Asili Media

Asili Media News & sports entertainment
Culture, nature, trending
Follow Asili Media
Advertising and promotion

🔴 TANGAZO LA WITO WA KUMTAFUTA MTOTO ALIYEPOTEATunatoa wito kwa jamii kusaidia katika kumtafuta mtoto  Hance Konoladi , ...
13/01/2026

🔴 TANGAZO LA WITO WA KUMTAFUTA MTOTO ALIYEPOTEA

Tunatoa wito kwa jamii kusaidia katika kumtafuta mtoto Hance Konoladi , ambaye AMEPOTEA maeneo ya Tegeta A – CCM Jijini Dar es Salaam.

📍 Maelezo Muhimu:
👦 Jina: Hance Konoladi
🏠 Anatokea: Tuliani, Morogoro
📅 Alipotea: Tarehe 18 Desemba 2025
👕 Mavazi: Tisheti ya rangi ya maziwa
🎂 Umri: Miaka 10

Tangu siku hiyo hadi sasa, hajapatikana. Ikiwa umeona au una taarifa zozote zitakazosaidia kumpata, tafadhali wasiliana na namba zifuatazo:

📞 0653 665 946
📞 0760 714 787

Tafadhali shiriki tangazo hili ili tuweze kumrudisha Hance mikononi mwa familia yake.
Msaada wako ni wa thamani kubwa.

🙏 Asante kwa ushirikiano wako!

  Yaondoa Waamuzi Kutokana na Utata wa Maamuzi AFCON 🇲🇱🇨🇲Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limeripotiwa kuwaondoa b...
13/01/2026

Yaondoa Waamuzi Kutokana na Utata wa Maamuzi AFCON 🇲🇱🇨🇲

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limeripotiwa kuwaondoa baadhi ya waamuzi waliokuwa wakisimamia mechi za AFCON 2025 nchini Morocco, ikiwa ni sehemu ya tathmini ya viwango vya uamuzi mashindanoni.

Miongoni mwa waamuzi walioondolewa ni Boubou Traoré kutoka Mali ambaye alisimamia mechi ya hatua ya 16 bora kati ya Tanzania na Morocco, ambapo alitoa maamuzi yaliyozua mjadala mkali.
Pia, Abdou Abdel Medire kutoka Cameroon naye ametajwa kuondolewa.

Hatua hiyo inaelezwa kuwa ni juhudi za CAF kuhakikisha haki na ubora wa maamuzi unaimarishwa katika hatua zilizosalia za mashindano.

📌 Endelea kufuatilia kwa habari sahihi na za kina.
👉 Follow Asili Media kwa taarifa moto moja kwa moja!

10/01/2026

📝 Tafakari: Je, Ni Haki Mwanafunzi Kuadhibiwa Hivi?

Picha na simulizi k**a hizi zimekuwa zikisambaa mara kwa mara mitandaoni — mwanafunzi akiadhibiwa vikali hadi kufikia hatua ya kuumizwa kimwili na kisaikolojia. Swali linabaki: *Je, alikosea kiasi gani?* Na zaidi, adhabu hii ni njia sahihi ya kurekebisha au ni udhalilishaji?

🔍 Ni chuki binafsi za walimu dhidi ya wanafunzi?
Au ni matokeo ya hasira zisizodhibitiwa? Kuna wakati walimu, kwa kisingizio cha “kurekebisha”, huenda mbali kupita kiasi — na hivyo kugeuza shule sehemu ya mateso badala ya kuwa mahali pa kujifunza na kukuza ndoto.

⚠️ Madhara kwa mwanafunzi ni makubwa:
- Kuporomoka kwa ufaulu
- Hofu ya shule
- Kuacha shule kabisa
- Matatizo ya afya ya akili

🎓 *Tunasimama na wanafunzi.*
Haki yao ni kufundishwa, kuelekezwa, na kusaidiwa — si kuumizwa. Nidhamu inahitajika, lakini *adhabu za kikatili* hazijawahi kuwa suluhisho sahihi.

🗣️ *Toa maoni yako k**a mzazi, mwanafunzi, au mdau wa elimu:*
- Nini kifanyike kudhibiti adhabu za namna hii?
- Tunajengaje mazingira salama na rafiki kwa wanafunzi?

👇 Andika maoni yako
📲 Fuatilia Asili Media kwa mijadala yenye mguso na hoja nzito za kijamii.

  SC inawaalika wawekezaji wenye sifa kuwasilisha barua za kuonyesha nia ya kushirikiana katika uendelezaji wa eneo la  ...
09/01/2026

SC inawaalika wawekezaji wenye sifa kuwasilisha barua za kuonyesha nia ya kushirikiana katika uendelezaji wa eneo la Jangwani – Uwanja wa Kaunda . Lengo ni kujenga uwanja wa kisasa kupitia mfumo wa ubia wa kibiashara ,ili kuboresha miundombinu ya michezo na kuongeza thamani ya uwekezaji wa klabu.

