Kanyamala Media

Kanyamala Media HABARI || MATUKIO || HAPA TANZANIA NA NJE YA TANZANIA
(2)

Jeshi la Akiba lilianzishwa mwaka 1965 k**a sehemu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Uanzishwaji wa Jeshi hili...
10/09/2026

Jeshi la Akiba lilianzishwa mwaka 1965 k**a sehemu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Uanzishwaji wa Jeshi hili una hadhi ya kisheria kupitia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu Na. 147 (1) (2), Reserve Force Act Na. 2 ya mwaka 1965 na sheria ya Ulinzi wa Taifa Na. 24 ya mwaka 1966 ibara ya 10. (1) (b) - (d). Jeshi hili liliundwa kwa lengo la kuandaa nguvu ya akiba kwa ajili ya kusaidiana na Jeshi la kudumu JWTZ na vyombo vingine vya usalama katika kudumisha Ulinzi na Usalama wa nchi yetu.

Shughuli za Jeshi la Akiba zilikuwa zikiratibiwa na Tawi la Jeshi la Akiba Makao Makuu ya Jeshi. Mwanzoni Tawi hili lilijulikana k**a Tawi la Mgambo. Mwaka 2010 kulifanyika mabadiliko ya Muundo Makao Makuu ya Jeshi ambapo Tawi la Mgambo lilibadilishwa jina na kuitwa Tawi la Jeshi la Akiba. Aidha, Halmashauri ya Majeshi ya Ulinzi katika kikao chake cha tarehe 16 Jul 13 ilijadili na kukubaliana uanzishwaji wa K**andi ya Jeshi la Akiba (KJA) “Reserve Forces Command” .

Waziri wa Ulinzi na JKT kwa Mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 10 (2) cha Sheria ya Ulinzi wa Taifa alianzisha K**andi ya Jeshi la Akiba tarehe 08 Disemba 2014.

DIRA: K**andi ya Jeshi la Akiba yenye Uwezo wa Kutekeleza dhana ya Ulinzi wa Taifa Kuwa Jukumu la kila Mtanzania (Umma).

DHIMA: Kuwa K**andi ya Jeshi la Akiba yenye Uwezo wa kuandaa nguvu ya akiba kwa ajili ya kusaidiana na Jeshi la Kudumu (Regular Force) na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama katika kudumisha Usalama wa Nchi yetu.

Zanzibar bado inaumwa; tena inaumwa ugonjwa unaoua hima (Terminal Disease) isipopata tiba makini, tiba yenye nguvu na kw...
10/09/2026

Zanzibar bado inaumwa; tena inaumwa ugonjwa unaoua hima (Terminal Disease) isipopata tiba makini, tiba yenye nguvu na kwa dozi kubwa.

Vipimo vya kitaaluma vinaonesha inasumbuliwa na mashetani, mizuka yenye kukalia kigoda cha mzimu wa watu wa kale. Mzimu huu unayumbisha Muungano wa Tanzania pia.

Juhudi za Serikali ya Muungano kutibu ugonjwa huu zimepwaya, kwamba badala ya kutibu ugonjwa wenyewe, mara nyingi zimeelekezwa kutibu dalili za ugonjwa pekee.

Mzimu wa ubaguzi kwa misingi ya rangi na uchama wa vyama mfu vya kale unaitafuna Zanzibar kwa kificho cha vyama vya siasa vya sasa – Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF) kwa staili ya mababu. Kwa vipi?.

Harakati za kisiasa za uhuru (modern independence struggles) Visiwani, ziliongozwa na vyama vikuu viwili: Zanzibar Nationalist Party (ZNP), kilichoundwa mwaka 1955; na Afro-Shirazi Party (ASP) kilichoanzishwa mwaka 1957.

Kipindi cha uchaguzi Mkuu wa mwisho, Julai 1963 kuelekea uhuru, kulijitokeza vyama viwili vibanzi (splinter parties) – Zanzibar and Pemba Peoples’ Party (ZPPP) cha waliojiengua kutoka ASP, na Chama cha Umma Party (UP) cha Abdulrahman Mohamed Babu na wenzake waliojiengua kutoka ZNP. UP hakikushiriki Uchaguzi Mkuu wa mwisho wa 1963, lakini kilishiriki kupanga na kuratibu kwa mafanikio, Mapinduzi ya Januari 12, 1964.

ZPPP na ZNP viliunda umoja (Ukawa) dhidi ya ASP na kushinda uchaguzi na hivyo kukabidhiwa serikali chini ya Waziri Mkuu Mohamed Shamte wa ZPPP. Siku 33 baadaye, serikali hiyo ilipinduliwa.

ASP ni muungano wa vyama viwili vya kijamii, “African Association” (AA) na “Shirazi Association” (SA), kufanya “Afro-Shirazi Party” (ASP).

Chama hiki kilijipambanua kuwa cha Waafrika zaidi, k**a ambavyo tu Chama cha “Tanganyika African National Union” – TANU cha Tanzania Bara kilicholeta uhuru wa nchi hiyo mwaka 1961, kilivyojipambanua mwanzoni, lakini kikajisahihisha haraka kuachana na ubaguzi na kuwa cha watu wa rangi zote. Mapinduzi ya 1964 yalikiweka ASP madarakani, chini ya Serikali ya Mapinduzi iliyoongozwa na Abeid Amani Karume wa ASP. Hapo ndipo ugonjwa unaoitesa Zanzibar hadi sasa ulipoanzia.

Kwa kuanzia, Wazanzibari wote waliokuwa wanachama wa ZNP/ZPPP na ndugu zao walihesabiwa k**a maadui wa Mapinduzi na kuvurumishwa nje ya Zanzibar, na waliobakia waliteswa kwa kutwezwa kwa ubaguzi mkubwa.

Mohamed Babu wa UP, aliyekuwa na asili ya Visiwa vya Ngazija, alitakiwa kuvunja Chama chake, naye akakubali ambapo yeye na baadhi ya vijana wake, kwa kutambuliwa mchango wao katika Mapinduzi ya 1964, walipewa Uwaziri katika Serikali ya Mapinduzi na baadaye katika Serikali ya Muungano.

