07/08/2026
π° ZIARA YA KITAALUMA | Wanafunzi wa UDOM Digital TV Wajifunza kwa Vitendo Mwananchi Communications Limited
Wanafunzi wa UDOM Digital TV, kutoka Idara ya Sanaa na Mafunzo ya Vyombo vya Habari katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), wamefanya ziara ya mafunzo kwa vitendo katika Mwananchi Communications Limited (MCL)kwa lengo la kupata uzoefu wa moja kwa moja kuhusu shughuli za uandishi wa habari, uzalishaji wa maudhui na uchapishaji wa magazeti katika mazingira halisi ya kazi.
Katika ziara hiyo, wanafunzi walipata fursa ya kutembelea idara mbalimbali za kampuni hiyo, zikiwemo kitengo cha uhariri, uandishi wa habari, uzalishaji wa maudhui ya kidijitali na uchapishaji. Aidha, walijifunza kuhusu hatua mbalimbali za uzalishaji wa habari kuanzia ukusanyaji wa taarifa, uandishi na uhariri, hadi uchapishaji na usambazaji wa magazeti pamoja na uchapishaji wa maudhui kwenye majukwaa ya kidijitali.
UDOM Digital TV inatoa shukrani za dhati kwa uongozi na wafanyakazi wa Mwananchi Communications Limitedkwa mapokezi mazuri, ushirikiano na elimu waliyoitoa kwa wanafunzi wetu. Ushirikiano huu unaendelea kuimarisha ubora wa mafunzo kwa vitendo na kukuza weledi wa wanahabari wa kizazi kijacho.