01/02/2026
https://youtu.be/A1RqYsQNDFY🎉 Maadhimisho ya Miaka 49 ya CCM – Wilayani Nyang’hwale 🎉
Karibu kwenye video yetu inayoonesha maadhimisho ya Miaka 49 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Nyang’hwale,Iliyoandaliwa na Jumuiya ya Wanawake Tanzani UWT (W).Nyang'hwale
Katika kuadhimisha sherehe hizi katika Wilaya,Mikoa na Taifa Lengo kuu la CCM ni kuonesha jamii mafanikio makubwa yaliyopatikana katika sekta mbalimbali kimaendeleo k**a vile Elimu, Afya, Maji na Miundombinu.chini ya DKT Samia Suluhu Hassan..........
📍 Elimu
✔️ Ujenzi wa shule za msingi na sekondari mpya
✔️ Kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi wanaopata elimu
✔️ Waraka wa elimu na vifaa vingi vya kufundishia
🏥 Afya
✔️ Zahanati na vituo vya afya vimejengwa au kuboreshwa
✔️ Upatikanaji wa huduma za msingi za afya umekua
✔️ Chanjo na huduma za mama na mtoto zimeimarika
💧 Maji Safi
✔️ Kupanua huduma ya maji safi vijijini
✔️ Visima vipya na miundombinu ya maji imewekwa
✔️ Jamii nyingi sasa zina huduma ya maji karibu na makazi
🚧 Miundombinu
✔️ Barabara zimeboreshwa/kujengwa
✔️ Daraja na vituo vya uchukuzi vimeimarika
✔️ Kuwekwa kwa miundombinu ya umeme na mawasiliano
AIDHA KUPITIA UONGOZI WA SERIKARI INAYOONGOZWA NA DKT SAMIA SULUHU HASSAN SEKTA ZOTE MUHIMU ZIMEBORESHWA NA KUIMARIKA KWA KIWANGO KIKUBWA MFANO:-
📚 Sekta ya Elimu
Kupitia serikali ya CCM, wilaya ya Nyang’hwale imeshuhudia ujenzi wa shule mpya nyingi zenye ubora wa kisasa za msingi na sekondari, madarasa yameongezwa, na vifaa vya kujifunzia vimeboreshwa. Hatua hizi zimeongeza upatikanaji wa elimu na kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto wetu,hali ambayo imeongeza ufaulu katika shule nyingi wilayani Nyang'hwale
🏥 Sekta ya Afya
Huduma za afya zimeimarika kwa kujengwa Hospitari kubwa ya WIlaya ikisheheni vifaa tiba kwa magonjwa mbali mbali k**a vile ,kuwepo kwa vipimo vya Ini,Figo,Moyo,Kinywa na Meno,sambamba na upasuaji mkubwa na mdogo kwa magonjwa mbalimbali,haya ni mafanikio makubwa kwa wilaya ya Nyang'hwale Pia kujengwa kwa vituo vya afya 5 vitano katika kata tofauti,pamoja Kibwa zaidi kwa sasa Vijiji vyote nyang'hwale kuna zahanati ya Kijiji. Wananchi sasa wanapata huduma bora za msingi karibu na makazi yao, ikiwemo huduma za mama na mtoto pamoja na chanjo.
💧 Sekta ya Maji
Upatikanaji wa maji safi na salama kupitia mradi wa maji mkubwa wa Iherere unaotoa maji kutoka ziwa Victoria umeongezeka kwa vijiji vingi nyang'hwale kwa maeneo machache ambayo bado jitihada zinafanyika kufikisha maji ya bomba kumechimbwa visima ambavyo vinasaidia kupunguza kero za upatikanaji wa maji hali ambayo inapunguza umbali na muda wa wananchi kutafuta maji,na kuienzi sera ya Rais Samia Suluhu Hassan ya KUMTUA NDOO MAMA KICHWANI
🚧 Miundombinu
Barabara zimeboreshwa, kwa kiasi kikubwa sasa vijiji vyote nyang'hwale vimeinganishwa na barabara za changarawe pia Rais Samia Suluhu Hassan sasa ametenga pesa kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya lami kutokea busisi mwanza,kupitia ngoma,busolwa,nyijundu,kharumwa ,chela,na Kahama hivyo miundombinu ya usafiri imeimarika, na huduma za umeme kwa sasa Vijiji vyote 62 vimefikiwa na Umeme na sasa umeme unasambazwa kwenye vitongoji na maeneo ya migodi (Wachimbaji Wadogo) Aidha sekta ya mawasiliano zimeendelea kupanuka kwa kuongeza minara katika vijiji mbalimbali hatua zinazochochea kukua kwa uchumi wa wananchi kwa ujumla.
HAYO NI KWA UCHACHE SANA ,MAMBO MAZURI YALIYOFANYWA NA CCM NI MENGI KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 49 TANGU KUZALIWA KWAKE....
Kwa pamoja, miaka 49 ya CCM ni miaka 49 ya maendeleo na matumaini mapya kwa wananchi wa Nyang'hwale na Tanzania kwa ujumla
✨ Tunaishukuru CCM kwa juhudi za maendeleo na ustawi wa wananchi wa wilaya ya Nyang’hwale.
📲 Usisahau subscribe, like na share video hii kwa maendeleo ya jamii yetu! 'HWALE TV ONLINE
🎉 Maadhimisho ya Miaka 49 ya CCM – Wilayani Nyang’hwale 🎉Karibu kwenye video yetu inayoonesha maadhimisho ya Miaka 49 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani...