhinikizwa na mfumo wa Serikali baada ya uhuru.

Bila kumjulisha mtu, lakini kwa shingo upande, na pengine kwa kushauriwa na aliyekuwa Rais wa Misri, Gamal Abdel Nasser; Nkrumah aliamua kuoa mke kutoka Misri; mwanamke ambaye hakuwahi kumsikia wala kukutana naye kabla ya hapo hadi siku alipoletwa Ghana siku ya kufunga ndoa, Desemba 30, 1957, iliyoshuhudiwa na watu wasiozidi 30.

Binti huyo wa Kimisri, Fathia Rizk, aliongea lugha ya Kiarabu pekee, na kidogo sana, Kifaransa kwa kubabia; wakati Nkrumah aliongea Kiingereza kufanya wanandoa hao kuhitaji wakalimani. Kwa nini Nkrumah alichagua ndoa baridi k**a hiyo?

Erica Powell, mwanamama wa Kiingereza Msaidizi maalum wa Nkrumah, aliyeachiwa na Wakoloni kumsaidia kuweka sawa mambo ya utumishi na utawala (k**a ambavyo tu Mwalimu Nyerere alivyopewa Mama Joan Wickens mwaka 1961) wakati wakiondoka, anamnukuu Nkrumah katika kitabu chake “Private Female Secretary in the Gold Coast”, akimwambia: “Erica, Je, wajua kwamba mimi ni mtu mpweke nisiye na rafiki wala makundi, na kwamba kwangu kilichomhimu ni Kazi tu?”

Aliwahi kumwambia (1965) pia kwamba, kitu ambacho angependa kufanya ni kujiuzulu Urais na kutumia muda wake wote kwa Umoja wa Afrika. Erica anakiri Nkrumah aliwahi kumtamkia pia kuwa, ikitokea kwamba ameoa, kwake suala la mke, watoto na mambo ya kifamilia kwa ujumla yasingekuwa masuala ya Kiserikali bali ya kibinafsi; akisema “ni hatari sana, na kwa kweli ni ubatili mtupu, kwa mke na familia kujiona kuwa sehemu ya utawala na Serikali”.

Nkrumah alimwambia Erica, ndoa haikumuondolea upweke, akasema: “Wajua Erica; sikutaka kuoa, wala sikuoa kwa kupenda ila kwa sababu ya Urais”. Erica hakuelewa, kwa nini mtu wa hadhi kubwa k**a Nkrumah, mwenye elimu, akili na busara kubwa, aliamua kuoa msichana mdogo na ambaye hawakuelewana kwa kizuizi cha lugha. Hapa kulikuwa na mshabihiano uliofichika.

Ilitokea kwamba, Nkrumah alioa Misri si kwa bahati mbaya, kwa Rais mwanaharakati Kanali Nasser, mwenye siasa za mrengo wa Kikomunisti, aliyeingia madarakani kwa kupindua kijeshi Serikali ya Mfalme Farouk mwaka 1956. Nasser na Nkrumah, licha ya kuwa miongoni mwa waasisi wa OAU, walikuwa Waasisi pia wa Umoja wa Nchi zisizofungamana na upande wowote duniani (Non-aligned Movement – NAM), pamoja na Josef Bronz Tito (Yugoslavia) na Pandit Jawaharl Nethru (India). Wanne hao walikuwa pia wanamstari wa mbele wa kwanza na majabali dhidi ya ukoloni mkongwe, ukoloni mamboleo na ubeberu wa kimataifa.

Lakini pengine sababu kubwa zaidi kwa Nkrumah kumuoa binti huyo wa Kiarabu, ilikuwa ni kujaribu kuimarisha mshik**ano wa Kiafrika (Pan-Africanism) kwa kujenga tafsiri mpya kwamba “Mwafrika” maana yake si “Mtu mweusi” pekee, bali ni “mzalendo yeyote mkazi wa Afrika mwenye mapenzi mema kwa Afrika”.

Mafanikio ya Nkrumah kisiasa hayakuwa bila mikwara k**a anavyoelezea Genevova Marais, katika kitabu chake “Kwame Nkrumah As I knew Him” kwamba, “Kadri alivyopata mafanikio nchini, ndivyo alivyozidi kutowamini marafiki zake wa karibu, bila kujali jinsi walivyojitahidi kuonesha utii kwake. Kwa jinsi hii, alipoteza ushirikiano kiserikali na kubakia kuungwa mkono na Wana-CCP pekee, waliomwambia kile tu waliona angefurahi kusikia na kuacha mambo mengine yajiendee hovyo hivyo”. Kwanini?

