Bongo Simulizi

  • Home
  • Bongo Simulizi

Bongo Simulizi Karibu kwenye dunia ya simulizi za kutisha!

Hapa utapata hadithi za kutisha, za kichawi, simulizi za maisha, mapenzi yenye drama, na matukio ya kushtua yanayokufanya ushike pumzi hadi mwisho.

😳😳😳😳👇👇👇👇👇
04/01/2026

😳😳😳😳👇👇👇👇👇

Asha alikuwa ana njaa tu. Hakutarajia kabisa kile ambacho macho yake yangeshuhudia siku hiyo.Alipoingia kula kwenye hoteli ya kawaida kabisa ya mtaani, kila ...

03/01/2026

Ndagu ya mwanangu, nilimtoa mwanangu ndagu ili nipate utajiri. Kilichotokea ni kibaya zaidi.

02/01/2026

Nyuma ya shule. Ni simulizi inayomuhusu binti rehema alietoka familia ya kimaskini akajiunga na shule ya sekondari ila alipofika akajiunga na kundi la mabinti walioshindikana kitabia na mwisho wa siku akajikuta amepoteza kila kitu.

Simulizi mpya  👇👇👇 Bonyeza kutazama👇👇👇👇
02/01/2026

Simulizi mpya 👇👇👇 Bonyeza kutazama👇👇👇👇

Kuna mambo ambayo hayafundishwi darasani…Rehema aliondoka nyumbani kwao Kigoma akiwa na sanduku lake la bluu,macho yakiwa yamejaa ndoto na hofu.Akiwa shuleni...

31/12/2025

Bundi mtu, uchawi alioenda kununua ili alipize kisasi baadae ukawa changamito kwake.

30/12/2025

Uchawi wa kisukuma, mzee mmoja apikua ndie mwenye nyumba akawa anaroga watu na kuwatoa misukule, je nini kitatokea? Fatilia simulizi hii upate kuelewa kiundani zaidi.

28/12/2025

Kilichomptapa mume baada ya kuchepuka, wivu wa mapenzi ndio chanzo. Ila mme wake kwa bagati nzuri akapona.

UNAWEKA PESA KILA SIKU BAADAE UNAKUTA HAKUNA PESA AU ZIPO KIDOGO.PESA ZINAONDOKA ZENYEWE KWENYE KIBUBU.VIBUBU ANAVYOUZA ...
27/12/2025

UNAWEKA PESA KILA SIKU BAADAE UNAKUTA HAKUNA PESA AU ZIPO KIDOGO.

PESA ZINAONDOKA ZENYEWE KWENYE KIBUBU.

VIBUBU ANAVYOUZA VINAUCHAWI NDANI YAKE.

KABLA YA KUVIUZA ANAVILAZA MAKABURINI KUVIROGA.

Karibu tujifunze kitu kwenye simulizi hii ya USINUNUE KIBUBU TENA.

Kabla hatujaianza simulizi yetu, Tafadhali nisaidie kubonyeza hiyo like batan hapo.
KISHA TUANDIKIE Comenti YAKO HAPA CHINI UNASOMA SIMULIZI HII KUTOKEA WAPI, MKOA GANI NA NINI MAONI YAKOJUU YA SIMULIZI HII JE HII YA KIBUBU ISHAKUKUTA.

HAYA , TUIANZE SIMULIZI YETU SASA

Mtaani kwangu kulikuwa na kijana mmoja anayeitwa Masanja. Alikuwa maarufu sana kwa kazi ya useremala. Hakuwa fundi wa kawaida, kila mtu alikuwa anamjua k**a bwana vibubu. Vibubu vya mbao, ndivyo vilivyomfanya awe na jina. Kila nyumba hapo mtaani, karibu kila familia, ilikuwa na kibubu cha Masanja.

Alikuwa kijana mtulivu, mkimya, na alionekana hana matatizo na mtu. Watu walimpenda, walimuita fundi hodari. Na kweli vibubu vyake vilikuwa vinavutia… vilikuwa vinauzwa kwa bei ndogo ambayo kila mtu aliweza kuimudu.

Kila alipomaliza kutengeneza vibubu vipya, Masanja hakuvihifadhi nyumbani. Wengi walidhani labda anavihifadhi chumbani kwake au kwenye ghala. la hasha. Masanja alikuwa akichukua vibubu usiku wa manane, akavibeba kwa gunia, kisha anaelekea kwenye makaburini.

Alipofika aalivilaza vibubu juu ya kaburi . Halafu alipomaliza, aliinua mikono yake juu na kuanza kunong’ona maneno kwa sauti ya chini, maneno ambayo hakuna mtu aliyeweza kuyaelewa.

Alipomaliza, aliondoka taratibu. Asubuhi, vibubu vile vilivyokuwa makaburini vilichukuliwa, vikapelekwa dukani kwake k**a bidhaa za kuuza. Watu walifika, wakavinunua kwa furaha, wakiamini vitawahifadhi pesa zao.