Mwaka 1971, Karume aliwatuhumu Washirazi kuwa na asili ya Uarabu na hivyo kwamba Uzanzibari wao ulikuwa wa kutiliwa shaka nakuwataka waukane “Ushirazi”, vinginevyo waondoke Zanzibar. Washirazi walikuwepo Zanzibar kabla ya ukoloni wa Sultani mwaka 1828. Mmoja wa Viongozi wa SA, mwenye damu ya Kishirazi, Thabiti Kombo, alifanywa Katibu Mkuu wa ASP.

Kufuatia kifo cha Karume Aprili 7, 1972, mzimu wa ubaguzi ukakita kwa kishindo kikubwa zaidi. Kwanza, Wazanzibari wote waliokuwa wanachana wa ZNP, ZPPP na Umma Party na koo zao, walitiwa ndani ya kapu moja la mauaji ya Karume bila udadisi na hivyo kuitwa maadui wa Mapinduzi.

Kisha ikapitishwa amri kwamba, Wazanzibari wa kundi hilo wasipewe nafasi za uongozi Visiwani, wala kuruhusiwa kujiunga na Jeshi la Ulinzi na Polisi.

Pili, Zanzibar ilifanywa kuwa ya Wazanzibari weusi; suriama (chotara) na wahamiaji wengine wa rangi tofauti, bila kujali walifika lini Zanzibar, hawakustahili kuitwa Wazanzibari.

Ubaguzi huu na manyanyaso yalikuwa yalisimamiwa na Serikali ya Mapinduzi chini ya Usimamizi wa kundi katili, maarufu k**a “Genge la watu 14” – (the Gang of fourteen), likiongozwa na Kanali Seif Bakari wa idara ya Usalama Zanzibar.

Hata pale Tanganyika na Zanzibar zilipoungana mwaka 1964, ubaguzi huu uliendelea kwa chukizo kubwa kwa Mwalimu Nyerere, ukifanywa kwa jina la Serikali ya Mapinduzi chini ya ASP kilichokuwa juu ya Serikali ya Muungano; Karume akageuka kuwa mwiba kwa Mwalimu.

Ili kukomesha ukatili na ubaguzi huu, mwaka 1976, Mwalimu Nyerere (TANU) alibuni Muungano wa Vyama vya TANU na ASP (k**a alivyobuni mapema Muungano wa nchi hizo mbili) kwa madhumuni ya kudhibiti maovu ya Zanzibar ndani ya Jamhuri ya Muungano, ili chaka la hayo yote (ASP) liweze kudhibitiwa na chama kipya chenye kushika hatamu za uongozi wa Jamhuri ya Muungano, Zanzibar ikiwa ndani.

Wazo hili lilipingwa vikali na Wahafidhina wa siasa za ubaguzi visiwani kiasi cha Rais wa Zanzibar wa wakati huo, Aboud Jumbe, kulazimishwa aachane na “Mbinu za Nyerere” za kutaka “Kuimeza” Zanzibar akatoa sababu za kutaka muda zaidi kufikiria.

Lakini baada ya vuta nikuvute, na kwa tishio la kuvunja Muungano, wahafidhina hao, waliojiita “Wakombozi” (Liberators), walikubali ASP na TANUviungane, lakini kwa masharti.

Sharti la kwanzalilikuwa kwamba, jina la Chama kipya lisiwe kwa lugha ya Kiingereza ili kutowakumbusha Wazanzibari enzi za ukoloni wa Mwingereza Visiwani; la pili, kwamba neno “Mapinduzi” lionekane na kusomeka bayana ndani ya jina la Chama kipya ili kutopoteza historia ya Mapinduzi ya 1964. Tatu, tarehe ya kuzaliwa kwa Chama kipya ioane na tarehe ya kuasisiwa kwa ASP na kwamba angalau tarakimu moja ya mwaka 1957 ionekane pia.

Potelea mbali, TANU ya Nyerere haikupoteza muda kwa hayo; ikakubali jina la Chama liwe “Chama cha Mapinduzi” (CCM) bila tafsiri ya Kizungu ambapo kingeitwa “Revolutionary Party of Tanzania” – RPT na ikakubalika kianzishwe Februari 5, 1977, tarehe ya kuasisiwa ASP, 5 Februari 1957.

Kisha, CCM kikatangaza kushika hatamu za uongozi hivi kwamba kiongozi yeyote aliyekwenda kinyume na maagizo ya Chama, alikwenda kinyume na Muungano na hivyo mhaini, Mzanzibari kwa Mtanzania Bara.

Kwa hatua hiyo, wahafidhina wa siasa za ubaguzi na ukatili Visiwani walivurumishwa; Baraza la Mapinduzi na “The Gang of 14” lik**alizwa nguvu kwa nafasi yake kuchukuliwa na Baraza la Wawakilishi; demokrasia ikamea Zanzibar.

Ukuu wa Chama (Party Supremacy), ndio uliomng’oa madarakani Rais wa awamu ya pili Visiwani, Aboud Jumbe, alipojaribu kuungana na Wahafidhina wa siasa za chuki, kuhoji uhalali wa Muungano, mwaka 1984.

Kurejea kwa mfumo wa demokrasia ya vyama vingi nchini mwaka 1992, kulifufua ubaguzi na chuki kwa misingi ile ile ya vyama vya kale kufanya Zanzibar kumeguka vipande vipande.

Kwamba wale ambao walitaka mabadiliko kwa kuona Zanzibar mpya (wanajiita “Frontliners”) na ambao hawako tayari hadi leo kuishi kwa “legacy” ya ukatili na ubaguzi wa kitabaka wa miaka 1950/1960, wanahesabiwa kuwa si Wazanzibari wa kweli na kuchukuliwa k**a maadui wa Mapinduzi.

Baadhi ya waliojaribu kufanya hivyo mwaka 1986, akiwamo Kada wa CCM wa zamani na kipenzi cha Mwalimu Nyerere, aliyesaidia kung’olewa madarakani kwa Jumbe, Maalim Seif Sharrif Hamad; walifukuzwa uanachama wa CCM kwa kusaliti Mapinduzi.