Erica Powell anasema, tatizo la Nkrumah, na la madikteta wema wote (benevolent dictators) ni kwamba, “alikuwa hatabiriki; kwa haiba, aliweza kubadilika ghafla, akawa mkali kupindukia, asiyeambilika; lakini alikuwa mcheshi pia na mwenye kufikiria upya jambo akiona inafaa kufanya hivyo”.

Nkrumah alipinduliwa na Jeshi lake Februari 24, 1966 akiwa mjini Beijing, China akielekea Hanoi, Vietnam k**a Kiongozi wa Kimataifa mwenye jukumu la kusuluhisha vita ya Vietnam, kati ya Vietnam na Marekani enzi hizo za vita baridi. Alirejea Afrika lakini si Ghana, bali k**a mkimbizi uhamishoni nchini Guinea.

Mwalimu Nyerere alitaja sababu zenye ukakasi kidogo, juu ya kuangushwa kwa Nkrumah kuwa, “alifanya kosa kuruhusu rushwa na rushwa ikamlemea”. Je, ilikuwa rushwa pekee iliyomwondoa?
Kuanguka kwa Nkrumah hakukuja kwa sababu ya kukithiri kwa rushwa nchini Ghana, la hasha; wala si kwa sababu ya uongozi mbaya au kuharibika kwa uchumi. Nkrumah aliangushwa kwa kuthubutu kuchokoza ubeberu wa Kimataifa na kwa kutaka kuunganisha Afrika na nchi za dunia ya tatu kupambana na ubeberu huo.

Ndoto ya Nkrumah ya kuunda Shirikisho la Mataifa ya Afrika (United States of Africa) – “USA” mithili ya USA ya Marekani; kuunda ngome ya Kijeshi Afrika, mithili ya Umoja wa Kujihami Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) na kwa kujaribu kuinasua Afrika kutoka kwenye ushawishi wa Mataifa makubwa (Non-alignment) ilichangia pia.

Dalili zilijionesha mapema. Kuchapisha kwake kitabu, “Neo-Colonialism: The Highest stage of Imperialism” (Ukoloni Mamboleo: Hatua ya Juu kabisa ya Ubeberu) Oktoba 1965 kushambulia Ubeberu, kuliitia kichaa Marekani na kufuta msaada wa dola milioni 35 kwa Ghana. Miezi minne baadaye, akapinduliwa kwa msaada wa Shirika la Kijasusi la Marekani (CIA).

Kanali A.A Afrifa aliyeongoza mapinduzi hayo, alielezea sababu hizo miezi mitano baadaye, katika kitabu chake “The Ghana Coup”, kuwa ni “ndoto za Nkrumah juu ya Pan-Africanism na Muungano wa Afrika; kuunga mkono ukombozi wa kitaifa nchini Kongo na kwingineko, na chuki bila sababu dhidi ya nchi rafiki zetu za Kimagharibi”.

Ni ukweli usiopingika, wala si uzushi, kwamba kupinduliwa kwa Nkrumah ulikuwa ushindi kwa ubeberu wa Kimataifa na ukoloni mamboleo Afrika. Kuanzia hapo, msukumo wa Afrika kuungana umetoweka, udikteta na uporaji wa rasimali za Afrika umetia fora; Afrika inazidi kudhoofika katika nyanja zote kuliko mwanzo; haina jeshi la pamoja la kujilinda wala kutetea uhuru wake ila kwa “msaada” kutoka nje. Afrika iko njia panda

Nilikutana na mshkaji wangu wa primary Alishangaa sana akasema *Athuman?* ndio wew? upo kaka?". Nikamjibu nipo kiongozi ...
27/01/2022

