
24/04/2025
Kesi imeanza kusikilizwa Mbele ya Mh. Hakimu Mhini
Mawakili wa utetezi wamefika lakini waserikali na mtuhumiwa watakuwa kwa njia ya mtandao.
Muda huu anaonekana kwenye screen afisa wa magereza (sijui k**a ni mkuu wa gereza) lakini Mh. Lissu haonekani. Kesi inaelekea kuanza hapa.
Mawakili wa serikali wanaulizwa wapo tayari nao hawaonekani kwa sasa. Maana wanaendesha kesi kwa njia ya mtandao.
Wakili Mpale Mpoki anasema upande wa utetezi tuko tayari na upande wa serikali walikuwa na taarifa ya kesi na wanajua tarehe ya kesi kwahiyo anasisitiza tuendeleeee
Upande wa Jamhuri tuko tayari, anasikiki Wakili wa Serikali anasema hivyo. Wanaulizwa Magereza mko tayari? Anajibu askari magereza huyu afisa anasema Msh*takiwa amegoma kusikiliza kesi kwa njia ya mtandao.
Anasema nimemjulisha mtuhumiwa na amegoma kusikiliza kesi kwa njia ya mtandao kwahiyo amegoma
Upande wa Jamhuri tupo, Job Mrema wakili wa serikali mwandamizi niko pamoja na
Nassoro Katuga PSA
Cathbert Mbiringi , Tuko tayari kuendelea na Shauri. Shauri lilikuja kwa maelezo ya awali. Ameambiwa atulie kwanza
Utetezi wanajitambulishaa anasema mzee Mpale Mpoki
Alute Mugwai
Ruge Nshala
Peter Kibatala
Jeremiah Mtobesya
Nashon Nkungu
Gaston Garubindi
Deus Singa
Eben Silayo
Deogratias Cosmas Mahinyila
Edson Kilatu
Fredrick Kihwelo
Michael Mwangasa
Catheters Rafael Mandiho
Dickson Matata
Emanuel Chengula
Paul Kisabo
Edward Heche
Jebra Kambole
Maria Mushi
Sisty Masawe
Ikoti Lissu
Fredrick Msaki
Jacob Mogendi
Fikiri Gabriel
Florian Francis
Hekima Mwasipu
Emmanuel Ukashu.
Wakili Mpale Mpoki Anamaliza kutambulisha jopo la Mawakili wa Utetezi.
Wakili wa Serikali Job Mrema anasema yuko tayari kuendelea na shauri ambalo liipangwa kwa ajili ya maelezo ya awali na upande wa jamhuri tuko tayari lakini msh*takiwa hayupo hapo.
Anasema tumewaserve utetezi maelezo ya awali leo asubuhi kupitia wakili Hekima Mwasipu.
Shauri hili lilokuja kwa maelezo hayo na msh*takiwa hayupo mbele ya Mahak**a. Kutokana na hali hiyo tuliyoipata kutoka magereza. Kwa upande wa jamhuri tunaomba ahirisho la shauri hili kwa tarehe nyingine.
Ambapo tunaomba kwa upande wa jamhuri tupewe mwezi mmoja kutoka sasa. Watu wanaguna hapa mahak**ani.
Anaendelea ili mawakili upande wa utetezi waongee namtuhumiwa ili akubali kuja kusomewa maelezo ya awali.
Hakimu anamuuliza umemaliza au bado?
Anasema Job Mrema Wakili wa serikali kuwa nimemaliza mheshimiwa.