Wengine waliofukuzwa pamoja na Hamad ni Shaaban Mloo, Ali Haji Pandu, Khatib Hassan, Soud Yusuf Mgeni, Hamad Rashid na mwingine mmoja.

Kufukuzwa kwa kundi hili, maarufu k**a “The Magnificent Seven” (Waadhimu Saba), kulifanya waungane na kuanzisha upinzani kwa mwavuli wa “K**ati ya Mwelekeo wa Vyama Huru” – “KAMAHURU”, iliyozaa Chama cha “Zanzibar United Front” [ZUF] mwaka 1992. Baadaye ZUF kiliungana na “Chama cha Wananchi” (CCW) cha Bara, kuunda Chama cha kitaifa cha sasa – “Civil United Front” (Chama cha Wananchi) – CUF.

Vyama hivi viwili, CCM na CUF vikawa na nguvu sawa Visiwani kiasi kwamba hakuna aliyekuwa na uhakika wa ushindi kwa chaguzi zote. Kwa wahafidhina wa siasa za kale Visiwani, ASP hakijafa, Bado kinaishi ndani ya kivuli cha CCM na vivyo hivyo Baraza la Mapinduzi na nadharia zake.

Kwa wahafidhina hao, Chama chochote cha upinzani kwa CCM ni cha upinzani kwa ASP mfu na Baraza la Mapinduzi, “Upinzani” wenye kuibua hisia za mzuka wa ZNP na ZPPP za kujitakia.

Wakati CCM Zanzibar kinaishi kwa hofu ya mzimu wa watu wa kale, CCM Bara kinasumbuliwa na hofu itokanayo na Katiba shaghalabagala ya Muungano, inayozua maswali mengi kuliko majibu k**a vile Je, iwapo, kwa mfano, CUF ingeshinda uchaguzi Zanzibar na Marehemu Seif Sharrif Hamad na angekuwa Rais wa Zanzibar, na Hayati John Pombe Magufuli wa CCM k**a Rais wa Tanzania, Hali ya kisiasa ingekuwaje kwa vyama hivi viwili tofauti kutawala sehemu mbili tofauti za Tanzania?.

Kwa kuwa Rais wa Zanzibar ni Mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Serikali ya Muungano (Angalia Katiba, - ibara 54 (1) ambalo wajumbe wake ni pamoja na Rais wa Muungano, hali ingekuwaje k**a Seif Sharrif Hamad kutoka CUF angekuwa mjumbe wa Baraza hilo? Je, lingeweza kufanya kazi ipasavyo?, wakahoji.

Kwa kuwa Baraza la Mawaziri linawajibika kwa Bunge la Muungano na kwa Rais katika ujumla wake, Je, Hamad naye angewajibika kwa Bunge hilo na kwa Rais wa Chama tawala Tanzania? Je, angewajibika pia kutekeleza uamuzi wa Baraza hilo la Mawaziri nchini Zanzibar..? K**a nani..??

Rais wa Zanzibar kuwa Mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Muungano kulitokana na hofu nyingine kubwa zaidi, juu ya uwezekano wa Hamad kuwa Rais wa Zanzibar na hivyo kuwa Makamu wa Rais wa Muungano, jambo ambalo halikuingia kichwani mwa CCM.

Hivyo, haraka haraka ikateuliwa Tume ya Jaji Mark Bomani mwaka 1994, kupendekeza marekebisho ya Katiba k**a ilivyo sasa kwa kukiuka mmoja wa misingi ya Muungano, k**a inavyofafanuliwa kwenye Mkataba wa Muungano [Articles of Union] wa mwaka 1964.

Tatizo ni upungufu katika Katiba ambao umeandikwa kana kwamba hapana uwezekano wa sehemu mbili za Tanzania kutawaliwa na vyama viwili tofauti, licha ya kufungua milango kwa mfumo wa demokrasia ya vyama vingi. Inapofikia hapo, hofu ya wahafidhina wa siasa za ubaguzi Visiwani na hofu ya wenye uchu wa madaraka Bara, zinaungana kwa kivuli cha CCM kubaka demokrasia na umoja wa kitaifa kwa kusigina Katiba na Sheria tulizozitunga wenyewe.

Sheria zinazotakiwa kuzingatiwa na kuheshimiwa ni Katiba ya Zanzibar, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria ya Uchaguzi Zanzibar, na kwa Wasimamizi wake kujiepusha na ushabiki wa vyama vya siasa.

Historia ya Zanzibar inaonesha kwamba, umwagaji damu wote uliowahi kutokea Visiwani ulitokana na machafuko yaliyosababishwa na chaguzi kuu zisizokuwa huru na za haki. Kwa mfano, uchaguzi wa kwanza, uliofanyika Januari 1961 haukutoa mshindi kati ya ASP na ZNP; ghasia zikazuka na watu kadhaa kuuawa na wengine kujeruhiwa.

Hata hivyo, chuki na uhasama wa kisiasa enzi hizo haukuwa mkubwa k**a ilivyo sasa; wanasiasa waliongozwa na azma moja ya kuipatia nchi uhuru kutoka kwa Waingereza bila kuingiza ubaguzi wa aina yoyote miongoni mwa Wazanzibari. Ndiyo maana, baada ya Vyama vyote kukosa ushindi katika uchaguzi wa Januari 1961, iliundwa serikali ya mseto ya mpito ya vyama vya ASP, na ZNP/ZPPP kuelekea uchaguzi mwingine uliopangwa kufanyika Juni 1961.

Kabla ya uchaguzi huo, Karume alimwomba Kiongozi wa Chama cha ZPPP, Mohamed Shamte waunganishe vyama vyao (ASP na ZPPP) ili kukipiku, lakini Shamte alikataa.