Nilikutana na mshkaji wangu wa primary Alishangaa sana akasema *Athuman?* ndio wew? upo kaka?". Nikamjibu nipo kiongozi tunasindikiza wenye maisha yao, akacheka sana,, Mara akaanza kuzungumzia matatizo ya familia yake, nikamwambia tuyaache hayo mim mwenzako nimepitia makubwa, aling'ang'nia kuzungumzia kero za familia yake, ~_NIKAMSTOPISHA_ nikamwambia " Unadhani familia yako ina matatizo?" Basi sikiliza kisa changu hiki…. "Miaka michache iliyopita nilikutana na mwanamke mjane aliyekua na binti mkubwa tu, mimi na huyo mjane tukaamua kuoana. Baadaye baba yangu ambae alikuwa mkiwa baada ya kufiwa na mama kitambo tu akaamua kumuoa binti yangu wa kambo (yaani binti wa huyu mke wangu niliyemuoa akiwa mjane), hivyo huyo binti yangu wa kambo akawa mama yangu wa kambo na Baba yangu akawa mtoto wangu wa kambo wa kiume ambapo mke wangu akawa mama mkwe wa mkwe wake. Baadaye binti wa mke wangu yaani binti yangu wa kambo (ambaye kwa sasa ndiye mke wa baba yangu na hivyo kuwa pia mama yangu wa kambo) alipata mtoto wa kiume. Mtoto huyo wa kiume akawa mdogo wangu kwa sababu tulichangia baba mmoja. lakini kwa vile pia alikua ni mtoto wa binti wa mke wangu papo hapo akawa mjukuu wa mke wangu na mimi nikawa babu yake huyo mdogo wangu. Lakini hayo yote yalikua si kitu mpaka mimi na mke wangu tulipopata mtoto wa kiume. Sasa msichana (yaani binti ya mke wangu ambaye pia ni mke wa baba yangu ambaye ni ndugu wa mtoto wangu huyo wa kiume kwa kuchangia mama yao mmoja, akawa pia bibi yake na mwanangu (mwee!!). Hali hiyo ilimfanya pia baba yangu kuwa shemeji wa mtoto wangu (achilia kuwa babu yake!!) ambaye ndugu yake wa k**e kwa upande wa mama yao ndie mke wake baba yangu. Kwa hiyo mimi ni shemeji yake mama yangu wa kambo ambapo mke wangu ni mama mdogo (anti) wa binti yake mwenyewe. Mtoto wangu wa kiume ni mpwa wa baba yangu ambapo mimi nikawa babu yangu mwenyewe. Kabla sijammalizia jamaa akaondoka.😀😆😆😆

Somo: usifikiri wewe ndiye mwenye matatizo kuliko mwenzako.., hivyo punguza lawama kwa ambaye hawezi kukupa msaada kwa wakati huo wa shida zako..😃

HEKIMA, MAARIFA NA UFAHAMU   Omba kwa Mungu vitu vyote lakini kamwe usije ukasahau kuomba hekima, ufahamu na maarifa kut...
07/11/2021

HEKIMA, MAARIFA NA UFAHAMU

Omba kwa Mungu vitu vyote lakini kamwe usije ukasahau kuomba hekima, ufahamu na maarifa kutoka kwake.

Kabla hujaomba akupe kazi, akupe mke mzuri, akupe mume mzuri, akupe rafiki mwema, akupe watoto wema, kitu cha kwanza omba hekima, maarifa na ufahamu viwe ndani yako kabla ya vitu vyote.

Pesa ili uitumie vyema unatakiwa uwe na hekima, maarifa na ufahamu, vitu hivyo vitatu vitakufanya uweze kutumia pesa vizuri huku ukiwa humkwazi Mungu

Mapenzi au ndoa yenu ili iwe bora kitu cha kwanza omba hekima, maarifa na ufahamu viwe ndani yako kabla hujampata huyo mwenza wako

Kazi unayo tamani kuipata ili iwe na matokeo mazuri unahitaji uwe na hekima, maarifa na ufahamu. Vitu hivyo vitatu vitakusaidia ujue namna ya kutoka na kuingia salama sehemu ya kazi

Kwenye biashara yako hakikisha unamuomba Mungu hekima, maarifa na ufahamu viwe ndani yako ili ujue namna ya kuboresha biashara yako, ujue namna ya kuwahudumia na kuwajali wateja wako mbali na Changamoto zao

Watoto ili uweze kuwalea vyema unahitaji hekima, maarifa na ufahamu kwanza.

Kwenye kila kitu unachokifanya hakikisha Jambo la kwanza unaomba hekima, maarifa na ufahamu ili uwe bora sana.