Lakini kumbe vibubu vile havikuwa vibubu vya kawaida. Vilibeba nguvu za giza.

Siku moja, Mzee Rashid ambae alikuwa mzee mstaafu, Alinunua kibubu cha Masanja, akakiweka chumbani. Kila siku alipokuwa akipokea hela ya pensheni yake ndogo ndogo, alikuwa akiweka ndani ya kibubu kile.

Baada ya miezi mitatu, siku ya kukifungua ikafika. Mzee Rashid alipiga mahesabu kichwani, alikuwa amehifadhi zaidi ya shilingi laki tatu. Akakikata kibubu… lakini cha kushangaza, kilikuwa tupu! Hakukuwa na hela hata moja.

Mzee Rashid alishtuka, akawa na hasira. Macho yake yakageuka kwa watoto wake. “Nyie! Nyie mnanihujumu! mmeniibia hela zangu kwenye kibubu changu!”

Watoto wakajitetea, wakasema hawajui lolote. Lakini mzee hakusikia. Akaanza kugomba kwa hasira, akiwatuhumu kuwa wezi.

Ndani ya nyumba ile, imani ikatoweka. Mtoto wa kwanza akaamua kuondoka nyumbani, akisema hawezi kuishi na baba anayemtuhumu kaiba wakati hajaiba.

Kwa siri, jirani zao wakawa wanasema, “Mbona hii imekuwa kawaida? Kila mtu anayenunua kibubu cha Masanja, hela zake hazikai.”

kwenye familia ya Bi Halima alikuwa mama wa sokoni, akiuza nyanya na vitunguu. Alinunua kibubu akiamini itamsaidia kuokoa hela za mtaji. Kila siku baada ya kuuza, akirudi nyumbani, aliweka hela kidogo ndani ya kibubu chake.

Siku moja, alipohesabu mtaji wake, akagundua hela hazilingani. Kila anachoweka hakionekani kikikua. Alihisi labda jirani yake ndiye anamuibia. Akamkabili sokoni mbele ya watu:

“Halima! Unadhani sijui? Wewe ndiye unaingia kwangu kuchukua pesa zangu! Siku nyingine utanijua mimi ni nani!”

Walichambana sana, wakawa maadui wakubwa. Hela za Halima ziliendelea kutoweka, akishindwa kueleza ni nani anayemnyonya.

Wakati sintofahamu inazidi kuwa kubwa, kijana aliyekuwa anapanga kufunga ndoa, naye alikuwa amenunua kibubu . Alitunza kila senti aliyopata kutoka kwenye biashara yake ndogo ndogo ya boda boda. Ndani ya miezi miwili mitatu, alikuwa ameweka zaidi ya milioni moja.

Lakini siku alipoamua kukifungua na kupeleka kwa mchumba wake k**a ushahidi wa maandalizi ya harusi… kibubu kilikuwa tupu! Hakuna hela hata moja.

Matukio haya yakaendelea kusambaa sana. Kila mtu aliyekuwa na kibubu cha Masanja alikuwa na malalamiko: pesa kupotea, ugomvi kuibuka, watu kuhisiana wizi.

Mtaani kukaanza kuwa cha migongano. Rafiki walikosa kuaminiana, familia zikavunjika. Watu walibaki wakishangaa: “Kwa nini kila mtu mwenye kibubu cha Masanja, pesa zake zinapotea au kukuta zipo tofauti na ulivyokuwa ukitegemea?”

Wazee wa kijiji walianza kusema huenda kuna mambo ya kichawi. Lakini bado hakukuwa na uthibitisho.

Siku moja usiku, vijana watatu walikuwa wakitoka sherehe ya harusi kijijini jirani. Walipita karibu na makaburi yaliyokuwa nyuma ya kijiji. Waliposogea, wakasikia sauti ya mtu akinong’ona maneno yasiyoeleweka.

Waliposogea kwa makini, wakamwona mtu akiinama juu ya kaburi, akiwa na gunia. Alikuwa akilaza vibubu juu ya makaburi na kuvifunika kwa kitambaa cheusi. Wakatizamana kwa mshangao.

“Huyo ni Masanja! Fundi seremala!” mmoja wao akanong’ona.

Walisimama wakiwa wanamrekodi na simu, wakamuona akiinua mikono juu kana kwamba anafanya tambiko. Walijificha kwenye vichaka hadi alipoondoka, kisha wakatoka na kuapa:

“Lazima tuwaambie watu wa kijiji. Huyu ndiye anayetumaliza.”

Asubuhi yake, vijana wale walipoamka, hawakukaa kimya. Walianza kusimulia walichokiona:

“Tulimuona kwa macho yetu! Masanja anapeleka vibubu makaburini!”