Juni 1961 ilipowadia, ZNP na ZPPP viliunda mseto dhidi ya ASP; ghasia kubwa zikazuka, huku kila upande ukimtuhumu mwenzake kupinda kanuni za uchaguzi. Katika ghasia hizo, watu 70 waliuawa, 400 walijeruhiwa na wengine 1,002 kutiwa mahabusu na Serikali ya Uingereza. Hapo ndipo uhasama mkali wa kisiasa ambao umedumu hadi leo uliposhika kasi.

Uchaguzi wa tatu na wa mwisho kabla ya uhuru uliofanyika Julai 1963 ulilalamikiwa na Chama cha ASP kwamba haukuwa huru na wa haki. Hata hivyo, Karume aliamua kutupa karata yake ya mwisho kwa kutaka kuundwe Serikali ya Umoja wa Kitaifa kati ya ZNP/ZPPP na ASP ili kumaliza manung’uniko na uhasama wa kivyama.

Aliwatuma Viongozi wawili waandamizi wa ASP – Othman Sharrif na Hasnu Makame, kumwomba Shamte akubali kuundwa kwa serikali hiyo, ambapo Shamte angeongoza serikali akiwa na uhuru kamili wa kuteua mawaziri kutoka ZNP, ZPPP na ASP. Kwa mara ya pili, Shamte alikataa katakata na badala yake akashauri ASP kivunjwe na wanachama wake wajiunge na ZNP/ZPPP.

Sote tunafahamu kilichotokea; Serikali ya Shamte ilipinduliwa katika Mapinduzi ya umwagaji damu, yaliyopangwa na kuongozwa na vijana wenye itikadi za Kisoshalisti wa vyama vya ASP na UMMA, Januari 12, 1964. Siku 100 baadaye tangu Mapinduzi hayo kufanyika, Zanzibar na Tanganyika ziliungana kuunda Tanzania.

Wazanzibari bado wanabaguana kwa misingi ya vyama vya siasa hai na mfu, rangi na kwa nasaba za koo zao ubaguzi ambao haupo Tanzania Bara. Haya yote ni ishara ya kuzorota kwa umoja wa kitaifa na chanzo cha ghasia. CUF Zanzibar kilikuwa kinahesabiwa kuchukua nafasi ya ZNP/ZPPP kabla la ujio wa ACT-WAZALENDO na CCM Zanzibar nafasi ya ASP.

Tunayoshuhudia sasa ni vituko vya uhuru vinavyofanywa na Wazanzibari waliochoka na hali ya amani. Kwa nini hatujifunzi kutoka Darfur, Sudani, Rwanda na Burundi na kwingineko kwa yanayotokea Visiwani.

Mzee Karume hakukosea alipowataka wapinzani wake kuunda serikali ya mseto mwaka 1961 na 1963 k**a njia ya kumaliza mgogoro na pale waliposhindwa kumsikiliza, ghasia ziliendelea kuitafuna nchi hadi Mapinduzi.

Kwa hali ilivyo Visiwani Zanzibar, kuna kila dalili kuonesha kwamba historia inaweza kujirudia k**a nguvu za CCM na CUF Baadae ACT-WAZALENDO hazitaweza kushabihishwa (harmonize) ziweze kutumika kwa maendeleo ya Wazanzibari.

Ushabiki na unafiki wa kisiasa unaochochewa na maswali magumu tuliyoyataja mwanzo hautalifikisha mbali taifa hili, badala yake utaliangamiza. Ilivyo, sasa Zanzibar inaumwa; tena ni mahututi kitandani.

Kauli tata na hasi za baadhi ya viongozi kwamba “Uhuru wa Zanzibar hauwezi kukabidhiwa kwa yeyote kwa njia ya sanduku la kura”; au kwamba, “k**a lolotelisilotarajiwa (kushindwa uchaguzi) litatokea, tuko tayari kutumia silaha za Mapinduzi ya 1964 kwani CCM Zanzibar wanazo funguo za sanduku la silaha hizo”, zinachochea chuki na kuvuruga umoja wa kitaifa Zanzibar na kuzua tufani kwa Muungano pia.

Kiongozi bora ni yule anayeweza kuchukua hatua, hata k**a hatua hizo hazitakuwa za manufaa kwa Chama chake cha siasa, mradi tu ni za manufaa kwa nchi nzima; au kuchukua hatua zinazogongana na matakwa ya wengi kwenye Chama chake, lakini ni hatua sahihi kwa nchi. Hapa iwe ni nchi kwanza, siasa baadaye.

Inatosha kwa leo..Tuulinde Muungano wetu kwa uwivu sana✍️🏿

Je, Rais wa Sudani Kisini Salva Kiir anaiga mtindo wa uongozi wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, nchini Sudan Kusini..?...
09/09/2026

Je, Rais wa Sudani Kisini Salva Kiir anaiga mtindo wa uongozi wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, nchini Sudan Kusini..???

Je, unafikiri k**anda mpya wa Divisheni ya Tiger, Atem Salva Kiir, anaweza kuwa Mkuu ajaye wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Sudan Kusini (SSPDF).???

T**i Mohammed Salum Mandangwa kazaliwa katika familia ya dini haswaa, lakini kapita vikwazo vingi. Amezaliwa 1926, Dar e...
09/09/2026

T**i Mohammed Salum Mandangwa kazaliwa katika familia ya dini haswaa, lakini kapita vikwazo vingi. Amezaliwa 1926, Dar es Salaam na kufariki Johannesburg, RSA katika hospitali ya Net Care, Novemba 5, 2000. Aliishi miaka 74 ya machozi, jasho na damu.

Alizaliwa kwa jina la T**i Mohammed Salum Mandangwa maarufu "Bibi T**i Mohammed". Baba yake aliitwa Bw. MOHAMED BIN SALIM na mama yake aliitwa Bi. HADIJA BINTI SALIM. Wazazi hawa walitokea Rufiji. Baba yake alikuwa mfanyabiashara ya mbuzi na ng'ombe na mama yake alikuwa mkulima.