KUTOKA MAKTABA PATA HISTORIA HII👇SAID MWAMWINDI MKULIMA ALIYEMUUA MKUU WA MKOA 👉Ilikua ni mnamo mwaka 1971 siku ya Krism...
07/09/2021

KUTOKA MAKTABA PATA HISTORIA HII👇

SAID MWAMWINDI MKULIMA ALIYEMUUA MKUU WA MKOA
👉Ilikua ni mnamo mwaka 1971 siku ya Krismasi ni miaka 48 imepita toka Mnyalukolo SAID ABDALLAH SIULANGA MWAMWINDI ammimimie risasi na kumuua aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Iringa marehemu Dr. WILBERT KLERUU.
Mauaji hayo yaliyokea tarehe 25/12/1971 kijijini Mkungugu Isimani Mkoani Iringa.

👉Dr. WILBERT KLERUU alikuwa ni mzaliwa wa Mwika Kilimanjaro ambaye alikuwa ni mmoja wa Watanzania wachache wakati huo waliokuwa na shahada ya uzamivu(PHD) ya uchumi wa kijamaa.
Dr. KLERUU alikuwa ni kipenzi cha Baba wa Taifa Mwalimu JK NYERERE kutokana na weledi na utendaji wake usio na mfano. Mwanzoni mwa mwaka 1971 DR.KLERUU alikuwaamehamishiwa mkoani Iringa kutokea Mtwara.

👉Dr. KLERUU alikuwa ni kiongozi machachari sana na ilikuwa kawaida kwake na alikuwa hana hiana kuwafokea hadharani watumishi wa umma wazembe.
Kwa hakika Dr. KLERUU alikuwa mbabe sana. Akiwa Iringa kuna wakati gari yake ilipigwa "overtake" na gari hilo lililompiga"-overtake" likamziba kwa mbele. Kufumba na kufumbua Dr. KLERUU alishuka k**a komandoo na kwenda kumuwasha vibao dreva wa gari hilo Dr. KLERUU mara kwa mara alipenda kuwafokea watu kwa kuwaambia "Hamnijui Mimi? Kawaulizeni watu wa Mtwara" na yeye hakuwa mtu wa kukaa ofisini k**a viongozi wengi wa wakati huo bali alijumuika na wananchi na kufanya nao shughuli za maendeleo bega kwa bega ambapo ilikuwa ni kawaida kwake kushika jembe kwa masaa kadhaa bila kula.

👉Kipindi hicho kulikuwa na kampeni kubwa ya kuwafanya wananchi walime mashamba ya pamoja na hivyo wakulima waliokuwa na mashamba makubwa walinyang'anywa kitendo ambacho hakikuwapendeza Wanyalukolo waliokuwa matajiri wenye mashamba makubwa ya mahindi.
Dr. KLERUU alihamishiwa Iringa ili akatekeleze mpango huo wa serikali na alipofika tu akatangaza kwamba mashamba yote binafsi yanapaswa kuwa ya ujamaa kufikia Novemba 1971.

👉Bw. MWAMWINDI alihamia eneo la Mkungugu Isimani mwaka 1954 akitokea Iringa mjini alikokuwa dreva. Alianza kilimo kidogo kidogo hatimaye akawa na mashamba makubwa ya mahindi ya hekari takriban 160. Akawa analima mashamba yake kwa trekta katika eneo hilo ambalo awali lilikuwa ni pori. Kipindi hicho hakukuwa na sehemu Tanzania iliyokuwa ikizalisha mahindi mengi k**a Isimani.

👉Jumamosi ya tarehe 24/12/1971
DR.KLERUU alitembelea mashamba mbalimbali maeneo ya Tarafani Igulu na Ndolela kuhamasisha kilimo cha pamoja. Kesho yake Jumapili ya tarehe 25/12/1971 Dr. KLERUU( ambaye hakuwa na Jumapili wala skukuu) aliendelea na shughuli hizo za kutembelea mashamba ya wakulima.

👉Muda wa saa 11 jioni Dr. KLERUU alifika kwenye shamba la MWAMWINDI na kumkuta akilima kwa trekta lake.
Pamoja nae kulikuwa na mtoto wake na watu wawili aliowaajiri
Bw. Joseph Kusava ambaye ni mkwe wake pamoja na wake zake waliokuwa wakishirikiana nae kulima siku hiyo.

