QmediaTz

QmediaTz P.O.Box 2364 Dodoma - Tanzania
+255-717-066-207
e-mail - [email protected]

03/03/2026

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema uwekezaji wa Serikali katika mradi wa ujenzi wa matenki 15 ya kuhifadhi mafuta wenye thamani ya Sh 678.6 bilioni ni hatua ya kimakakati inayolenga kuimarisha Tanzania k**a kitovu cha biashara cha ukanda na kimataifa.

Dkt Samia ameeeleza hayo leo wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa matenki hayo eneo la Kigamboni, Dar es Salaam. Ujenzi huo ukikamilika utapunguza muda wa meli kusubiri kushusha mafuta kutoka siku 22 za sasa hadi siku saba tu, huku mchakato wa kushusha mafuta ukitarajiwa kufanyika ndani ya siku moja badala ya siku saba.

“Hatua hii ni uthibitisho k**a Taifa tumeamua kujiandaa na kutumia kikamilifu jiografia ya nchi yetu k**a lango kuu la kuhudumia nchi zisizo na bahari.Tumedhamilia kuhudumia wenzetu kibiashara na uwekezaji na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara katika ukanda huu,” amesema Dkt Samia.

Amesema bandari za Tanzania ikiwemo ya Dar es Salaam, zina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi na ustawi wa wananchi, ndio maana Serikali imeamua kufanya maboresho ya miundombinu na huduma za bandari za Bahari ya Hindi na maziwa makuu.

Dkt Samia amesema katika mchakato wanashirikiana na sekta binafsi k**a ambavyo sera inavyoeleza kuwa ‘maendeleo yetu, hatutakwenda peke yetu, tutakwenda na sekta binafsi’.

“Tumekubaliana na kushirikisha sekta binafsi katika safari yetu ya maendeleo na tija ndio hii mnayoiona leo,” ameeleza Dkt Samia.

Address

Kondoa Road
Dodoma
670

Telephone

+255-767-066-207

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when QmediaTz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to QmediaTz:

Share