Baba aligoma T**I asipelekwe shule. alikataa T**I asisome shule kwa hofu angekuwa kafiri. Mama yake T**I alimpeleka shule baadae. Baba yake alifariki T**I akiwa na miaka 9 tu. Mamaye akatumia fursa hiyo kumpeleka T**I Shule ya Wasichana Uhuru ambako alisoma hadi darasa la 4

T**I aliolewa na mwanaume mzee ambaye angeweza hata kuwa baba yake wakati yeye akiwa binti wa miaka 14 tu. Bibi aliolewa na mtu mzima, T**i akiwa na miaka 14 tu. T**I aliolewa na mwanaume mzee ambaye angeweza hata kuwa baba yake wakati yeye akiwa binti wa miaka 14 tu.

T**I alijifungua mtoto wa k**e aitwae HALI ambaye alikuja kuolewa na MZEE IDD HAMIS, Mshambuliaji hatari wa zamani wa Cosmopolitans, klabu ya kwanza kutwaa ubingwa Tanzania ambapo walikuwa wakiishi mtaa wa Sikukuu na Udowe na kubahatika kupata watoto 3 wa kiume.

Baadae, T**I aliachana na mume huyo kijeba ambaye alikuwa ni baba wa HALIMA , mume ambaye hakuwa chaguo lake. T**I alianza kuwa maarufu angali mdogo alipokuwa kiongozi wa ngoma za maulid ambazo zilimjenga uwezo wa kujiamini na hivyo akawa maarufu sana.

T**I aliolewa na dereva wa teksi aitwae Boi Selemani, baada ya ndoa yake ya kwanza kusambaratika. BOI, alikuwa ni rafiki wa SCHNEIDER PLANTAN aliyekuwa mmoja wa viongozi wa TAA, Bw. PLANTAN alienda nyumbani kwa BOI na kumweleza kuwa ametumwa kumweleza T**I ajiunge na TANU

BOI alikubali na akajinunulia kadi na.15 ya TANU na pia akamnunulia T**I kadi na.16. Jumla alitoa TZS 12/= kwani kila kadi iliuzwa TZS 6/=.Ndivyo walivyojiunga TANU. BOI pia alichangia TSH 10/= kwa ajili ya nauli ya Mwalimu NYERERE kwenda UNO (TSH 5/= kila mmoja).

TANU ilizaliwa tarehe 7.7.1954. Wanachama wa mwanzo kupata kadi za TANU walikuwa NYERERE (Kadi na.1), A. SYKES Na.2, A. SYSKES No.3 D. AZZIZ No.4, DENIS PHOMBEAH No.5, DOME OKOCH Na.6, J. RUPIA Na.7

Bibi T**i Mohammed alikutanishwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere 1954, wakafanikiwa kuwa marafiki wa kudumu (ingawa baadae walikuja kuwa na uadui wa kisiasa, usiokuwa na uwazi) na uadui ambao ulimfikisha Bibi T**i Mohammed magereza kwa makosa ya uhaini dhidi ya serikali

Bibi T**i Mohammed hakuwepo wakati wa TAA au TANU ya mwanzo. aliletwa baadae na kukutana na Nyerere, 1954/55 na dereva Taxi aliyejuana na shemeji wa Bibi T**i, ingawa katika pekenyua yangu nimekutana na jina la Schneider Plantan (k**a mtu aliyemshawishi kujiunga na TANU).

Boi aliwahi kumlalamikia Schneider kuwa mkewe Bi. T**i hatulii nyumbani kwa ajili ya shughuli za TANU kiasi imekuwa yeye ndiyo mfuaji wa nguo zake na mpishi wa chakula chake. Boi Selemani alikuwa dereva wa taxi. Schneider ana historia kubwa pia kwa historia ya siasa za TANU

Kuna wakati Boi (mumewe Bibi T**i Mohammed) alilalamika kwa Schneider Plantan hadi kusema, "T**I ni mwanamke wa kiislam, kasoma madrasa, kapanda jukwaani bila baibui. Hii si sawa kabisa".. Picha hii ni viwanja vya Jangwani 1955 Nyerere akijianda kwenda UNO (Umoja wa Mataifa)

Schneider Plantan ndiye aliyesimama kidete kuwaleta vijana wasomi katika chama cha TAA ili kuwaondoa wazee wa mwanzo waliokuwa wamechoka na kuifanya TAA isifanye siasa za maana za harakati kwa ajili ya ukombozi wa Tanganyika. Hii ilikuwa mwaka wa 1950.

Sasa TANU ilipokuja kuasisiwa mwaka wa 1954 Schneider ndiye aliyemleta Bi. T**i Mohammed katika TANU pamoja na wenzake akina Tatu Binti Mzee na wanawake wengine ili kuipa nguvu TANU mbele ya makundi ya wanawake waliokuwa nyuma wakati huo.

Mwaka 1955 wakati safari ya Nyerere kwenda UNO inatayarishwa ugomvi wa Boi na Bibi T**i ulipamba moto. Boi akimlaumu Schneider kwa kumuingiza mkewe kwenye siasa na harakati za kudai uhuru. Bi. T**i na wenzake wako katika hekaheka ya kuhamasisha wananchi kujiunga na TANU

“BOI mwenyewe ndie aliyeniruhusu kujiunga na TANU na tena ndiye aliyeninunulia kadi ya uanachama. TANU pia ilimwandikia barua anisaidue mambo ya TANU.Lakini mwisho hizi safari zilimshinda. Nilikuwa nakaa nje ya DSM hata kwa miezi 3 na nikirudi sikai hata siku 10, nasafiri tena”

“BOI akaniambia anataka kuoa mke mwingine. Nikamwambia sawa, niache na kazi yangu kwani nimeizoea. Kwahiyo BOI akamuoa Bi. KHADIJA lakini wakashindwana wakaachana. Nilifunga mizigo yangu nikaondoka kwa BOI”. Anasema T**I baada ya ndoa yake na Boi kuparanganyika

Baadae sana, Nyerere alivutiwa na T**i, akapewa kadi namba 16. Nyerere alikuwa na kadi namba 1 na Boi Selemani alipewa kadi namba 15. Kulia ni Bi. T**i Mohamed, Clement Mtamila, Sheikh Suleiman Takadir, Mwl Nyerere na nyuma ya Nyerere ni Maria Nyerere, Rajab Diwani na John Rupia