Habari zikaanza kuenea kwa kasi. Kila nyumba, kila kona ya kijiji, watu walikuwa wakisema maneno yale yale:

“Masanja ndiye mchawi! Vibubu vyake si vya kawaida.”

Wazee wa kijiji wakaita mkutano mkubwa chini ya mti . Watu walijaa kwa wingi, kila mtu akitaka kusema lake.

Mzee mmoja akasema:

“Kwa muda mrefu tumevumilia. Vibubu vyake vimetugombanisha. Vijana wamethibitisha walichokiona makaburini. Huyu Masanja lazima afanyiwe kitu.”

Wanawake walipiga kelele:

“Ndiyo! Tumeteseka vya kutosha!”

Wanaume walijibu:

“Tumfate. Huyu kijana lazima ajibu! na leo usiku lazima tukachome ofisi yake”

Wakati haya yote yakipangwa, Masanja hakuwa na habari. Alikuwa dukani kwake.

Habari hizi hazikufichika. Rafiki wa karibu wa Masanja, kijana mmoja aliyekuwa akikaa naye mara kwa mara, alisikia mpango huo. Usiku ule akampigia simu Masanja kwa haraka:

“Masanja, sikiliza vizuri. Watu wamepanga kesho kuvamia kibanda chako. Wamekasirika sana. Wanasema wewe mchawi, vibubu vyako vimeleta balaa. Kimbia Masanja, ondoka kabla hawajakupata!”

Masanja alinyamaza kwa muda, akashika kichwa kwa hofu. Sauti yake ikatetemeka:

“Kumbe… wameshaanza kujua?”

Asubuhi ilipofika, kijiji kizima kilikusanyika. Watu walikuja kutoka kila upande—wanawake, wanaume, vijana na wazee. Sauti zao zilikuwa kali, kila mtu akipaza hasira yake:

“Leo Masanja lazima atoe majibu!”

“Huyu ndiye ametugombanisha, ametumaliza!”

“Hatuwezi kuendelea kuibiwa na huyu mchawi masanja!”

Walielekea moja kwa moja kwenye kibanda cha useremala cha Masanja. Kibanda kilikuwa katikati ya kijiji, na ndani yake kulikuwa na vibubu vilivyopangwa vizuri, vingine vipya, vingine vikiwa tayari kwa wateja.

Mtu wa kwanza alichukua jiwe, akapiga ukuta wa mbao. Ukuta ukapasuka. Wengine wakachukua mawe, wakarusha. Ndani ya muda mfupi, kibanda kizima kilikuwa kimezingirwa.

wakawasha moto na kukichoma kibanda cha masanja.

Lakini wakati moto ukiwaka, Masanja hakuwepo tena. Rafiki yake alikuwa amemwambia aondoke, na kweli alitoroka usiku ule. Alikimbia bila kuaga mtu, bila kuchukua chochote.

Mara watu walipotambua hakuwepo, kelele zikawa kubwa zaidi:

“Amekimbia! Anajua kosa lake!”

“Hatutamruhusu arudi tena!”

Siku zikapita, na maisha yakaanza kurudi kawaida. Familia zilizokuwa zimegombana zilipatanishwa. Marafiki waliokuwa wamekosana walikumbatiana tena, wakikumbuka kuwa adui wa kweli wa kweli ni kibubu cha masanja

Masanja hakuwahi kuonekana tena. Wapo waliodai walimuona akielekea miji ya mbali, wengine wakasema huenda alikimbilia mkoa mwingine. Lakini ukweli mmoja ukabaki: hakurudi kijijini hapo tena.

Kijiji kikaapa: “Tusionunue tena kibubu kutoka kwa mtu tusiyemjua. Tumepata funzo. Uchawi unaweza kufichwa popote.”

Ndugu mtazamaji na msikilizaji , Ukitaka kununua au kutunza hela kwenye kibubu , tafadhali nenda kwa fundi mwambie atengeneze ukiwepo au tumia hata njia mbaala kutunza hela zako.

dunia sasa imebadilika.

unaweza tizama simulizi nyingine kwa kubonyeza hilo jina BONGO SIMULIZI. asanteni sana natukutane katika simulizi nyingine

26/12/2025

Utajiri wa nyoka ulivyomtokea puani kinana masalu baada ya kuvunja mashart ya mganga juu ya ndagu.

24/12/2025

Hoteli ya maajabu, hamna usafi hata kidogo part mwanzo mwisho.

23/12/2025

Pedi yenye damu ya hedhi ( period ya mwanamke ) ndio huwa wanatumia kufanya kafara. wanatoa kafara ya pedi ili wazidi kuwa matajiri

22/12/2025

Usinunue kibubu kutunzia pesa tena 🤬🤬. Fundi wa kutengeneza vibubu anatumia uchawi kuiba pesa ambazo wateja walionunua vibubu wake hutunza.

Address

Kalangalala

30101

Telephone

+255682711910

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Bongo Simulizi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Bongo Simulizi:

  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share