  SC 0 - 1 AZAM FC“Dakika 90 Simba Wapo Uwanjani, Lakini Mpira Hauwajui”Simba SC walicheza k**a waliokwenda matembezi, s...
09/01/2026

SC 0 - 1 AZAM FC
“Dakika 90 Simba Wapo Uwanjani, Lakini Mpira Hauwajui”

Simba SC walicheza k**a waliokwenda matembezi, si kwa ajili ya ushindani. Hakukuwa na kasi, nia, wala ubunifu uwanjani—ni k**a walijikuta tu wamevaa jezi. Azam FC walitumia mwanya huo kuwapa kichapo kidogo lakini cha maana:
1-0

⚽️ Matokeo haya yameacha maswali kwa mashabiki wa Simba. Je, huu ni mwanzo wa mwelekeo mbaya?

👉 Fuatilia Asili Media Media kwa uchambuzi zaidi na habari motomoto.

Tangu nimjue Djigui Diara ikifika wakati wa Penati basi Huwa naamini upande wake unaweza Fanya lolote .... ! Ni mara cha...
04/01/2026

Tangu nimjue Djigui Diara ikifika wakati wa Penati basi Huwa naamini upande wake unaweza Fanya lolote .... !

Ni mara chache sana timu yake imepoteza kwenye upande wa mikwaju ya Penati ....

Djigui sijawahi mshuhudia kwenye Penati 5 ukamfunga zote hio hakuna haipo kabisa wakuu 😄

Leo kachomoa Penati 2 zimemtosha kuwapeleka Mali robo fainali ......

Kituo kinacho fuata ni dhidi ya Senegal !

🇺🇸🇻🇪 BREAKING: Marekani Yamtia Mbaroni Rais wa Venezuela Nicolás Maduro!Aliyekuwa Rais wa Marekani  Donald Trump ametang...
03/01/2026

🇺🇸🇻🇪 BREAKING: Marekani Yamtia Mbaroni Rais wa Venezuela Nicolás Maduro!

Aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuwa Rais wa Venezuela Nicolás Maduro na mkewe wamek**atwa huku Marekani ikianzisha mashambulizi makubwa ya kijeshi dhidi ya Venezuela.

⚖️ Mwanasheria Mkuu Pam Bondi amesema Maduro amefunguliwa mashtaka ya *madawa ya kulevya na silaha huko New York, na atashtakiwa kikamilifu katika mahak**a za Marekani.

🌐 Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio amesema hakutakuwa na hatua zaidi za kijeshi, kulingana na taarifa kutoka kwa Seneta wa Republican.

🇻🇪 Serikali ya Venezuela imetangaza hali ya hatari ya kitaifa, ikilaani hatua hiyo k**a *uvamizi wa kijeshi wa hali ya juu.

👀 Mshuhuda mmoja huko Caracas ameiambia BBC: "Moyo wangu ulikuwa unapiga kwa kasi, miguu ikitetemeka," huku video zikionyesha moshi mzito ukitanda angani

Tukio hili linakuja baada ya wiki za mvutano mkali kati ya Trump na Maduro.

📍Je, uko Venezuela? Tuandikie ushuhuda wako.
Asili Media

🟠 "Msukuma Nimetolewa Ushamba!" - Phina Afurahia Likizo Ya Kipekee Dubai 🇦🇪  Mrembo na msanii nguli kutoka Tanzania *Phi...
02/01/2026

🟠 "Msukuma Nimetolewa Ushamba!" - Phina Afurahia Likizo Ya Kipekee Dubai 🇦🇪

Mrembo na msanii nguli kutoka Tanzania *Phina* amewashangaza mashabiki wake baada ya kueleza kuwa ni hadi Disemba 2025 ndipo alielewa maana ya “vacation” 😄! Akiwa Dubai, amefurahia kila sekunde hadi kudai "Nimezurura, nimetolewa ushamba kabisa!"👏🔥

Anasema atashare uzoefu wake wote kupitia *TikTok, Instagram & Snapchat — mambo bado ni moto!

📌 Kwa burudani na taarifa k**a hizi, endelea kuifuatilia kurasa yetu.
🔸Follow Asili TZ kwa simulizi motomoto na updates za burudani, lifestyle na utalii!

02/01/2026
02/01/2026

🧵 "Sindano ndogo inayoshona makoti..."
— Twenty Percent (20%)🎙️

_"Ukitaka amani ya kweli:_
✔️ Punguza mahitaji yako
✔️ Ridhika na ulicho nacho
✔️ Ongeza kipato chako
✔️ Epuka tamaa mbaya"_

🧠 Maneno ya busara kutoka kwa msanii mkongwe wa muziki Tanzania 🇹🇿
| |
✨ Maisha ni rahisi, tukiyachukulia kwa urahisi.

Address

Dodoma

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Asili Media posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share