Moja ya wake wake alisema👇
Dr. KLERUU alifika shambani hapo akiendesha gari lake binafsi aina ya rangi ya bluu na ubavuni ikiwa imeandikwa RC-Iringa.
Baada ya kushuka alimfuata moja kwa moja MWAMWINDI na kuanza kumuhoji maswali mengi kwanini hataki mashamba yake yawe ya ujamaa. Akamwambia "Unafanya nini hapo?"Shuka shenzi we". MWAMWINDI akamuuliza "kwanini unanitukana?" Dr. KLERUU akamjibu "Funga mdomo wako, n'ge n'ge n'ge nini? Kwanini nawaambia hamsikii? Blood fool" Dr. KLERUU aliyekuwa na kawaida ya kutembea na kifimbo kidogo akakitumia kumchomachoma nacho MWAMWINDI.

👉MWAMWINDI akafura sana hivyo akaanza kwenda ndani kupitia eneo la makaburi ya baba yake na ndugu wengine huku Dr. KLERUU akimfuata na alipoyaona makaburi akasema "Tazama unaendelea kujenga nyumba za kudumu" MWAMWINDI akamjibu "Hizi sio nyumba ni mahali ninapozika ndugu zangu". Dr. KLERUU akajibu "Ni mahali unapozikia mirija wenzio mbwa we!".

Mnyalukolo MWAMWINDI akawaamehamaki sana. Akasema akaingia ndani akachukua gobore akatoka nalo nje na kumfyatulia risasi Dr. KLERUU ambaye alianguka na kufariki hapohapo MWAMWINDI aliuchukua mwili wake akauweka kwenye buti ya gari ya Mkuu huyo wa Mkoa akachukua na kofia ya Pama ya Mkuu wa Mkoa akaivaa yeye na kuanza safari ya kilometa 40 kwenda Iringa mjini.

👉Mjini Iringa watu walishangaa kuona gari ya Mkuu wa mkoa inapita upande wa kulia kwa vile mtaa wa Jamatini ulikuwa ni "One way" lakini wakahisi huenda Mkuu wa mkoa ana dharura. Saa 1 jioni MWAMWINDI akafika kituo kikuu cha polisi akaenda moja kwa moja kaunta akamkuta PC MBETA KASONDA na kukwambia "Ebu nenda kwenye buti ukaitoe mbwa yenu nimeishaiua" na kumkabidhi bunduki pamoja na funguo za gari. PC KASONDA hakuamini macho yake alipouona mwili wa Dr. KLERUU ukiwa umetapakaa damu. Dr. KLERUU alikuwa amevaa ovaroli nyeusi na miwani. Hivyo mara moja PC KASONDA akamuweka MWAMWINDI chini ya ulinzi. Mtu mwingine aliyekuwepo kituoni hapo ni mzee DAVID BUTITINI(ambaye alikuwa askari polisi na baadaye kada wa CCM Iringa). Tarumbeta likapulizwa na askari wakakusanyika na kupewa rasmi taarifa ya kifo hicho cha Mkuu wao wa mkoa na gari lake likahifadhiwa nyuma ya kituo cha polisi. Askari wanne wakaenda kuleta kitanda cha magurudumu toka hospitali na hatimaye mwili wa Dr. KLERUU ukapelekwa "mortuary" Kesho yake siku ya jumatatu mji mzima wa Iringa uligubikwa na simanzi kubwa.

👉Kuna kundi la watu ambao walikuwa wakimchukia sana Dr. KLERUU kutokana na aina ya uongozi wake hivyo lilipopata tu taarifa za kifo chake wakanunua makreti ya bia usiku huohuo na kuanza kunywa kwa kushangilia hadharani Msako ulipoanza usiku huohuo jamaa hao walikuwa wa kwanza kuk**atwa😁

👉Mzee BUTININI ambaye pia alikuwa Mtwara wakati DR. KLERUU alipokuwa Mkuu wa Mkoa anakiri kuwa ni kweli DR. KLERUU alikuwa mtu wa shoka
"Ni kweli hata kule Mtwara alionekana mtemi sana mwenye kuhimiza mambo kwa nguvu. Lakini lazma muelewe maeneo ya Mtwara yalikuwa ya vita na tulikuwa tukiwasaidia ndugu zetu wa Frelimo hivyo kule kulihitaji mtu k**a DR. KLERUU Mtwara DR. KLERUU hakukumbana na upinzani ila Iringa hali ilikuwa tofauti Kwa mawazo yangu Dr. KLERUU alipaswa kwanza kujifunza juu ya mila na desturi za watu wa Iringa Maana watu wa Iringa ni watu wa Iringa tu."