Mapambano yote ya wanawake wa TANU katika kudai uhuru wa Tanganyika wakati huo wakiongozwa na Bibi T**i Mohammed yalikuwa yakifanyika kwa kuanzia katika ofisi za Lumumba (ambazo sasa CCM wamejimilikisha k**a jengo lao na kuziita ofisi ndogo za CCM). Zilijengwa kwa nguvu ya umma

Mwaka 1955 (baada ya kujiunga na TANU na kuwa mwanachama kamili), Nyerere na Bibi T**i Mohammed walifanya mkutano mkubwa wa hadhara Tabora. Walipata mwaliko kutoka kwa watu wa Tabora, Kumbuka kuwa Tabora ya wakati huo ilikuwa na hamasa kubwa katika harakati za kudai uhuru.

T**I ndiye aliyekuwa akiimbisha na kuhutubia kwanza kabla ya NYERERE kupanda jukwaani “kushusha” nondo. Kwa hakika, T**I alikuwa akikonga nyoyo kwa kiswahili chake cha pwani na nyimbo zake: (Hongera mwanangu eeh na mi nihongere eeh hongera X 2) na (Mama Usungu, Mama Usungu X 2).

Baada ya kufahamiana na Mwalimu Nyerere, Bibi T**i Mohammed alipewa uongozi katika Women Wing ya TANU ambapo alishiriki katika kuhamasisha wanawake kuunga mkono harakati za TANU za kudai uhuru. Aliongoza makongamano, mihadhara na harakati za nyumba kwa nyumba kuhamasisha

Tarehe 8.7.1955, T**I binti Mohammed akiwa Mwenyekiti wa Tawi la Wanawake wa TANU, alifanya mkutano mkubwa na kuvuna wanachama 400 na ndani ya miezi 3 tu akawa amepata wanachama 5,000: Bibi anasema kwa kauli yake;

“Nilizunguka Tanganyika nzima. tulienda Tanga tarehe 1.1.1956 na Bwana mkubwa na RAJAB DIWANI tukazunguka siku 21. K**ati Kuu ikanipa ruhusa ya kusafiri peke yangu. Pia nilifanya safari nyingi na OSCAR KAMBONA. Tukiwa na KAMBONA tulikuwa tukipita nyumba hadi nyumba, usiku na mchana”

Mwaka 1957, pale kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, mbele ya mgeni kutoka chama cha LABOUR cha Uingereza, Bibi T**i alipewa nafasi ya kuhutubia mkutano wa TANU wakati Nyerere akiwa Butiama mapumzikoni kwa mama yake. Nyakati hizo siasa haikuonekana k**a ni shughuli ya wanawake, wao walitakiwa kubaki nyumbani tu.

Bibi T**i akihutubia akinyoosha vidole kwa wanaume aliwaeleza wanawake wenzake “wanawake amkeni. Tokeni majumbani tupambane pamoja na wanaume mpaka uhuru ipatikane. Msiogope. Msiogope. Msiogope”

“Mnawaona hawa? Basi wafanye watakavyofanya hawa, pamoja na hao wengine wote wanaowatisha Duniani, wametoka katika matumbo ya wanawake na waliishi humo miezi tisa.. kila mmoja kanyonya ziwa la mama yake miaka miwili.. sasa tujitokeze wasituahinde hawa”

“Kutawaliwa siyo kuzuri ndugu zangu, hili ni letu sote siyo la wanaume pekee yao, njooni akina dada, njooni akina mama na vikongwe pia.”

Aliunguruma Bibi T**i Salum Mohammed Mandangwa jukwaani huku zikisikika kelele za vifijo na nderemo, hoihoi na vigelegele.

Kutoka hapo jina la Bibi T**i ndiyo likawa habari ya mji wote. Habari zake zikazagaa hadi Afrika ya Mashariki yote. Wanawake wengi sana wakajitokeza na kujiunga na TANU na harakati zake. Msibani, harusini, nyumbani habari ikawa “T**I, T**I, T**I, T**I”

Wapigania uhuru wa Kenya wakati huo akiwepo Tom Mboya, Jaramogi Oginga Odinga, wakaleta maombi Tanganyika, Hibi T**i aende Kenya kuwasaidia kushawishi serikali ya Uingereza kumtoa kifungoni Mzee Jomo Kenyatta aliyefungwa kwa kosa la uhaini (kudai uhuru).

Bibi T**i akaenda zake hadi Kenya. Akatoa fora katika mikutano yake ya Mombasa, Kisumu, Machakos na Nairobi. T**i jukwaani alikuwa akivalia mini-skirts sawa na wanawake wa Kenya, akilia kwa uchungu na kulitaja jina la Kenyatta awe huru lakini mwisho wa ujumbe wake akiwataka wanawake wampiganie Kenyatta watoke ndani.

Haikupita kitambo kirefu, Mzee Jomo Kenyatta aliachiwa huru na safari yake ya kwanza alisafiri hadi Tanzania na kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam na muda mwingi alimshukuru Bibi T**i Mohammed.

Katika mkutano huo Nyerere alisema yupo tayari kuhairisha uhuru wa Tanganyika (ambao tayari ulikuwa umejulikana) ili tusubiri Kenya wapate uhuru wao nchi ziungane kuwa moja na Kenyatta awe Rais wake.

Tamko zito sana ambalo bila shaka lilitokana na kazi ya Bibi T**i. Uhuru uhairishwe na Rais awe mtu mwingine kutoka Kenya? Mwalimu Nyerere aliipenda sana Afrika, alitamani muungano wa Afrika sawa na muungano wa Marekani moja. Taifa lenye nguvu kiuchumi.