👉Mauaji hayo ya Dr. KLERUU yalimsikitisha sana Mwalimu NYERERE wakuu wa mikoa na wananchi mbalimbambali Lilikuwa ni tukio lililoongelewa nchi nzima Majirani na wazee wengi waliokuwa wakilima pamoja na MWAMWINDI walisombwa na vyombo cha usalama na kumwekea ndani kuisaidia polisi ambapo walikuwa wakik**atwa na kusafirishwa usiku kwa ndege za jeshi. Takribani watu 30 walik**atwa wakiwemo wazee maarufu k**a IBRAHIM KHALILI, PESAMBIL MURSALI na wengineo na kupelekwa sehemu mbalimbali za nchi mfano Shinyanga, Mwanza na Zanzibar. Cha kusikitisha ni kwamba ndugu zao hawakujua wamepelekwa wapi Aidha nyumbani kwa MWAMWINDI huko Mkungugu kukawa kunalindwa na askari wa FFU muda wote.

👉Kitendo cha kuk**atwa majirani na marafiki wa MWAMWINDI kilileta uhasama mkubwa baina ya ndugu wa majirani hao na familia ya MWAMWINDI.
Ikabidi mwanae AMANI MWAMWINDI (21) alazimike kutafuta kibali cha DC Iringa kwenda gereza la Dodoma alikokuwa anashikiliwa MWAMWINDI. Alipoganikiwa kukipata alikwenda na akamueleza hali hiyo ambayo ilimsikitisha sana Mzee MWAMWINDI.
AMANI akamshauri baba yake aandike barua kwa Rais NYERERE nae akafanya hivyo siku hiyohiyo. Katika barua hiyo MWAMWINDI alimueleza Mwalimu kwamba yeye ndiye aliyemuua Dr. KLERUU hivyo wengine hawahusiki hivyo waachiwe Baada ya kupita siku kadhaa wazee hao majirani wakaachiwa na kurejea kijijini hapo Isimani. Hata hivyo tafrani hiyo iliyokuwa imewakumba ikafanya wengi wahame eneo hilo kwani waliishaona "togwa limeingia nzi"😁
Upelelezi wa mauaji hayo ulienda haraka na MWAMWINDI akafunguliwa kesi ya mauaji ya kukusudia Mahak**a kuu.

👉Kesi ilipoanza kusikilizwa ilivuta hisia za watu wengi na umati wa watu uliokuwa ukitamalaki kila siku mahak**ani ulikuwa si wa nchi hii
Tarehe 2/10/1972 baada ya mashahidi wa pande zote kutoa ushahidi wao akiwemo RPC wa Iringa (Abubakar Hassan) aliyetoa ushahidi upande wa MWAMWINDI kwamba hakuwa na taarifa kwamba Mkuu huyo wa Mkoa angetembelea eneo hilo ndio maana hakumpa "Police es**rt"

👉Jaji GABRIEL CHIKE ONYIUKE toka Nigeria alimtia MWAMWINDI hatiani na kumuhukumu kunyongwa hadi afe. Hii ilikuwa ni baada ya kuukataa utetezi wake kwamba alitenda kosa hilo baada ya kurukwa na akili na pia alikasirishwa na marehemu Mh. Jaji aliona kwamba ingawa ni kweli MNYALUKOLO wa kawaida huwa si mtu wa mchezo😁 mchezo anapodhihakiwa hasa mbele za wake zake lakini kitendo cha MWAMWINDI cha kwenda ndani kufuata bunduki kilionesha pasina shaka kwamba aliua kwa kudhamiria.

👉Adhabu hiyo ya kifo ilitekelezwa mara moja kwani Mwalimu NYERERE alisaini hati ya kifo cha MWAMWINDI
hiyo ilikuwa ni moja ya hati tatu za vifo zilizosainiwa na Mwalimu NYERERE kuidhinisha kunyongwa kwa binadamu katika uongozi wake wa miaka 24 katika taifa hili.
Kesi hii ilikuwa ya aina yake na haikuchukua hata mwaka mmoja toka tukio kutokea na adhabu kutolewa tofauti na kesi nyingine za mauaji ambazo kwa kawaida huchukua miaka mingi kabla ya hukumu kutolewa Kesi hii ilichukua miezi kumi tu🤔

Address

Mipango
Dodoma

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Maarifa Katika Jamii posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category