Baada ya uhuru kupatikana Bibi T**i alipata ubunge Rufiji na akateuliwa kuwa waziri mdogo wa utamaduni na maendeleo. T**I akapeleka hoja ya KISWAHILI Kutumika Bungeni: T**I alikuwa ameishia darasa la 4 tu hivyo alikuwa hawezi “kutema yai” kwa ufasaha. Siku moja mwanzoni mwa 1960s akiwa bungeni akatoa hoja kwamba wananchi wa Magomeni wanataka nao wawe na taa za barabarani ambapo alisema

“We want fire in Magomeni.... We want fire in small bottles”. Maneno ya Bibi T**i. Wabunge walicheka pamoja na NYERERE akiwa Waziri Mkuu ambapo aliamuru KISWAHILI kianze kutumika bungeni.

Bibi T**i Mohammed alikuwa pia mwenyekiti wa UWT na EAMWS tawi la Tanganyika. Mjumbe wa tume ya Maulid (k**ati ndogo ya kuandaa Maulid kila mwaka), Mwenyekiti wa k**ati akiwa Tewa Said Tewa (mbunge wa Kisarawe) na katibu akiwa Chifu Abdallah Said Fundikira (aliyekuwa waziri wa sheria). Wakapata kiwanja kikubwa Chang’ombe kwa ajili ya ujenzi wa chuo kikuu (kabla hata UDSM haijapata eneo).

Nyerere alialikwa kuweka jiwe la msingi. Nyerere na serikali yake hawakupendezwa na jambo hilo. Mradi ulikuwa unafadhiliwa na Rais wa Misri, Gamal Abdel Nasser Hussein. Serikali ikasimamisha mradi na kuvunja kabisa EAMWS na kuundwa baraza lingine kwa ajili ya waislam.

Mwalimu Nyerere na wenzake ndani ya TANU, pamoja na kukataa ubaguzi kwa kukubali kuwapokea na kuwapigia kura wahindi kwenye mpango wa kura tatu, kwenye hili la uislam - wahindi hawakutakiwa wasaidie waislam na hapo ikavunjwa EAMWS kwa amri ya serikali likaundwa BAKWATA la waafrika watupu kutoka Sunni.

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1965 Bibi T**i Mohammed na Tewa (Tewa Said Tewa alikuwa Rais wa jumuiya ya EAMWS) wakapoteza viti vyao ndani ya TANU na serikalini. Aliyekuwa katibu, chifu Abdallah Fundikira akapelekwa Nairobi kuwa mwenyekiti wa shirika la ndege la jumuiya ya Afrika Mashariki (EAAC).

Ndani ya halmashauri kuu ya Taifa ya TANU, Bibi T**i alipambana na kuwabwaga wanasiasa wakongwe kwa hoja nzito pale mjadala wa kuivunja EAMWS ulipokuwa unajadiliwa. Mwaka 1968, Bibi T**i Mohammed alik**atwa na kuhusishwa na tukio la uhaini (ni hadithi nyingine ndefu)

Mwaka 1967, T**I, bila kupepesa macho wala kutikisa pua, akabwaga manyanga na kujiuzulu ujumbe wa K**ati Kuu ya TANU kwani alikuwa hakubaliani na Kipengele cha 5(a) cha Azimio la Arusha kuhusu maadili kwamba ni marufuku kiongozi wa serikali au TANU kuwa na nyumba ya kupangisha.

Safari hii ya pili Bi. T**i Mohammed na Tewa Said Tewa walikwenda Msasani kumuona Mwalimu Nyerere kumuuliza kwa nini anaachia vyombo vya dola vinapiga vita East African Muslim Welfare Society (EAMWS).. Hii ilikuwa mwaka wa 1968 katikati ya kile kilichokuja kujulikana k**a “mgogoro wa EAMWS.”

T**I alikuwa na nyumba 2 ambapo moja aliijenga kwa kuuza vito vyake vya dhahabu na nyingine ni ya mkopo. Nyumba moja ipo Upanga mkabala na Makao Makuu, JWTZ na nyingine ipo Temeke. Uhusiano wa NYERERE na T**I ukawa umelegalega baada ya kumkosoa Nyerere kwenye azimio la Arusha.

Oktoba ya mwaka 1969, Bibi T**i Mohammed na aliyekuwa waziri wa kazi wakati huo, Michael K**aliza walik**atwa, pamoja na maafisa wa jeshi wengine wapatao wanne na kufanya idadi ya waliok**atwa kufikia 7, wakituhumiwa kwa kupanga njama za kuipindua serikali iliyokuwa madarakani.

T**I alikuwa ni mwanamke pekee katika kesi hiyo. Walidaiwa kupanga kutekeleza azma hiyo wakati Rais NYERERE atakapokuwa nje ya nchi. Kesi ilianza kurindima 6.6.1970 chini ya Jaji Mkuu, Georges, CJ na upande wa mashtaka ukiongozwa na MARK BOMANI.

Washtakiwa wengine katika shtaka hilo la uhaini walikuwa ni Gray Likungu Mattaka, John Dustan Lifa Chipaka, Michael Marshal Mowbrya, William Makori Chacha na Alfred Philip Millinga. Wote kwa pamoja walishtakiwa kwa tuhuma za kupanga njama kumpindua Rais Nyerere

JUMAMOSI ya Agosti 1, 1970 Mahak**a Kuu ya Tanzania iliambiwa na mkurugenzi wa mash*taka ni jinsi gani Bibi T**i Mohammed alivyogharamia mapinduzi ya kumuua Julius Nyerere na kuiangusha serikali yake (jaribio la kimapinduzi dhidi ya serikali iliyokuwa madarakani)

Kesi ilinguruma kwa siku (127). T**I na wenzake kasoro Bw. MILLINGA walitiwa hatiani kutokana na ushahidi madhubuti na kupewa kifungo cha maisha. T**I akaenda kutumikia kifungo gereza la Isanga, Dodoma.

Bi. T**i akiwa Gereza la Isanga Dodoma, moja ya magereza magumu. Kabla yake mwaka wa 1953 mwanasiasa mkubwa sana Tanganyika sehemu za Maziwa Makuu, Ali Migeyo alifungwa gereza hilo na wakoloni wa kiingereza kwa kosa la kufanya mkutano wa siasa K**achumu bila idhini ya serikali

Miaka 17 baadae, mpigania uhuru Bibi. T**i Mohammed nae anajikuta kifungoni kwa kuhusika na kesi ya uhaini katika jaribio la kutaka kuipindua na kuiondoa madarakani serikali ya Mwalimu Nyerere aliyoipigania wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika kutoka kwa wakoloni.

Akiwa hapo gerezani Bi. T**i anaandika historia ya uhuru wa Tanganyika na anaeleza ushirikiano wake na Nyerere wakati wakiwa katika ofisi ya TANU New Street. Bibi T**i anaeleza katika muswada wake, anaoandika jela jinsi yeye na wenzake walipita mtaa kwa mtaa kueneza TANU.

Baada ya T**I kukumbwa na dhahama ya kesi ya uhaini, mumewe akaamua kumuacha aliona hiyo ni fedheha kubwa isiyovumilika kwenye jamii! Nyumba 2 za Bibi T**I Zataifishwa: Wakati akiwa anatumikia kifungo chake cha maisha, serikali ikataifisha nyumba zake mbili zilizotajwa hapo juu

Baada ya kuhukumiwa kwenda jela kwa kosa la uhaini, Bibi T**i Mohammed aliamua kukata rufaa yake katika mahak**a ya rufaa Afrika Mashariki - Court of Appeal for Eastern Africa (iliyokuwa chini ya East Africa Community, ile jumuiya ya zamani), rufaa ambayo nayo ilishindikana pia.

Mwanamama mmoja mwanasiasa machachari wa Kenya baada ya kupata habari za T**I kufungwa maisha alikuja Butiama na akaomba aonane na Mwalimu na mama yake. Alipoonana nao akasema

“Utakuwa ni wizi wa fadhila k**a wewe NYERERE utaendelea kumfunga T**I licha ya yote aliyokufanyia wewe, TZ na sehemu hii ya dunia. Tafadhali sana nimetumwa na wanawake wa Kenya nikuombe umwachie huru k**a yeye alivyopigania kuachiwa huru kwa JOMO KENYATTA”.

Mwalimu Julius Kambarage NYERERE alimjibu mama huyo kuwa maombi hayo ameyapokea na atayafanyia kazi. Rais NYERERE, akitumia mamlaka yake chini ya ibara ya 45 ya Katiba, alimsamehe Bibi T**I Mohammed mwezi April 1972.

Baada ya kusikia msamaha huo, Bi. T**I Mohammed hakuamini masikio yake kwani aliishaamua kupambana na hali yake na alijua angelifia gerezani. Hivyo, alipanda garimoshi kutoka Dodoma kwenda Dar es salaam akiwa na furaha tele na meno yote 32 nje.

Ndugu zake walimlaki kwa bashasha na nderemo na akaenda kuishi kwenye nyumba liyozeeka kweli ya mama yake mzazi iliyokuwa maeneo ya Temeke. Mama yake, aliyekuwa mtu mzima sana, almanusra azimie kwa mshtuko wa kumuona mwanae baada ya kutoka magereza.

Baada ya kuachiwa, T**I alienda kuishi Temeke. Maisha ya kipweke sana kwani ndugu na marafiki walimnyanyapaa: “Mtu angeweza kufikiri kwamba nina ugonjwa wa kuambukiza”. T**I akawa muda mwingi anakaa kibarazani kwao akiuza mafuta ya taa ya rejareja ili kuweza kumudu maisha!

Akiwa ofisini kwake Nairobi, Kenya tayari amesahau kuhusu Ujumbe wake kwa Nyerere, siku moja akapata habari kwamba kuna mgeni kutoka Tanzania anataka kumuona. Akaagiza apite ndani.

Alikuwa waziri wa mambo ya nje wa Tanzania, John Samuel Malecela akiwa na ujumbe kutoka kwa Nyerere “nimetumwa nije nikupe habari njema kwamba Nyerere tayari amemuachia huru T**i Mohammed Salum Mandangwa”

Baada ya kupata ujumbe huo, mwanasiasa Mwanamama huyo kuutoka nchini Kenya aliyejawa na furaha akasema: “Naomba kamwambie Mwalimu NYERERE kwa niaba ya wanawake wote wa Kenya na wananchi wa Afrika Mashariki, nasema ahsante sana kwa uungwana wake na uaikivu wake”.

Bibi T**i aliendelea kuishi maisha ya chini kabisa Temeke, mtaa wa Ngarambe, nyumba zake mbili za kisasa kabisa Upanga zilitaifishwa na Azimio la Arusha. Bibi T**i aliwekwa chini ya ulinzi fulani (semi house arrest), kutwa nzima alikuwa akikaa nje ya kibaraza chake akiuza mafuta ya taa kwa kupimia watu vibaba.

Nyumba zake Bi. T**i Mohammed alirudishiwa na Rais Mwinyi. Nyumba moja ipo mkabala na Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Hivyo, Bibi T**I akahamia nyumba ya Upanga.

Mara zote wakati akiwa uraiani baada ya kutoka gereza la Isanga, Dodoma, Bibi T**i akihojiwa na wanahabari kuhusu masuala ya kesi yake ya uhaini akiwa gerezani alikuwa akiwajibu “tumuachie Mungu” lakini alieleza kwa kirefu tu ugomvi na tofauti yake na Mwl, Nyerere.

T**i Mohammed alikuja kueleza kirefu ugomvi wake na Mwl, Nyerere katika mahojiano aliyofanya na gazeti la RAI mwaka 1994. Alisema kuanguka kwake kisiasa kulitokana na kumpinga Mwalimu Nyerere kwenye halmashauri kuu ya TANU, wakati Nyerere anatafuta kuungwa mkono na waislam ndani ya TANU baada ya kuivunja EAMWS.

T**I alifariki tarehe 5.11.2000 katika hospitali ya Net care, Johannesburg, Afrika Kusini alikokwenda kupata matibabu. Mwaka mmoja baada ya kifo cha Nyerere.

Salum Hussain Chirwa

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kanyamala Media posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Kanyamala Media:

Shortcuts

Share